Posts

Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal afungua mkutano wa Mabunge ya SADC mjini Arusha

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia vikundi vya sanaa vya ngoma za aina mbalimbali alipowasili katika Jengo la Ukumbi wa mikutano A I C C mjini Arusha kwa ajili ya kufungua mkutano wa siku 11 wa 34 kwa Mabunge ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC leo Octoba 20, 2013. (Picha na OMR) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mbunge wa Arusha mjini Mhe. Godbles Lema nje ya ukumbi wa mikutano wa A I C C Arusha, Baada ya kufungua mkutano wa siku 11 wa 34 kwa Mabunge ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC katika ukumbi wa A I C C mjini Arusha leo 20 Octoba 2013. Kushoto Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mbunge wa wawi kisiwani Pemba Mhe Hamad Rashid nje ya ukumbi wa mikutano wa A I C C Arusha, Baada ya kufungua mkutano wa siku 11 wa 34 kwa Mabunge ya Nchi wanac...

KATI YA HAWA MASTAA WA KIKE WANAOTINGISHA BONGO NI NANI MKALI?

Image
Wema Sepetu...I just love her voice,lips, skin tone and that caring heart Lulu Michael she knows sifa zake zote ambazo nilikuwa nampa kila siku tukiwa wote... her smile huwa linaninyong'onyeza kabisa. Ana heshima, ni mwelewa na ni Jambazi wa hisia za watu.. akiamua kuiteaka tanzania kwa hisia tu anaweza  Jackie cliff.... am sure hapa sipo peke yangu bana kwa kutokwa na udenda... look at her sexy body.... kimwili kisichokomaa!! ana akili na ni mtafutaji katika maisha.. in her Young age she is married and managed to kip her life more personal Tune to 88.4Fm utajua nini kimeniteka kwa huyu mtoto....mke wangu akikosa sauti ya Wema apewe Ya Diva Lovess love... anateka vijana wengi muda wa show yake ukifika... mahusiano yamevunjika sababu ya watu kusikiliza show yake badala ya kula chakula cha usiku na wapenzi zao TUPE MAONI YAKO, NA USISAHAU KULIKE KURASA WETU WA FACEBOOK

WASTARA AUUMIZA TENA MGUU WAKE

Image
MWANADADA anayeendesha maisha yake kwa kupitia filamu za Bongo, Wastara Juma ameumia mguu baada ya kuwekewa mwingine mpya wa bandia huko Nairobi nchini Kenya. Akizungumza na paparazi wetu siku chache baada ya kurudi Bongo, Wastara alisema aliumia wakati akifanya mazoezi ya mguu mpya aliowekewa ambapo kwa sasa anaendelea kuuguza jeraha hilo na amerudi mara moja kwa ajili ya Sikukuu ya Idd, ikimalizika atarejea tena nchini humo kwa ajili ya matibabu zaidi. “Nimeshindwa kula sikukuu mbali na watoto wangu ndiyo maana nikaja mara moja japokuwa siko vizuri kwa sababu niliumia kwenye mazoezi ya kutumia mguu mpya huko Nairobi na sasa nauguza kidonda lakini baada ya hapo nitarudi tena Nairobi kwa ajili ya matibabu,” alisema Wastara.

MTOTO WA MIAKA 14 AJIFUNGUA MAPACHA HUKO MOSHI

Image
UKISTAAJABU ya musa utayaona ya firauni ndivyo ilivyotokea kwa mtoto wa miaka miwili ambaye amejifungua mtoto. Mtoto huyo aliyefahamika kama Xiao Feng alijifungua kwa njia ya upasuaji katika hospit ali moja mjini Xuaxi nchini China. Kwa mujibu wa taarifa, madaktari waligundua kuwa mtoto Xiao alikuwa na mimba baada ya kupelekwa na mama yake. Binti wa miaka 14 akiwa na mtoto wake katika Manispaa ya Moshi.Picha ya Maktba. Awali mzazi wake huyo aligundua kuwa tumbo la binti yake lilikuwa kubwa isivyo kawaida hivyo alimpekeka hospitali kujua kulikoni. Nao matabibu hao wakafanya kazi yao ya kumpiga picha za mionzi ya jua ‘x-rays’ na kubaini mtoto huyo alikuwa amebeba mwenzake tumboni. Walimfanyia upasuaji ambao ulimalizika kwa mtoto huyo kuzaa watoto pacha

Mama mwenye UKIMWI amchukua mtoto wa jirani na kumnyonyesha maziwa yake....Serikali yamkamata na kumfunga miaka miwili jela

Image
MWANAMKE mmoja raia wa Zimbabwe aliyenyonyesha mtoto wa jirani bila ruhusa anakabiliwa na kifungo cha karibu miaka miwili kwa kumwambukiza mtu HIV kwa kukusudia kwa kuwa yeye ni mwathirika. Annie Mpariwa, 39, alifikishwa mbele ya mahakama ya Gaborone wiki iliyopita na kesi hiyo iliahirishwa hadi Oktoba 24 kuruhusu kipimo cha pili cha HIV kufanyiwa mtoto huyo. Matokeo ya kwanza ya mtoto huyo yalionyesha hana virusi ilhali ya mama huyo yalikuwa na virusi. Mpariwa alikamatwa wiki jana kwa mashtaka ya usumbufu na iwapo mtoto huyo atapatikana na virusi, mashtaka hayo yatazidishwa hadi 'kumwambukiza mtu mwingine HIV kimakusudi.’ Mama wa mtoto huyo wa miezi 14, Nyasha Mironga, alisema kumwona mwanawe akinyonyeshwa na jirani wake lilikuwa ni jambo lililomshtua sana. Kisa hicho kimetokea baada ya kupitishwa kwa sheria mpya ya HIV/Aids inayotoa adhabu kali zaidi kwa wale wanaowaambukiza wengine HIV kimakusudi

WABAMBWA WAKIFANYA MAPENZI KWENYE NDEGE

Image
skip to main | skip to sidebar Wapenzi wawili wamekamatwa kutokana na kitendo cha kufanya ngono ndani ya ndege. Kwenye shitaka lao, wawili hao walipatikana na hatia hivyo kila mmoja alitozwa faini ya $250 kutokana na kitendo hicho kilichotokea wakati ndege hiyo ilipokuwa inatoka Medford, Ore., kwenda Las Vegas. Wapenzi hao walitozwa faini hiyo mnamo June 21, huku ikielezwa, abiria walishuhudia mwanaume aitwaye Christopher Martin, akijiachia kwa raha zake kwa kufanya mapenzi na mwenza wake aitwaye Jessica Stroble, licha ya onyo lililotolewa na wafanyakazi wa ndege hiyo wenza hao waliendelea kufanya yao. Baadaye Martin aliomba msamaha kwa wale walioumizwa au kukwazwa kutokana na kitendo hicho.  

Julius Nyaisanga (Mtangazaji wa zamani Radio One na Mkurugenzi wa Abood Media) afariki dunia

Image
Aliyekua mkurugenzi wa Abood media bwana Julius nyaisanga,amefariki dunia huko Morogoro katika hospitali ya Mazimbu... Marehemu aliwahi pia kufanya kazi katika kituo cha Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na katika Kituo cha Redio One ambapo alikuwa Mkurugenzi. Mpaka sasa chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika japo marehemu alikuwa akiugua kwa muda mrefu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN! BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

Ndugu wataka mtoto auawe ili kutoa UCHURO katika familia hiyo......Ni mkasa wa kutisha sana....

Image
MTOTO aitwaye Mwajuma Haji (16) ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili anayesumbuliwa na ugonjwa wa kusinyaa kwa viungo yuko katika hali mbaya baada ya baadhi ya ndugu kudaiwa kutaka auawe ili kutoa uchuro katika familia. Kwa mujibu wa mama mzazi wa mtoto huyo, Tatu Musa baadhi ya ndugu (siyo wote) wamekata tamaa ya kumuuguza mtoto huyo na kupendekeza heri mtoto huyo akatishwe maisha yake. “Mwanangu haumwi wala hajawahi kuumwa ila ghafla alianza kusinyaa na kukosa nguvu, kinachoniuma baadhi ya ndugu zangu wamekata tamaa wanataka wamuue, waniachie mwanangu,” alisema mama huyo huku akilia mfululizo. Mwandishi wetu amemshudia mtoto huyo akiwa amesinyaa viungo kiasi cha kutoweza kufanya kitu chochote zaidi ya kulala. Mama mzazi wa mtoto huyo alisema kuwa alijifungua mtoto huyo akiwa na afya njema lakini alipofikisha umri wa miaka mitatu hali ikabadilika na viungo vyake kuanza kusinyaa. Mama huyo amedai kwamba kutokana na hali hiyo hakuweza...

TATIZO LA HARUFU MBAYA UKENI LIJUE VYEMA NA NJIA ZA KULIKABILI

Image
Tatizo la uchafu ukeni Leo tutazungumzia tatizo linalowasumbua wanawake wengi, tatizo la kutokwa na uchafu unaotoa harufu mbaya sehemu za siri. Kitaalamu hali ya mwanamke kutokwa na majimaji yenye rangi nyeupe au ya njano, ni hali ya kawaida na wala siyo tatizo endapo majimaji hayo siyo mazito sana na wala hayatoi harufu mbaya. Lakini endapo majimaji yanayotoka yapo katika hali ya ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia, yanatoa harufu kali na yanawasha, basi hiyo ni ishara ya ugonjwa uitwao Vaginosis. Majimaji au ute unaoteleza kutoka sehemu za siri ni njia inayowezesha viungo vya uzazi vya mwanamke kujisafisha na kuutoa uchafu wa seli zilizokufa na mabaki ya damu ya hedhi nje ya mwili. Pia huvikinga viungo vya uzazi dhidi ya maambukizi ya bacteria au fangasi wanaoleta magonjwa. Kwa kawaida huwa hayatoi harufu na huwa na rangi nyeupe au ya njano. Pia huwa na asidi ya Lactic ambayo huzuia kuzaliana kwa vijidudu vya maradhi na huzalishwa kwenye tezi z...

MCHUNGAJI ADAI KUWAUA SHARO, KANUMBA

Image
Mwanaume aliyetambulishwa kwa jina la Mchungaji Mayanga amewashangaza waumini baada ya kudai kanisani kuwa yeye ndiye aliyewaua mastaa wawili Bongo, Hussein Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ na Steven Kanumba ‘The Great’. Mchungaji Mayanga (mwenye kipaza sauti) akitoa ushuhuda. Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita ya Oktoba 13, mwaka huu, huko Mzambarauni, Mbagala-Charambe jijini Dar katika Kanisa la Powerful Gospel Ministry lilipo chini ya Mchungaji Meshak Punkanya ambapo Mayanga alipewa nafasi ya kutoa ushuhuda. VIFO MILIONI 605 Mchungaji huyo alielezea kujuta kwake mbele ya kanisa kwa kudai kuwa kabla ya kuokoka alikuwa mchawi mkubwa aliyeishi kuzimu na kufanya kazi za mauaji sambamba na shetani mkuu (Lusifa) kwa kuwatumia vibaraka wake na majini. Mchungaji Mayanga alikiri kutekeleza vifo vya watu wapatao milioni 605 wakiwemo waigizaji hao. Steven Kanumba. WAMO FIVE STARS, MTOTO WA DANDU Alisema kuwa kati ya watu aliowaua kwa njia za kishirikina wamo waimbaji wa Taarab w...

LULU AELEZEA MIPANGO YA KUOLEWA KWAKE

Image
STAA wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekataa kabisa suala la kuolewa kwa sasa akidai moyo wake haupo tayari kwa tendo hilo. Lulu alifunguka hayo Jumatatu iliyopita katika kipindi cha Mkasi kinachorushwa kupitia Runinga ya East Africa ambacho humpa nafasi staa kuzungumzia mambo mbalimbali yanayohusu maisha yake na sanaa kwa jumla. Wakati mahojiano hayo yakiendelea, mmoja wa watangazaji wa kipindi hicho anayefahamika kwa jina la Muba, alimtupia Lulu swali ambalo lilimtaka aeleze utayari wake endapo mtu akijitokeza na kutaka kumuoa. “Sitaki kuolewa kwa sasa, muda wa kuolewa haujafikia. Ukifika nitafanya hivyo lakini kwa sasa sipo tayari kuolewa,” alisema Lulu. Aidha, Lulu alikiri kuwa licha ya kutokuwa tayari kuolewa lakini amekuwa akipata usumbufu mkubwa wa kutongozwa na wanaume. Aliainisha kuwa alikuwa akitongozwa kabla na baada ya kutoka Segerea alipokuwa akishikiliwa kwa kesi ya kifo cha aliyekuwa mpenzi wake, marehemu Steven Kanumba. “Watu wanan...

Mwanaume akatwa Uume wake na mwanamke aliyemvamia kwa lengo la Kumbaka...Bofya hapa ujionee

Image
Hii ni stori fupi ya mwanaume aliyekatwa uume wake na mwanamke ambaye alimwingilia kwa lengo la kumbaka... Taarifa toka eneo la tukio nchini Kenya zinaarifu kuwa mbakaji huyo alimvamia mwanamke huyu majira ya saa nane usiku kwa kuvunja dirisha na kisha kuingia ndani huku akiwa amejihami kwa kisu kikali... Alipoingia ndani, alimvaa mwanamke huyu ambaye ni mke wa mtu ( mumewe alikuwa safarini ) na kuanza kumkaba kwa lengo la kufanya naye mapenzi huku akimtishia kumchoma kisu endapo atapiga kelele... Mwanamke hakuwa na jinsi, ilibidi akubaliane naye ili kuunusuru uhai wake.Wangali wakiwa katika tendo huku jamaa akiwa amenogewa, yule mwanamke alimgeuza kwa ujasiri na kufanikiwa kuviminya VIAZI MVINGO VYA MWANAUME... Baada ya kuviminya viazi mviringo ( Korodani ), yule kaka hakuwa na jinsi na ndipo mwanamke yule alipoitumia nafasi ile kuikata MAMBO (Mhugo ) ya ...

CHADEMA yamwaga nyaraka za siri kumjibu Zitto Kabwe...Yawataka Msajili wa vyama na CAG wawajibike

Image
Hii ni taarifa ya Chadema: Kutokana na taarifa zilizotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali kuwa vyama vya siasa ambavyo vinapata ruzuku kutoka serikalini havijawasilisha taarifa yake ya mapato na matumizi kwa ajili ya kufanyiwa ukaguzi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa kipindi cha miaka minne mfululizo, yaani kuanzia mwaka 2009/2010- 2012/2013. CHADEMA tunapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo juu ya taarifa hizo; i. Kuwa taarifa hizo sio sahihi na hazina ukweli kuhusiana na CHADEMA labda kwa vyama vingine, hii ni kutokana na ukweli kuwa tulishawasilisha taarifa zetu za fedha kwa msajili wa vyama vya siasa na zilizokaguliwa kwa mwaka wa fedha 2010/2011, 2011/2012 na hili linathibitishwa na barua ya msajili wa vyama vya siasa yenye Kumb.Na . CDA.112/123/01a/37 , ya tarehe 04 september 2012. Iliyopelekwa kwa makatibu wakuu wa vyama vyote vya siasa (nakala imeambatanishwa). Aidha, hesabu za mwaka wa fedha zilizokaguliwa za 2009/20...

Mwanamke akatwa mguu na Mume wake huko tarime ....Kosa lake ni kuchelewa kumfungulia mlango mumewe

Image
Ghati Chacha (21) mkazi wa kijiji cha Nyanitira kata ya Nyansincha Wilayani Tarime amesababishiwa kilema cha maisha kwa kukatwa mguu wake wa kulia na Mume wake baada ya kuchelewa kumfungua mlangao nyakati za usiku na hivyo kumfanya aamini kuwa alikuwa na mwanaume mwingine ndani. Akisimulia mkasa huo huku akiwa wodi namba sita alikolazwa akiuuguza vidonda na majeraha,Ghati alisema, mume wake aliye mtaja kwa majina ya Chacha Mwita (23) alifika nyumbani saa mbili usiku akiwa amelewa. "Aliniuliza kwa nini nimechelewa kumfungulia mlango nikamjibu sikuwa nasikia .Akaaza kunifokea kwamba nilikuwa na mwanaume mwingine ndani , baadaye akaniomba kurunzi na panga, nikamletea kurunzi na kumwonesha panga lilipo kwa kidole" alisema Ghati. Wakati anamwonesa lilipo panga na kumpa kurunzi Ghati hakujuwa nini kinafuata , alifikiri kuwa ni mambo ya wanaume tu, pengine anataka kwenda sehemu kwa kuwa ndizo tabia za wanaume wa maeneo haya kuondoka u...

Picha tano za dada yetu UFOO SARO baada ya kunusurika kuuawa na Mpenzi wake

Image
Ufoo Saro baada ya kufanyiwa upasuaji huo. Muuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), akimpeleka wodini Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufo Saro, baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondolewa risasi kufuatia kushambuliwa kwa silaha ya moto nyumbani kwa mama yake Kibamba jijini Dar es Salaam leo na mchumba wake ambaye pia alimuua mama yake na kisha kujiua. Wanahabari wakimpiga picha Ufoo Saro baada ya kuondolewa chumba cha upasuaji. Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakimsindikiza Ufoo Saro wakati akipelekwa wodini.

BAADHI YA PICHA ZA DIAMOND ZINAZOMTESA PENNY HIZI HAPA

Image
Baada ya habari kuenea kuwa Diamond PLatnumz amerudiana na Wema walipokuwa Malaysia katika moja ya show zake na Platnumz kukanusha habari hiyo kupitia website yake, hatimaye BK imepata picha nyingi za Diamond na C.E.O wa Endless Fame Wema Sepetu wakiwa kwenye pozi tofauti tofauti za kimahaba nchini humo. Baadhi ya picha hizo, moja inawaonesha Diamond na Wema wakiwa wamevaa Mapajama (nguo za kulalia) sehemu kama hotelini hivi na nyingine ikimuonesha Diamond akim-kiss Wema wakiwa kitaa .   Lakini Diamond ni real boyfriend wa Penny…

GARI YATEKETEA KWA MOTO MBELE YA ASKARI WA USALAMA BARABARANI

Image
Gari aina ya HIACE inayofanya safari zake mkoani kilimanjaro katika root ya Moshi-Marangu kila siku, Juzi asubuhi tarehe 13/10/2013 Majira ya saa mbili asubuhi iliwaka moto maeneo ya YMCA ikiwa inatokea Marangu na abiria wapatao 18, ila hakuna madhara kwa abiria. Ikiwa katikati ya mji kabisa pasipo kuwa na msaada wa haraka kutoka FIRE iliyojirani na eneno la tukio na hata msaada wa  askari wanaosaidia katika maeneo hayo, kwa mujibu wa Mwanahabari wetu FRANK aliyeshuhudia tukio ilo, hapakuwa na msaada wa haraka toka FIRE mpk baada ya dakika kadhaa kuteketea kwa gari hilo ndio walipokuja kusaidia.  Askari wa barabarani wakigeuka kuwa waandishi wa habari na kusahau majukumu yao kama wanavyoonekana  hapa askari wakiwa wanajadili jambo mara baada ya kutokea ajali hiyo katika maeneo wakiwa na mashuhuda mbalimbali hapa ni FIRE mara baada ya kufika na kukuta gari likiteketea walianza kuzima moto katika gari hilo kama wanavyoonekana. NGUDU WANANCHI PANAPOTOKE...