LAPF yakana kumdai Mbowe Yaruka kuwasaidia Msigwa, Mbilinyi SIKU chache baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Serikali za Mitaa Tawala za Mikoa (Tamisemi), Hawa Ghasia, kusema kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amekopa kiasi cha sh bilioni moja kwenye Mfuko wa Pensheni kwa Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (LAPF), Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, Eliud Sanga, amekanusha. LAPF pia imekana kuwasaidia fedha au vifaa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na Iringa Mjini, Peter Msigwa, kama ilivyosemwa bungeni. Juzi, Ghasia alisema kuwa Mbowe anadaiwa sh bilioni moja na LAPF na ametumiwa waraka wa kumkamata ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria. Waziri huyo alisema si kosa kwa wabunge kupewa fedha na LAPF, lakini ni kosa kwa mbunge kutorejesha fedha alizokopeshwa. Kauli ya LAPF Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, Sanga, alibainisha kuwa LAPF haijawahi kumkopesha Mbowe sh bilioni moja, na kwamba mfuko huo hauna utaratibu wa kuk