Obama ataka bunge liamue kuhusu Syria;

bungeobama_e4086.jpg
Kwa muda wa zaidi ya wiki sasa , Ikulu ya Marekani ya White House imekuwa ikielekeza mashambulizi yake kuelekea kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Syria. Lakini hayo yamebadilika rais Obama anataka sasa bunge liamue.
Uamuzi wa Rais Barack Obama wa ghafla badala yake wa kuomba ruhusa ya bunge unamuweka katika hatari ambayo inaweza kuharibu hali yake ya kuaminika iwapo hakuna hatua itakayochukuliwa kujibu shambulio la silaha za kemikali ambalo limekiuka kile binafsi alichosema kuwa ni kuvuka "mstari mwekundu".
Bunge la Marekani halijatatua karibu chochote cha maana tangu mwaka 2010, likishindwa kukamilisha kile ambacho hapo kabla kilikuwa wajibu wa msingi kwa masuala ya barabara , shule , mashamba na masuala ya mawasiliano nchini Marekani.
Kuomba ruhusa ya baraza la wawakilishi ambalo linadhibitiwa na chama cha Republican pamoja na baraza la seneti linalodhibitiwa na chama chake cha Democratic kukubali kuchukua hatua za kijeshi , suala ambalo tayari lina utata ndani na kati ya vyama hivyo , inaingiza hali nyingine ya kutokueleweka kuhusiana na jibu la Marekani katika mzozo wa Syria.
Uwezo wa rais
Mabadliko hayo ya ghafla pia yanazusha maswali juu ya uwezo wa rais wa maamuzi na inaweza kuwafanya viongozi wa Syria, Iran, Korea ya kaskazini na kwingineko , kuwa na kichwa kigumu , na kusababisha wapate hisia kuwa rais wa Marekani hayuko tayari kuchukua hatua pale anaposema anaweza kufanya hivyo.
Bunge la Marekani hata hivyo halitaanza vikao hadi Septemba 9, kwa hiyo alama ya kuuliza itaendelea kuwepo katika sera za Marekani kuhusu suala la Syria kwa muda wa wiki, huku kukiwa na hisia kali pamoja na huenda mijadala yenye mvutano.
Hakuna mtu ambaye analijua baraza hilo la Congress vizuri ambaye alikuwa tayari kutabiri kwa uhakika kile kinachoweza kutokea katika azimio la kuiruhusu nchi hiyo kuishambulia Syria. Hali hiyo ya kutokuwa na uhakika inazidishwa mara nyingi na uhusiano mbaya na wa mbali wa Obama na bunge la Marekani.
Mwandishi : mjengwa

Comments

Popular posts from this blog