RAIS KIKWETE AWATUNUKU KAMISHENI MAAFISA WA JWTZ CHUO CHA MAFUNZO YA KIJESHI MONDULI, LEO
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiingia katika uwanja wa gwaride wa Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, Arusha, tayari kwa kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ leo Julai 13. Pamoja naye ni Mkuu wa Chuo hicho Meja Jenerali V.K. Mritaba. Jumla ya wahitimu 205, wakiwemo wanawake 25, wametunukiwa kamisheni na kuwa Luteni Usu, ambapo wahitimu wawili ni wa kutoka Uganda na Visiwa vya Shelisheli. Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride katika Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, Arusha, kabla ya kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ leo. ZAIDI BOFYA HAPO CHINI Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi Ofisa Kadet Ngodoke kwa kuibuka mwanafunzi bora wa jumla mwaka huu katika Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Mondu...