DALADALA YANUSURIKA KUINGIA BUCHANI MWENGE
Daladala lenye namba za usajili T 741 AEG baada ya kuhama njia na kuparamia mtaro uliopo jirani na bucha eneo la Mwenge. Daladala lenye namba za usajili T 741 AEG linalofanya safari zake kati ya Temeke na Mwenge asubuhi hii nusura liingie katika bucha iliyopo maeneo ya Mwenge jijini Dar katika barabara iendayo Afrika Sana. Daladala hilo lilisaidiwa na mtaro uliopo mbele ya bucha hiyo baada ya dereva wake kushindwa kuliongoza na kuhama barabara. Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa eneo la tukio, daladala hilo halikuwa na abiria na hakuna mtu aliyejeruhiwa. JIUNGE NASI KWA KUBOFYA LIKE FACEBOOK PAGE KWA HABARI MOTO MOTO