RAY C AAMUA KUWAPA LIVE WASANII WENZAKE




Rehema Chalamila aka Ray C jana alifunguka kupitia kipindi cha Mkasi jinsi ambavyo wasanii wenzake walimtenga wakati alipokuwa amelazwa hospitali kupatiwa matibabu ya ‘uraibu’ (addiction) wa madawa ya kulevya.

Ray C alisema japokuwa mama yake alitoa kwa umma mawasiliano yake na maelekezo ya namna ya kumsaidia, simu hiyo iliyokuwa busy saa 24, ilikuwa ikipokea simu na ujumbe kutoka kwa mashabiki wake pekee na sio msanii yeyote anayemfahamu.

Muimbaji huyo aliyewahi kutamba na vibao vingi vikali vikiwemo ‘Niwe Nawe Milele’ Uko Wapi na Sogea Sogea, alisema hiyo ilimpa funzo kuwa mtu maarufu huwa na marafiki pale tu anapokuwa juu lakini akipata matatizo hutengwa na hata watu wake wa karibu


Katika kipindi hicho pia, Ray C aligusia jinsi ambavyo Lord Eyez alimuingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya ambapo alikuwa akimchanganyia unga kwenye bangi bila ya yeye kufahamu na kwamba alifanya hivyo kwa mwaka mzima.

Alisema baada ya kujigundua kuwa tayari ameingia kwenye tatizo kubwa aliamua kuchukua uamuzi wa haraka wa kuachana na rapper huyo ingawa anasema alikuwa akimpenda kwa dhati.

Katika hatua nyingine, Ray C alisema hakuna mtu anayeweza kumshukuru zaidi kama Rais Jakaya Kikwete ambaye alimuelezea kuwa ni mtu mwenye moyo wa kipekee kwakuwa amemsaidia kwa hali na mali na kumtoa kutoka kwenye janga la uteja.

Aliongeza kuwa Rais Kikwete amekuwa akiwasaidia vijana wengi wenye matatizo hayo na sio yeye peke yake.

Alisema kwa sasa tayari amesharekodi nyimbo takriban 12 na watayarishaji tofauti wa muziki akiwemo Tudd Thomas na Ema The Boy na kwamba hivi karibuni ataachia wimbo wake mpya.

SOURCE: TIMES FM

Comments

Popular posts from this blog