Posts

Kigwangalla: “Walipanga Kuniangamiza, Walitaka Nitumbuliwe”

Image
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dkt Hamis Kigwangalla, ameeleza kuwa kwa sasa anaishi kwa hofu na tahadhali kubwa juu ya uhai wake kutokana na kuwepo kwa kundi la watu wanaomuwinda wakitaka kumuangamiza huku wengine wakimfanyia mipango ya kumuharibia ili atumbuliwe uwaziri. Kupitia akaunti yake ya instagram Kigwangala ameweka wazi kuwa hata alivyopata ajali aliwekewa ulinzi mkali wodini ili wabaya wake wasiweze kummalizia kwa namna yoyote. Kupitia instagram yake ameandika hivi; Sikusudii kufanya press conference. Watu wengi wamenishauri niishie hapa. Team yangu imefanya kazi nzuri, imenipa uthibitisho wa majina ya wanaotaka nichafuliwe ili niondolewe uwaziri. Bahati mbaya hakuna cha kunichafua nacho, wanapika hadithi za kitoto na kurudia tu. Walidhani ningekaidi maelekezo ya Mhe. Rais juu ya mgogoro wa ndani ya Wizara yetu ili Rais achukie aniondoe, wakakwama. Sikukaidi. Wakaona wafanye mwendelezo kupitia gazeti, sijataka kujibishana nalo, tutakutana mahakamani ambapo m...

Shiza Kichuya Aanza Kazi Simba SC leo

Image
BAADA ya kuvuna pointi sita muhimu katika michezo miwili ya Ligi Kuu Bara huko Kanda ya Ziwa, kikosi cha Simba leo kinaingia kambini kujiandaa na mchezo wa Kombe la FA, huku kiungo mshambuliaji Shiza Kichuya akiwemo kati yao. Simba inajianda na mechi ya Mwadui FC ya mkoani Shinyanga itakayopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Jumamosi hii. Katika mchezo huo, Simba wataingia uwanjani wakiwa na hasira za kufungwa katika mchezo wa ligi uliopigwa Uwanja wa Kambarage huko Shinyanga ambao ulimalizika kwa Mwadui kushinda bao 1-0. Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja Mkuu wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu alisema kuwa kikosi chao kitaingia kambini leo jioni huko Ndege Beach nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Rweyemamu alisema kuwa maandalizi ya mchezo huo yanakwenda vizuri na wachezaji wote wataingia kambini tayari kwa kuwawinda Mwadui kwa ajili ya kulipa kisasi cha kufungwa katika ligi. Aliongeza kuwa kiungo wao wa zamani Kichuya huenda akawa katika sehemu y...

Mshitakiwa Afariki Mahakamani

Image
SHUGHULI zilisimama kwa muda katika Mahakama Kuu mjini  Mbale  nchini  Uganda  baada ya mtuhumiwa kuanguka na kufariki dunia. Simon Mayuya  mwenye umri wa miaka 54 ambaye ni mkazi wa kijiji  Buyobo  Wilaya ya  Sironko  nchini  Uganda,  alifariki dunia muda mfupi baada ya kuanguka katika chumba cha watuhumiwa kabla ya kupandishwa kizimbani. Mayuya alikuwa amekaa miezi sita rumande katika gereza la  Maluku  ambapo alikua anakabiliwa na tuhuma za jaribio la mauaji. Anatuhumiwa kwa jaribio la kumuua binamu yake ambaye amemuajiri kama dereva wa lori. Mwanasheria wa  Mayuya  aitwaye  David Moli  amesema mteja wake alikuwa anasumbuliwa na maumivu ya uti wa mgongo kutokana na kunusurika kwenye ajali ya gari aliyopata kabla ya kukamatwa na kuwekwa rumande. Moli ameongeza kuwa kabla hali ya mteja wake kuwa mbaya aliiomba mahakama kumpa dhamana ili apelekwe hospitali kupatiwa matibabu kabla y...

Amkata Kichwa Bosi Wake Kisa Kutomlipa Mishahara

Image
FUNDI makenika wa Halmashauri ya Wilaya ya  Sumbawanga  mkoani Rukwa,  Cathbert Mwangalaba  (47) ameuawa kwa kukatwa mwili wake na kiwiliwili chake, kutenganishwa na kichwa na kitu chenye ncha kali. Mlinzi ambaye alikuwa ameajiriwa na marehemu anadaiwa kumuua mwajiri wake huyo kwa kumchinja na kiwiliwili chake kutenganishwa na shingo yake. Anatuhumiwa kutenda ukatili huo, baada ya bosi wake huyo kushindwa kumlipa msh ahara wa miezi sita unaofikia Sh 360,000. Baada ya kumuua, mwili wake ulifukiwa katika shimo lililochimbwa shambani mwake katika Kijiji cha Kaondo Manispaa ya Sumbawanga. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Justine Masonje alithibitisha matukio hayo. Alisema kwamba mauaji ya kikatili ya Mwangalaba, yanadaiwa kufanyika saa 3:00 asubuhi Januari 17, mwaka huu shambani mwake kijijini Kanondo. Mwili wa marehemu ulibainika ukiwa umeviringishwa katika mfuko wa sandarusi, ukiwa umefukiwa katika shimo lililo ndani ya uzio wa shamba hilo. Baada y...

TCU Yavifutia Usajili Vyuo 9 Tanzania

Image
TUME ya Vyuo Vikuu ( TCU ) imefuta hati za usajili wa vyuo vikuu vishiriki vitano, vyuo vikuu vitatu na chuo kikuu kishiriki kimoja. Akizungumza jana Jumanne, Januari 21, 2020, jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa,  amesema vyuo hivyo vimeshindwa kujirekebisha na hata vingepewa muda zaidi visingeweza. Amesema vyuo vishiriki ni Chuo Kikuu Kishiriki cha Askofu Mkuu Yakobo (AJUCO), Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Kardinali Rugambwa (CARUMUCo) na Chuo Kikuu cha Theofilo Kisanji (Teku-Dar es Salaam), Chuo kikuu cha Mtakatifu Yohana cha Tanzania Kituo cha St Marks na Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta cha Kilimo tawi la Arusha (JKUA). “Kufuatia mashauriano na maombi yaliyofanywa na wamiliki wa vyuo na tume katika kikao chake cha 97 kilichofanyika Januari 20, 2020,  imeridhia maombi ya wamiliki hao kusitisha utoaji wa mafunzo, hivyo tume imefuta hati za usajili wa vyuo hivyo vishiriki na kuvifutia vibali,” amesema Profesa Kihampa. TCU pia im...

Matokeo Kidato cha Nne, Kidato cha Pili, Darasa la nne Haya Hapa

Image
Baraza la Mitihani la Taifa (Necta)  leo Alhamisi, Januari 9, 2020 limetangaza matokeo ya mtihani wa upimaji darasa la nne, kidato cha pili na kidato cha nne. Matokeo hayo yametangazwa na  Katibu Mtendaji wa Necta ,  Dk Charles Msonde  amesema ufaulu katika mtihani wa upimaji wa darasa la nne umeongezeka kwa asilimia 26.21. Jumla ya watahiniwa 1,531,120 kati ya wanafunzi 1,665, 863 wamepata alama A,B,C na D ikilinganishwa na wanafunzi 1,213, 132 waliofaulu mwaka 2018. Katika mtihani wa upimaji kidato cha pili, wanafunzi 514,251 sawa na asilimia 90.04 kati ya wanafunzi 571,137 wamefanya vizuri katika mtihani huo na kuwawezesha kuingia kidato cha tatu. Dk Msonde amesema mtihani wa kidato cha nne jumla ya watahiniwa 340,914 sawa na asilimia 80.65 ya watahiniwa 422,722 wameefaulu mitihani yao. Watahiniwa hao ni sawa na ongezeko la asilimia 1.38 ikilinganishwa na watahiniwa 284,126 sawa na asilimia 79.27 waliofaulu mtihani huo mwaka 2018. KUTAZAM...

Mbaroni kwa Kusimamisha Msafara wa Rais na Kuomba Kazi

Image
MWANAMME mmoja aliyejulikana kwa jina la Uvinalies Nyabuto amekamatwa leo kwa kuusimamisha msafara wa magari wa Rais Uhuru Kenyatta katika barabara ya kuelekea Ikulu. Kwa mujibu wa Polisi, msafara huo ulikuwa unaelekea Ikulu ukitokea Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta (KICC) ambapo Rais Kenyatta alitoka kwenye mkutano wa 9 wa Wakuu wa Nchi za Caribbean na Pacific. Nyabuto alisimamisha msafara akiwa ameshika bango lililoandikwa “Mheshimiwa, Tafadhali naomba nafasi ya kujiunga na Majeshi ya Ulinzi. Nisamehe kwa kutoheshimu Ulinzi wako. Samahani Rais. Nyabuto.”. Mara moja alikamatwa na Walinzi walio kwenye msafara wa Rais na baadaye alipelekwa katika Kituo cha Polisi Kilimani ambapo aliendelea kushikiliwa.

Yanga Yataja Hatma ya Sadney, Lamine na Madeni Yake

Image
Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Mshindo Msolla. MWENYEKI wa Klabu ya Yanga, Mshindo Msolla, leo Desemba 10, 2019 amezungumzia tetesi za klabu hiyo kutowalipa mishahara wachezaji kwa muda wa miezi miwili na akaweka wazi hatma ya wachezaji Sadney Urikhob na Lamine Moro ambao inasemekana waliandika barua za kutaka kuondoka katika klabu hiyo kwa kutolipwa mishahara yao kwa miezi mitatu. Akiongea na wanahabari alisema ni kweli klabu yake haijawalipa wachezaji mishahara ya miezi miwili ambayo ni Oktoba na Novemba mwaka huu na kwamba iwapo mambo yakienda vizuri watalipwa leo. Aliongeza kwamba habari zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mshambuliaji Sadney Urikhob na beki  Moro Lamine, viongozi wamekubaliana kuachana na Sadney na watabakia na Lamine ambaye atalipwa mishahara yake. Akifafanua hali ilivyo klabuni hapo, amesema walipoingia madarakani mwezi Mei 2019 walikuta madeni mbalimbali ikiwa ni pamoja na kudaiwa Sh. milioni 800 na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA)....

Rasmi Matola Kocha Msaidizi Wa Simba, Aanza Na Mkwara Huu

Image
SELEMAN Matola, ametangazwa kuwa Kocha Msaidizi wa Simba leo akipokea mikoba ya aliyekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo. Matola amesema kuwa amerejea nyumbani na anaamini kwamba atafanya kazi kwa ukaribu kutokana na uzoefu alionao. “Nimerejea nyumbani na nina imani ya kufanya vema, nahitaji sapoti kwa mashabiki kutokana na kutambua vema falsafa ya Simba. “Nilikuwa ndani ya Simba kwenye timu ya vijana kwa sasa nitaendelea gurudumu kwa kushirikiana na benchi la ufundi,” amesema. Matola alikuwa kocha wa Polisi Tanzania alivunja nao mkataba wake wa mwaka mmoja baada ya kufika makubaliano mazuri na uongozi wa Simba na kwa sasa Polisi Tanzania ipo chini ya Malale Hamsini.

Mfungwa Aliyesamehewa na Rais JPM Agoma Kutoka Gerezani, Ajijeruhi

Image
KATIKA Sherehe za kuadhimishi kumbukumbu ya siku ya Uhuru wa Tanganyika, maadhimisho ambayo hufanyika kila mwaka Disemna 9, jana Rais Dkt Magufuli alitangaza msamaha kwa jumla ya wafungwa 5,533, ikiwa ni sehemu ya sherehe hizo ambapo kila mwaka wafungwa huachiliwa. Licha ya kuwa wengi huamini kwamba mfungwa anapopata taarifa kwamba anaanchiwa huru atakuwa mwenye furaha na kuchangamkia fursa hiyo, lakini kiuhalisi hali huwa haiko hivyo kwa kila mtu. Katika hali ya kushangaza Merad Abraham ambaye ni miongoni mwa wafungwa 70 waliosamehewa na Rais Dkt John Magufuli jana Disemba 9, amekataa kuondoka katika Gereza la Ruanda mkoani Mbeya akidai kuwa hana mahala pa kwenda huku akijijeruhi usoni kwa jiwe kwa nia ya kutaka ahamishiwe katika Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam. Meradi ambaye alifungwa kwa kesi ya kubaka alihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela, Juni 20, 2000 na alitakiwa kumaliza kifungo Juni 20, mwakani. Kwa sasa mfungwa huyo amepelekwa kwenye zahanati ya ...

Jinsi yakumtambua mpenzi wako kama anamapenzi ya dhati kwako

Image
Watu wengi huwa wanajiuliza sana swali hili,nitamjuaje kama mpenzi wangu ananipenda kweli,swali hili huwa ni gumu sana kwa watu wengi,lakini minapenda kulijibu leo kama ifuatavyo; Hapa duniani kuna mapenzi ya aina mbili(selfish love and unselfish love)mapenzi ya uchoyo na mapenzi yasio ya uchoyo,mapenzi ya uchoyo ni yale mapenzi ambayo mpendwa mmoja wapo hupenda kupendwa yeye tu kujaliwa yeyetu, pasipo kurudisha upendo kwa mwenzie vile inavyotakiwa kwa lugha nyingine mtu mwenye mapenzi ya uchoyo huwa sio mbunifu katika kupendezesha penzi na mara nyingi huwa ni mtu mwenye lawama na ambae haridhiki kwa kila jambo zuri atakalofanyiwa,(unselfish love)mapenzi yasiyokuwa ya uchoyo haya ndio mapenzi ya kweli,watu wenye mapenzi ya kweli huwa wanapenda kutoa kuliko kupewa na pia hutoa pasipo kuwa na matarajio ya kupata kitu flani. Bali kutoa kwao ndio furaha ya moyo wao,kama ni mwananke anakuwa anamjali sana mpenzi wake pale anapokuwa na vijisenti kidogo akiona shati ama ...

MREMBO SUDAN AOLEWA KWA NG’OMBE 520, TOYOTA 3 KALI

Image
Nyalong na mumewe Kok Alat siku ya ndoa. HATIMAYE familia ya mrembo wa Sudan ya Kusini aliyekuwa anagombewa na waposaji kibao walioahidi kutoa mahali kubwa zisizo za kawaida, imepokea mahari ya ng’ombe 520 na magari matatu aina ya Toyota V8 baada ya binti yao kuolewa! Mrembo Nyalong Ngong Deng (17) kutoka eneo la Awerial, alikuwa na wachumba sita waliokuwa wanamtaka na kila mtu alikuwa tayari kutoa mahali bab’kubwa ikiwa ni pamoja na Sh. milioni moja za Kenya ambazo ni sawa na Sh. milioni zipatazo 20 za Tanzania! Akiwa amekaa kwa utulivu kando ya mumewe, tajiri mkubwa aitwaye Kok Alat katika ukumbi wa Freedom Hall jijini Juba, Ijumaa iliyopita, Novemba 9, Nyalong, mrembo wa kabila la Dinka,  alikuwa nadhari ya mshangao uliowapata watu waliokuwa katika sherehe hiyo. Nyalong akiwa nyumbani kwao; na baba na nduguze kabla ya ndoa. Nyalong, mumewe.

NYUMBA ALIMOFICHWA ‘MO’ YAFAHAMIKA, NI MBEZI BEACH DAR

Image
Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, akiongea na waandishi wa habari leo. NYUMBA inayodaiwa kuwa ndimo alifichwa mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo’ baada ya kutekwa na watu ambao bado hawajajulikana hadi leo ipo eneo la Mbezi-Beach jijini Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, ameonyesha nyumba hiyo ambayo watekaji hao waliikodisha kwa kupanga kwa kusaidiwa na mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la Twalib Mussa.Kwa mujibu wa maelezo ya Mambosasa, kufuatana na uchunguzi uliofanywa kwa kumhusisha pia Twalibu, watekaji hao walitoka  Afrika Kusini. Mohammed Dewji ‘Mo”. Mambosasa alisema kupatikana kwa nyumba ambayo ilikuwa inamilikiwa na mtu mmoja marehemu aliyemtaja kwa jina la Mwansasu, ni moja ya hatua muhimu katika sakata hilo lililoanza kwa kutekwa kwa mfanyabiashara huyo kijana siku ya Oktoba 11 mwaka huu ambapo leo umetimia mwezi hadi kupatikana kwa nyumba aliyokuwa ...

Tamasha la Tigo Fiesta laacha gumzo jijini Arusha

Image
Msanii Maua Sama anayetamba na kibao chake cha Iokote akitoa burudani ya aina yake kwa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya walioshiriki katika tamasha la Tigo Fiesta mwaka 2018. Wasanii wanaounda kundi la Weusi wakiongozwa na Joh Makini wakiwapagawisha mamia ya mashabiki walioshiriki katika tamasha la Tigo Fiesta mwaka 2018 lililofanyika katika uwanja Sheikh Amri Abeid jijini Arusha mwishoni mwa wiki. Msanii Rich Mavoko akitoa burudani kwa maimia ya mashabiki waliofurika katika Tamasha la Tigo Fiesta mwaka 2018. Msanii Whozu na madensa wake wakitumbuiza katika Tamasha la Tigo Fiesta 2018 lilofanyika katika kiwanja cha  Sheikh Amri Abeid jijini Arusha mwishoni mwa wiki. JIJI la Arusha, jana lilishuhudia show za kufunga mwaka zilizojaa ubunifu na vituko vya aina yake kutoka kwa wasanii mbali mbali waliopanda jukwaani kutumbuiza kwenye Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyilka katika  uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Msanii Whozu alikuwa ni kivutio...

Waziri Kabudi akwepa kujibu swali la Zitto Kabwe

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Palamagamba Kabudi, Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe. Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Palamagamba Kabudi amekwepa kujibu swali la Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kutokana na kile alichokisema kuwa ni mtego ambao unaweza kuliingiza taifa kwenye hasara dhidi ya kesi zake za kimataifa. Katika kipindi cha maswali na majibu kwenye Mkutano wa 13 Zitto Kabwe amehoji juu kwanini serikali ishitakiwe wakati imekuwa kwenye mazungumzo na kampuni tanzu za ACACIA pamoja na kuhoji kwanini serikali imefungua kesi dhidi ya kampuni za madini juu ya kukwepa kodi. Naye Waziri wa Katiba na Sheria, Palamagamba Kabudi akijibu swali amesema maswali ya mbunge huyo asingeweza kuyajibu kwasababu yataathiri ushahidi wa serikali kwenye kesi zake zinazoendelea. "Masuala yote ya uliyoyasema yaliyo kwenye mahakama za kitaifa na kimataifa ni yanaendelea, nataka niwaambie mtego huo uwe wa bahati mbaya, wa kutumwa au bahati ambaya sitauingia kamwe kwa sab...

Diamond kumfungulia Hawa biashara baada ya kuona afya yake inaimarika

Image
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz amefurahishwa na habari zilizoenea za kuwa Hawa anaendelea vizuri baada ya kumgharamia matibabu yake. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandiaka hivi:-