Rehema Chalamila aka Ray C jana alifunguka kupitia kipindi cha Mkasi jinsi ambavyo wasanii wenzake walimtenga wakati alipokuwa amelazwa hospitali kupatiwa matibabu ya ‘uraibu’ (addiction) wa madawa ya kulevya. Ray C alisema japokuwa mama yake alitoa kwa umma mawasiliano yake na maelekezo ya namna ya kumsaidia, simu hiyo iliyokuwa busy saa 24, ilikuwa ikipokea simu na ujumbe kutoka kwa mashabiki wake pekee na sio msanii yeyote anayemfahamu. Muimbaji huyo aliyewahi kutamba na vibao vingi vikali vikiwemo ‘Niwe Nawe Milele’ Uko Wapi na Sogea Sogea, alisema hiyo ilimpa funzo kuwa mtu maarufu huwa na marafiki pale tu anapokuwa juu lakini akipata matatizo hutengwa na hata watu wake wa karibu Katika kipindi hicho pia, Ray C aligusia jinsi ambavyo Lord Eyez alimuingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya ambapo alikuwa akimchanganyia unga kwenye bangi bila ya yeye kufahamu na kwamba alifanya hivyo kwa mwaka mzima. Alisema baada ya kujigundua k