Posts

JK Avutiwa Na Wimbo Wa Matatizo Wa Harmonize

Image
Msanii wa muziki, Harmonize (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete. Wimbo ‘Matatizo’ wa msanii wa muziki Harmonize, ni moja kati ya nyimbo ambazo zinapendwa na Rais Mtaafu, Jakaya Mrisho Kikwete. Wiki moja iliyopita Mh.Rais Mstaafu Jakaya Kikwete aliwaalika viongozi wa WCB pamoja na wasanii wake nyumbani kwake na kula nao chakula cha mchana. “Unajua wakati Mh Jakaya Kikwete anatoka madarakani Diamond Platnumz bado alikuwa hajasaini wasanii wengine chini la WCB Wasafi, hivyo tulikwenda kuwatambulisha kina Harmonize, Raymond pamoja na Rich Mavoko pia na kukabidhi kazi zao, lakini uzuri wakati tunakabidhi kazi Mh Jakaya Kikwete alikuwa amevutiwa na wimbo wa Harmonize wa matatizo, akawa anasema alikuwa kwenye gari aliisikiliza kazi hiyo na kusema kuwa kijana ameimba sana,” Sallam alikimbia kipindi cha Enewz cha EATV. Sallam alisema hatua ya kukutana na JK wanaimani itawasaidia kuwapa conne...

MAGAZETI YA LEO JUMATATU TAREHE 19.09.2016

Image

Fiesta Yawapagawisha Wabunge Na Mawaziri Dodoma

Image
  Mwanamuziki Vanessa na Jux wakitumbuiza kwenye tamasha hilo. Baadhi ya waheshimiwa wabunge waliohudhuria tamasha hilo akiwemo Profesa Maji Marefu (wa pili kulia), Venance Mwamoto (wa kwanza kulia) na William Ngeleja (katikati). Mheshimiwa Waziri Nape Nnauye akiwa na Naibu Spika Dkt. Tulia na Waziri January Makamba. Kundi la weusi likitumbuiza jukwaani kwenye tamasha hilo lililohudhuriwa na mashabiki wengi. Mwanamuziki Adam Mchomvu akitumbuiza mbele ya mashabiki lukuki ndani ya Uwanja wa Jamhuri. Mwanamuziki Belle 9 naye alikuwa miongoni mwa wasanii waliotumbuiza kwenye tamasha hilo, usiku wa kuamkia leo. Mwanamuziki Darasa akitumbuiza mbele ya mashabiki. Mwanamuziki Darasa akitumbuiza mbele ya mashabiki. Baraka The Prince akitumbuiza usiku wa kuamkia leo. Sehemu ya umati mkubwa wa mashabiki waliohudhuria tamasha hilo kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma, usiku wa kuamkia leo. Mwanamuziki Jux akionesha madoido ya kucheza na jukwaa na mpenzi wake ambaye pia ni mwanam...

RC Makonda Azindua Chama Cha Waendesha Bodaboda Na Bajaj Mkoa Wa Dar es Saalam

Image
Mkuu wa mkoa Paul Makonda akihutubia. Sehemu ya umati ya waendesha bodaboda waliojitokeza. Mmoja wa madereva aliyeshiriki zoezi hilo akiwa kwenye muonekano mpya. Mkuu wa Mkoa akiongozana na baadhi ya viongozi wa chama hicho. Sehemu ya umati waliohudhuria zoezi hilo. Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akivaa koti kama ishara kwa madereva wote ambao watapaswa kuvaa wawapo safarini. Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akijianda kuvaa Helmet. Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akiwa tayari kuvaa kofia nguvu ‘Helmet.’ Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akiwa katika muonekano mpya wa madereva wa bodaboda. Mkuu wa Mkoa akiongoza maandamano ya waendesha bodaboda yaliyoanzia viwanja vya Biafra na kuishia viwanja wa Leaders, Kinondoni. Kopro Rioba akieleza jambo kwenye uzinduzi huo. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mheshimiwa Paul Makonda, mapema leo amezindua Chama cha Waendesha Bodaboda na Bajaj kwa Mkoa wa Dar es Salaam. Pia ameongoza maandamano ya waendesha bodaboda kuanzia viwanja vya Biafra hadi viwanja vya Leade...

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA, AKABIDHIWA MSAADA WA DOLA LAKI MBILI UTOKA KWA RAIS MUSEVENI WA UGANDA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi mchango wa fedha cha dola za Kimarekani laki mbili (USD 200,000) - takriban Tshs. 437,000,000/- taslimu uliotolewa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kwa ajili ya kusaidia waathirika watetemeko la ardhi mkoani Kagera Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea msaada wa fedha cha dola laki mbili za Kimarekani (USD 200,000) -takriban Tshs. 437,000,000/- taslimu kutoka kwa Balozi wa Uganda hapa nchini Mhe. Doroth Samali Hyuha ( wa pili kutoka kushoto) akiwa pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Elibariki Maleko. Msaada huo umetolewa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa Tetemeko la ardhi mkoani Kagera leo Ikulu jijini Dar es salaam. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma taarifa ya Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Rais wa ...