HUYU ndo MWANAJESHI ALIYEKAMATWA NA JINO LA TEMBO ANGALIA PICHA



Mwanajeshi anayesadikiwa kukutwa na jino la Tembo akiwa chini ya ulinzi pamoja na kidhibiti chake, huyu alitegemewa kuilinda Nchi lakini .
(Picha na maktaba)


Alitaka kuingia Malawi, apandishwa kizimbani

OFISA Uvuvi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Suleiman Chesana, anayekabiliwa na kesi ya kukutwa na meno ya tembo yenye thamani ya Sh bilioni nne, amepandishwa tena kizimbani baada ya kukutwa na meno mengine ya tembo kilo 781 yenye thamani ya Sh bilioni 9.3.

Mshtakiwa huyo, alipandishwa tena kizimbani jana kwa mara nyingine katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mjini Dar es Salaam, mbele mbele ya Hakimu Sundi Fimbo na kusomewa mashtaka na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka.
Kweka alidai kosa la kwanza ni la kujishughulisha na nyara za Serikali bila kibali, kinyume na Sheria ya Uhujumu Uchumi.
Ilidaiwa Mei 23, mwaka huu, katika mpaka wa Malawi na Tanzania, mtuhumiwa alikamatwa akisafirisha isivyo halali nyara zenye thamani ya Sh bilioni 9.3, zikiwa zimefichwa katika mifuko ya saruji, wakidai wanasafirisha saruji.

Comments

Popular posts from this blog