Posts

Vanessa Atokwa Povu Kuambiwa Anajichubua

Image
Ubuyu unaotrendi Bongo unamgusa staa wa Bongo Fleva anayekamata anga za kimataifa, Vanessa Mdee ‘V- Ubuyu unaotrendi Bongo unamgusa staa wa Bongo Fleva anayekamata anga za kimataifa, Vanessa Mdee ‘V-Money’ ambaye wikiendi iliyopita alitawala mitandao ya kijamii kwa picha yake iliyomuonesha akiwa amevaa kibukta na kuachia maungo yake wazi kisha mashabiki wakahoji kuwa rangi ya maungo haifanani na rangi ya uso wake ‘eti baadhi ya sehemu amekunywa maji mengi’.  Staa wa Bongo Fleva anayekamata anga za kimataifa, Vanessa Mdee ‘V-Money’ akiwa na mpenzi wake staa wa Bongo fleva, Jux. Mwana-ubuyu wetu alipoona picha hiyo imefunika mitandaoni, aliamua kuangaza kwenye kila akaunti ambapo alikutana na komenti nyingi zilizoonesha madai kuwa mwanadada huyo, kuna wakati huwa anaediti sura yake na kuonekana mweupe na kuna wakati anakuwa na ngozi ya maji ya kunde. Hata hivyo, wapo waliomvaa jumlajumla wakidai amekuwa akitumia mkorogo na kusahau baadhi ya maungo lakini pia wapo

Rais Magufuli Atembelea Bandari jijini Dar

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi i Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi i Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi  Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 akiwa am

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASIMAMISHA KAZI MAOFISA MISITU WANNE, APIGA ‘STOP’ UVUNAJI MAGOGO RUFIJI

Image
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi Maofisa Misitu wanne na kusimamisha shughuli za uvunaji wa mazao ya misitu wilayani Rufiji kwa muda usiojulikana baada ya kutoridhishwa na usimamizi wake. Maofisa waliosimamishwa kazi ni pamoja na Mkuu wa Idara ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Dk. Paul Ligonja, Ofisa Misitu wilaya Gaudens Tarimo, Ofisa Misitu Yonas Nyambuya na Ofisa wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) wa wilaya Seleman Bulenga. Waziri Mkuu amefanya uamuzi huo leo (Jumatatu, Septemba 26, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Rufiji kwenye ukumbi wa halmashauri kabla ya kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye viwanya jumba la maendeleo wilayani Rufiji. Aidha, Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Wilaya hiyo, Juma Njwayo kukusanya magogo yoye yaliyoko msituni na kuyapiga mnada na kuitaka wizara ya Maliasili na Utalii kwenda wilayani Rufiji kufanya uchunguzi wa leseni za uvunaji walizozitoa kwa wilaya hiyo. Waziri Mkuu

Diamond Na Zari Waendeleza Bata Zanzibar

Image
Diamond. Diamond na mpenzi wake Zari. Kutoka kushoto Moses Iyobo, Aunt Ezekiel, Diamond na Zari. Mwanamuziki Diamond akiwa katika mapozi tofauti  na mchumba wake Zari na baadhi ya marafiki zao. Mwanamuziki Nassib Abdul amedhihirisha ule usemi wa wahenga wa zamani kwamba pesa maua na ukiwa nazo unaweza kufanya jambo lolote lile. Baada ya kumfanyia sherehe ya kuzaliwa mchumba wake Zari, aliyezaa naye mtoto mmoja na ambaye ni mjamzito kwa sasa wawili hao bado wapo visiwani Zanzibar wakiendelea kula bata hata baada ya kumaliza kwa sherehe ya siku ya kuzaliwa ya Zari zilizofanyika visiwani humo . Na Leonard Msigwa/GPL.

Msimamo wa CUF kuhusu uamuzi wa Jaji Mutungi kuamua kuwa Prof. Lipumba bado ni Mwenyekiti

Image
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI The Civic United Front (CUF – Chama Cha Wananchi) kimepokea kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kile kinachoitwa “Msimamo na Ushauri wa Vyama vya Siasa kuhusu Mgogoro wa Uongozi wa Kitaifa wa Chama cha Civic United Front (CUF)” ambao uliwasilishwa Ofisi Kuu ya Chama, Buguruni, jana usiku.   Baada ya kupokea Ushauri huo, The Civic United Front (CUF – Chama Cha Wananchi) kinapenda kueleza yafuatayo:   1. Sheria ya Vyama vya Siasa (Political Parties Act, No. 5 of 1992) haimpi mamlaka wala uwezo wowote Msajili wa Vyama vya Siasa kutoa ushauri, msimamo au mwongozo kwa vyama vya siasa kuhusiana na maamuzi ya vikao vya Chama.   2. Msimamo huo wa kisheria wa nchi hii umetiliwa nguvu na kuthibitishwa na Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia UAMUZI wa tarehe 9/5/2005 wa Jaji T.B. Mihayo katika kesi ya Emmanuel Nyenyemela na Magnus Msambila v/s Registrar of Political Parties & Others (Civil Case No. 6 of

Hoja 11 Zilizomrudisha Lipumba CUF

Image
Profesa Lipumba akiwa na Maalim Seif kabla ya hajajiuzulu kama mwenyekiti wa CUF. DAR ES SAALAM: Hoja 11 zilizotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, zimetosha kumrejesha katika wadhifa wake, Mwenyekiti ‘aliyejiuzulu’ wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba. Mbali ya Lipumba viongozi wengine ambao msimamo wa Msajili unawarejesha madarakani moja kwa moja baada ya kusimamishwa na Baraza Kuu la Uongozi la CUF, katika kikao chake cha Agosti 30, mwaka huu kilichofanyika jijini Dar es Salaam ni Naibu Katibu Mkuu Bara Magdalena Sakaya ambaye pia ni Mbunge wa Kaliua na Naibu Mkurugenzi wa Habari Taifa, Abdul Kambaya. Wengine ni Mbunge wa Mtwara, Maftaha Nachuma, wajumbe wa Baraza Kuu Taifa, Masudi Omari Mhina, Thomas Malima, Ashura Mustafa na Kapasha Kapasha. Pia Musa Haji Kombo, Habibu Mnyaa na Haroub Shamis ambao wataendelea kuhesabika kama wanachama halali wa chama hicho. Katika barua yake kwa viongozi wa CUF, Msajili ali

RAIS MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA JUMAPILI KUADHIMISHA SIKU YA BWANA YA 19 BAADA YA PENTEKOSTE KANISA LA MTAKATIFU ALBANO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakishiriki katika Ibada ya Jumapili kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 baada ya Pentekoste asubuhi ya leo Septemba 26, 2016. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakishiriki katika Ibada ya Jumapili kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 baada ya Pentekoste asubuhi ya leo Septemba 26, 2016. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakishiriki katika Ibada ya Jumapili kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 baada ya Pentekoste asubuhi ya leo Septemba 26, 2016.   Waumini wakipokea baraka katika kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano jijini Dar es salaam wakati wa Ibada ya Jumapili kuadhimisha siku ya Bwana ya 19 baada ya Pentekoste asubuhi ya leo Septemba 26, 2016. Mpiga kinanda Bw. Charles Mang'enya akielekeza wimbo kwa waumini katika kanisa la Anglikana l