RAGE: MKUTANO MKUU SIMBA AGOSTI 20



rage-11 672e1
WEKUNDU wa Msimbazi Simba “Taifa kubwa” wanatarajia kufanya mkutano mkuu wa wanachama Agosti 20 mwaka huu jijini Dar es salaam ili kujadili mambo mbalimbali yahusuyo maendeleo ya klabu hiyo.

Mwenyekiti wa klabu ya Simba ambaye ni mbunge wa Tabora mjini, Alhaji Ismail Aden Rage amesema kwa kawaida mkutano huo ulitakiwa kufanyika Agosti 5 kwani mwaka jana ulifanyika tarehe hiyo, lakini wamelazimika kusogeza mpaka tarehe tajwa ili kuepukana na mwezi mtukufu wa Ramadhan. (HM)
Rage alisema katika mkutano wa mwaka huu kutakuwa na ajenda mbalimbali ambazo zitajadiliwa na wanachama halali wa klabu hiyo.

Mwenyekiti huyo alisema ajenda ya kwanza itakuwa ni kujadili taarifa ya ukaguzi wa fedha za klabu, na baada ya kujadiliwa kwa ajenda hiyo, watajadili ya pili ambayo ni mipango endelevu ya klabu hiyo.
Rage aliendelea kueleza kuwa ajenda ya tatu ni Taarifa ya klabu itakayosomwa na katibu mkuu Evodius Mtawala, baada ya hapo wanachama watachangia, huku hotuba ya mwenyekiti ikifuatia na hatimaye kufungwa kwa mkutano huo.
Rage aliwataka wanachama wa Simba kujiandaa na mkutano huo ambao utakuwa chachu ya mafanikio ya klabu yao ikiwemo kutwaa ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu ujao.
Ili kufanikisha mkutano huo, leo hii wadhamini wakuu wa klabu hiyo, Kampuni ya bia ya TBL kupitia kinywaji chake cha bia ya Kilimanjaro, wamekabidhi shilingi milioni 20 kwa uongozi wa Simba ikiwa ni sehemu ya udhamini wao.
Akiongea wakati wa makabidhiano hayo, meneja wa TBL, George Kavishe alisema wao wanajipanga kuendeleza klabu ya Simba chini ya mwavuli wa udhamini wao, hivyo wanawatakia mkutano mwema wekundu hao wa Msimbazi Simba wenye makazi yao mitaa ya Msimbazi Kariakoo jijini Dar es salaam. Chanzo: Baraka Mpenja

Comments

Popular posts from this blog