Posts

YANAYOENDELEA MUDA HUU KATIKA VIWANJA VYA LEADERS KWAAJILI YA WATANZANIA KUTOA HESHIMA YA MWISHO KWA DADA YETU RACHEL HAULE

Image
 Mchungaji akiendesha Sala kwaajili ya Marehemu Rachel Haule ambaye alipoteza maisha Jumatatu ya Wiki Hii kwa Uzazi  Sehemu lilipo Jeneza lenye Mwili wa Mpendwa Wetu Rachel Haule   Baadhi ya waombolezaji waliofika katika viwanja vya leaders kwaajili ya kutoa heshima za mwisho kabla Mwili wa Marehemu Rachel haujapelekwa kupumzishwa katika Nyumba yake ya Milele MChungaji akiendelea kutoa Neno katika Msiba wa Msanii Rachel Haule aliyefariki Jumatatu, Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuagwa muda si mrefu katika viwanja hivi vya leaders na hatimaye kwenda kupumzishwa kwa amani katika Makaburi ya Kinondoni.Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog. Picha Zaidi zitakujia Baadae

WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU HAWA GHASIA AUMBUKA KUTOKA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI.

Image
LAPF yakana kumdai Mbowe Yaruka kuwasaidia Msigwa, Mbilinyi SIKU chache baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Serikali za Mitaa Tawala za Mikoa (Tamisemi), Hawa Ghasia, kusema kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amekopa kiasi cha sh bilioni moja kwenye Mfuko wa Pensheni kwa Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (LAPF), Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, Eliud Sanga, amekanusha. LAPF pia imekana kuwasaidia fedha au vifaa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na Iringa Mjini, Peter Msigwa, kama ilivyosemwa bungeni. Juzi, Ghasia alisema kuwa Mbowe anadaiwa sh bilioni moja na LAPF na ametumiwa waraka wa kumkamata ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria. Waziri huyo alisema si kosa kwa wabunge kupewa fedha na LAPF, lakini ni kosa kwa mbunge kutorejesha fedha alizokopeshwa. Kauli ya LAPF Mkurugenzi Mkuu wa mfuko  huo, Sanga, alibainisha kuwa LAPF haijawahi kumkopesha Mbowe sh bilioni moja, na kwamba mfuko huo hauna utaratibu wa kuk

HALIMA MDEE AMLIPUA PROF TIBAIJUKA

Image
Adai anamiliki maelfu ya ardhi hapa nchini Wabunge wamshambulia, Makinda amuokoa CCM waitisha kikao cha dharura kumnusuru MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (CHADEMA), amemlipua Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, kwamba anamiliki maelfu ya ekari za ardhi katika maeneo mbalimbali nchini. Mdee ambaye ni Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alirusha kombora hilo jana bungeni wakati akisoma maoni ya kambi hiyo kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka wa fedha 2014/2015. Makombora hayo ya Mdee, yalimfanya Waziri Tibaijuka, kutumia muda mrefu zaidi kujibu mashambulizi badala ya hoja za wabunge wakati akihitimisha hoja yake. Majibu hayo yalimfanya Spika wa Bunge, Anne Makinda, kila mara kumtaka Waziri Tibaijuka ajibu hoja za wabunge badala ya kujikita kumjibu Mdee, katika masuala yanayoonekana ni binafsi. Waziri Tibaijuka, alisema kuwa Mdee amekuwa bingwa wa kuiba siri za serikali ikiwemo mwaka jana k

Vilio vyatawala nyumbani kwa marehemu Recho Haule baada ya mwili huo pamoja na wa mwanaye kuletwa toka Muhimbili

Image
Mwili wa marehemu Recho aliyekuwa msanii wa bongo muvi na mwili wa mtoto wake umetolewa katika hospitali ya taifa muhimbili na kupelekwa nyumbani kwao maeneo  ya  Palestina jijini Dar , na baadaye viwanja vya leaders club kwa ajili ya kuagwa Simanzi  na  vilio  vilitawala nyumbani kwa marehemu  wakati  mwili  huo  ukiagwa  na  ndugu wa karibu kwa dakika chache kabla  ya  kwenda viwanja vya leaders    

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AWASILI WILAYANI BABATI LEO, AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI MANYARA

Image
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ukivuka katika mto Magara mapema leo asubuhi kuelekea wilayani Babati mkoani Manyara. Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi,siasa na Uenezi Nape Nnauye,wakiwa kwenye ziara ya siku saba ya kukagua kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Chama,kukagua maandalizi ya uchaguzi ya serikali za mitaa,kusikiliza kero za wananchi na kuzitafututia ufumbuzi. Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Magara wakivuka mto Magara wakielekea shuleni mapema leo asubuhi,Mto huo umekuwa na changamoto kubwa kwa wakazi wa maeneo hayo,wakati wa Masika kwa kukosa daraja la kuvukia kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine,daraja hilo ndilo linalotenganisha Wilaya ya Mbulu na Babati mkoani Manyara. Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Magara baada ya kumsimamisha katika mto Magara wakitaka kujengwa daraja katika mto huo litakalounganisha Wilaya ya Mbu

Mrembo Anaswa Kavaa Nguo za Marehemu Adamu Kuambiana, Afunguka Yote

Image
Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya AMA kweli duniani kuna sarakasi! Takribani siku kumi tangu alipofariki dunia aliyekuwa ‘kichwa’ kwenye filamu za Kibongo, Adam Phillip Kuambiana (38), mrembo aliyejitambulisha kwa jina Mary Njombe amenaswa na nguo za staa huyo wakati mali za marehemu hazijagawanywa. Kwa mujibu wa vyanzo vyetu makini, Mary ambaye ni mkazi wa Magomeni Hospitali, Dar amekuwa akipigilia pamba za marehemu hasa baada ya jamaa huyo kutangulia mbele ya haki. “Jamani njooni huku Magomeni Hospitali hapa mtaa wa pili kuna mwanamke anatinga nguo za marehemu Kuambiana,” kilisema chanzo chetu. Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, wanahabari wetu walifanya msako eneo hilo hadi wakamnasa Mary. Katika mahojiano na gazeti hili, Mary alisema kuwa alikuwa mchumba wa Kuambiana na alichobahatika kubaki nacho ni nguo ambazo alimpatia mara ya mwisho amfulie (zinaonekana pichani). Mary alisema kuwa yeye na Kuambiana walifahamiana tangu mwaka 2006 ambapo alikuwa aki

Mlela Kuoa Mwanamke Aliyemzidi Umri

Image
STAA wa filamu Bongo, Yusuf Mlela ametoa kioja cha aina yake baada ya kufunguka kuwa akifika hatua ya kuingia kwenye ndoa anataka mwanamke atakayemzidi umri. Tofauti na vijana wengine ambao wanapenda kuoa wake wadogo kwao, Mlela alisema anaamini mwanamke akimzidi umri ndoa itadumu na maisha yao yatakuwa mazuri kwani atakuwa tayari ameshakomaa kiakili na atakuwa na uwezo mkubwa wa kuiendesha familia. “Nahitaji mwanamke anayenizidi umri na sitaki nimzidi mimi naamini huyo tutaelewana na ndoa itadumu, sitaki mwanamke ninayemzidi umri mimi maana itakuwa shida kwani sijapangilia hivyo,” alisema Mlela. Na Gladness Mallya

Hata Wema Atembee Peku Posta, Hawezi kumfikia Vanessa Mdee kwa Hili.

Image
Ukiongelea watu maarufu hapa town, ni wazi kwamba Wema ndiye maarufu zaidi kuliko celebrity yeyote yule wa kike hapa bongo, cause kila rika linamjua Wema Sepetu, na haswa vijana wengi wa kike hutokea kumpenda sana Diva huyu, ila tukienda kwa level zakimataifa hapo kidogo ndio utata unapokuja haswa ukilinganisha na presenter maarufu hapa town na mwanamuziki mkali wa Come Over yaani Vanessa Mdee. Haina budi tukubaliane na ukweli kwamba, yuko famous zaidi ki-international zaidi kuliko mtu mwingine anavyodhani kwa mtazamo wa haraka haraka hapa Bongo. Vanessa ni moja ya msanii wa kike ambaye mbali tu na umaarufu wake huo kimataifa bali, ana ule muonekano wa ki-star, kitu ambacho ni nadra sana kukipata kwa wasanii wengi hapa Bongo, ila tukirudi kwa Wema Sepetu ambaye ndiye ana-run industry ya watu maarufu hapa Bongo , upande wa wanawake, ukilinganisha na Vanessa Mdee bado jibu utapata kuwa Vanessa ndie anayekimbiza kwa upande wa muonekano wakistar na umaarufu wa kimataifa

MAMBO 6 AMBAYO WANAUME HAWAPENDI KUFANYIWA NA WENZI WAO

Image
Haya niliyapata kutoka kwa mshauri wa masuala ya mahusiano, ndoa na vijana Frederick Kyara. Hizi ni baadhi tu nakuwekea hapa japo kuna vitu pia wanawake hawavipendi kutoka kwa wenzi wao wanaume. Nayo ni haya hapa, ungana nami kujadili jambo hili ambalo kwangu nimeona ni changamoto au niseme sikujua.  1. Wanaume hawapendi kuambiwa cha kufanya na wenzi wao Mwanamke unapotaka mwanaume afanye jambo usimwambie alifanye bali fanya kama una mpa ushauri.  Mfano ..... hivi kwa nini tusiweke balbu hapa kwenye korido maana kuna giza kweli. Badala ya hivi wewe ...... huoni hapa kwenye korido kuna giza balbu imeungua mwezi sasa hujabadilisha kwa nini? Weka balbu bwana. Atafanya au asifanye kabisa kwa sababu umemwambia cha kufanya.  2. Wanaume hawapendi mwenzi mwenye makelele, mlalamishi Yeye ni kulalamika kuanzia Jumatatu hadi Jumapili. Japo wanawake nao wanasema kuna wanaume walalamishii balaaa. Na wenye gubu wanasusa kula mpaka kuongea wanawanunia wake zao mmmmh!   3

CHEKI PICHA MAMBO YALIVYOKUWA KWENYE PARTY YA WASANII WA BONGO MOVIE DAR LIVE FULL BURUDANI

Image
Kundi la Scorpion Girls likiongozwa na Isabela Mpanda (katikati) likiporomosha burudani wakati wa  Tamasha la Usiku wa Mastaa wa Filamu lililofanyika Dar Live usiku wa kuamkia leo . Mrembo Jacqueline Wolper akiwapa 'hi' mashabiki. Jacob Steven 'JB' akionyesha umahiri wake wa kusakata rhumba wakati wa tamasha hilo. Steve Nyerere naye akionyesha manjonjo yake stejini. Mastaa wa filamu wakiwa jukwaani kuwasalimia mashabiki waliofurika ndani ya Dar Live. Snura Mushi akiwapagawisha mashabiki. Msanii Afande Sele akiwarusha mashabiki ndani ya Dar Live. Tundaman akiwachizisha mashabiki. ...akizidi kuwapa raha mashabiki. Kingwendu akifanya vitu vyake. Richie naye akionyesha ufundi jukwaani. Dk. Cheni na mwanadada wakienda sambamba. Shamsa Ford akisema na mshabiki. Bi. Mwenda akiwa kapagawa na shangwe za Dar Live. Mrisho Mpoto akiwapa raha mashabiki. Afande Sele akiwapa 'hi' mashabiki. Mgeni rasmi katika tamasha hilo ambaye pia ni Me