MWANACHUO WA MWAKA WA KWANZA ALAANI KITENDO CHA KUPIGWA "EXILE" NA MADENTI WENZIE
Vitendo vya wanafunzi kupigana exile ( kumpisha room ili angonoke na mpenzi wake ) vimekuwa vikishika kasi ya ajabu katika hosteli za wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali ambao kwao limekuwa ni jambo la kawaida...!! Hali imekuwa ni tofauti kidogo kwa mwanafunzi wa chuo kimoja hapa nchini ambaye yuko mwaka wa kwanza na anategemea kuingia mwaka wa pili. Akiongea na mtandao huu kwa sharti la kutotajwa jina , mwanafunzi huyo amefunguka na kudai kuwa Exile imemuathiri sana kisaikolojia.Imemfanya aishi kama mtumwa huku taaluma yake ikiyumba kwa kasi. Hili ni simulizi la mwanafunzi...