Waliopanda mbegu DECI hatarini kutolipwa
WATEJA wa Kampuni ya DECI waliopanda mbegu, wanaweza wasilipwe fedha zao, MTANZANIA Jumatatu limebaini. Wateja hao ambao wanaidai kampuni hiyo Sh bilioni 39.27, huenda wasilipwe fedha zao kwa kuwa mchezo wa upatu hautambuliki kisheria. Utata huo ulijulikana mwishoni mwa wiki, baada ya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndullu, kuzungumza na MTANZANIA Jumatatu. "Kwanza kabisa, niseme tu kwamba hadi sasa hatujapata nakala ya hukumu hiyo ili kujua inatuelekeza nini kuhusu mchakato wa kuwalipa hao waliopanda mbegu. "Tukipata hukumu hiyo, ndiyo tutaisoma na kufahamu tumepewa jukumu gani na gharama zitalipwa na nani katika kutekeleza mchakato huo. "Sisi tunataka tujue hiyo hukumu inamaanisha nini, maana kwa kawaida anayechezesha na anayecheza upatu wote wana makosa, sasa utamlipaje aliyecheza? "Lakini, kwa kuwa hatujaiona hiyo hukumu, hatujui imetuelekeza nini, lakini i