MKE ANUNUA TALAKA KWA MILIONI 4
UNAWEZA kusema ni jeuri ya fedha baada ya mwanamke, Rukia Apach kukubali kulipa shilingi milioni 4 ili apewe talaka na mumewe, Mohamed Kismati baada ya kuzuiwa kufanya kazi na mkwewe. Ndoa hiyo ilifungwa miaka miwili iliyopita na kufuatiwa na sherehe ya kifahari katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar mwaka juzi. Kwa mujibu wa chanzo chetu, wawili hao wameachana kwa madai kwamba baba mkwe wa Rukia kukataa mkwewe huyo afanye kazi zaidi ya kuwa mama wa nyumbani. Akizungumza na Ijumaa, Rukia alisema kwamba mumewe alimuahidi kumwendeleza kielimu wakati alipokuwa akisoma kidato cha sita pindi akimuoa. “Awali mume wangu aliniahidi kuniendelea kimasomo, lakini baada ya kuolewa nikakataliwa hata kufanya kazi, amri ambayo ilitolewa na baba mkwe wangu ambaye ni mfanyabiashara,” alisema Rukia. Mwanamke huyo alidai kwamba familia ya mumewe ilishikilia msimamo huo hadi ndoa yao ilipovunjika hivi karibuni. Kama vile haitoshi, Rukia amedai kuwa alilazimika kulipa baadhi ya