Mwanamke akatwa mguu na Mume wake huko tarime ....Kosa lake ni kuchelewa kumfungulia mlango mumewe



Ghati Chacha (21) mkazi wa kijiji cha Nyanitira kata ya Nyansincha Wilayani Tarime amesababishiwa kilema cha maisha kwa kukatwa mguu wake wa kulia na Mume wake baada ya kuchelewa kumfungua mlangao nyakati za usiku na hivyo kumfanya aamini kuwa alikuwa na mwanaume mwingine ndani.

Akisimulia mkasa huo huku akiwa wodi namba sita alikolazwa akiuuguza vidonda na majeraha,Ghati alisema, mume wake aliye mtaja kwa majina ya Chacha Mwita(23) alifika nyumbani saa mbili usiku akiwa amelewa.

"Aliniuliza kwa nini nimechelewa kumfungulia mlango nikamjibu sikuwa nasikia.Akaaza kunifokea kwamba nilikuwa na mwanaume mwingine ndani , baadaye akaniomba kurunzi na panga, nikamletea kurunzi na kumwonesha panga lilipo kwa kidole" alisema Ghati.


Wakati anamwonesa lilipo panga na kumpa kurunzi Ghati hakujuwa nini kinafuata , alifikiri kuwa ni mambo ya wanaume tu, pengine anataka kwenda sehemu kwa kuwa ndizo tabia za wanaume wa maeneo haya kuondoka usiku ama anataka kuangalia mji kama uko sawa alafu arudi kulala.

" Alipoipata ile panga akaniambia leo atamitumbua utumbo, akaanza kunipiga kwa panga ile akanijeruhi sikio, mkono wa kushoto na mguu wa kushoto na kunikata mguu wa kulia ukakatika kama unavyoona" alieleza kwa masikitiko akiifunua kanga iliyokuwa amejifunika akiwa amelala kitandani hospitali ya Wilaya Tarime.

Wakati anafanyiwa ukatili huo alipiga kelele lakini majirani hawakuwahi kufika kumsaidia kwa kuwa ni kawaida ya mume na mke kugombana na vilio kama hivyo kusikika katika maeneo hayo.

"Baadaye walikuja na aliposikia majirani wamefika alikimbia kwa kupitia mlango wa nyuma akitumia baisikeli yake, majirani walinifunga mguu uliokuwa ukivuja damu na kunikimbiza katika kituo cha afya Muriba na baadaye kuletwa hapa" alieleza .

Jeshi la polisi baada ya kupata taarifa lilifika lilifika eneo hilo la tukio na kushuhudia kipande cha mguu kama inavyoonekana kwenye picha hapa na kuamru kizikwe na juhudi za kumtia nguvuni kuanza.

Hata hivyo siku moja baadaye Chacha Mwita alikamatwa na jeshi la polisi kwa kusaidiana na nguvu za wananchi ambapo alifikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Tarime kujibu mashitaka hayo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamishina masaidizi wa polisi kanda maalumu ya Tarime (ACP) Justus Kamugisha lisema kuwa baada ya kuhojiwa , Mwiata alikiri kumsababishia mke wake ukilema wa maisha.

" Vitendo vya kikatili vilishapitwa na wakati, kumsababishia mtu ukilema wa maisha nii jambo lisilo la utu na linaonesha kuwa hakuna ubinadamu kwa watu japo si wote" alisema Kamugisha kwa nija ya simu.
JE UKATILI HUU UTAKOMA LINI? TUPE MAONI YAKO

Comments

Popular posts from this blog