Posts

Zombe na Wenzake Washinda Kesi, Christopher Bageni Kunyongwa

Image
Aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kinondoni,  SP Christopher Bageni (kushoto) baada ya kuhukumiwa kunyongwa akiagana na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi,  (ACP) Abdallah Zombe (katikati). …Akiongea jambo na aliyekuwa wakili wake baada ya hukumu kutolewa. Polisi wakimpeleka katika chumba maalum mahakamani  baada ya hukumu kutolewa. Bageni akielekea katika chumba maalum. Abdallah Zombe (mwenye nguo nyeupe katikati) akiwa na ndugu zake baada ya kuachiwa huru.  BAADA  ya kimya kirefu, Mahakama ya Rufaa leo imemuachia huru aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi,  (ACP) Abdallah Zombe, na maofisa wenzake wawili. Hata hivyo, mahakama hiyo imemuhukumu kunyongwa hadi kufa aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kinondoni,  SP Christopher Bageni. Zombe na wenzake walikuwa wakituhumiwa kuwaua wafanyabiashara watatu wa Mahenge Morogoro na teksi dereva mmoja

Jacqueline Mengi Afanya Uzinduzi Wa Duka La Samani (Molocaho – Amorette)

Image
Mrembo wa taji la Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akizungumza na wageni walikwa pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa duka lake la samani za ndani “Amorette” lililopo katika jengo la Village Walk gorofa ya kwanza karibu na Sea Cliff Hotel, Masaki jijini Dar es Salaam. Muonekano wa nje utaokutambulisha hili ndio duka la “Amorette”  Bi. Jacqueline Mengi akikata utepe kuzindua duka lake hilo. Ha ha ha ha, sasa mko huru kuingia wageni waalikwa kujionea yaliyomo,…..Bi. Jacqueline Mengi akifurahi jambo mara baada ya kukata utepe. Bi. Jacqueline Mengi akiongozana na baadhi ya wageni waalikwa kuingia ndani ya duka la “Amorette” Balozi Juma Mwapachu na baadhi ya wageni waalikwa wakiangalia moja ya meza ya chakula (dining table) iliyotengenezwa kwa mbao aina ya Mninga baada ya kuzinduliwa duka hilo lililopo katika jengo la Village Walk, Masaki jijini Dar. Wageni waalikwa wakiendelea kukagua samani mbalimbali katika duka

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA WAKUU WA MAJESHI YA POLISI WA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA (SARPCCO)

Image
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akihutubia wakati wa Ufunguzi wa mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO) kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC jijini Arusha.  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Ernest Mangu ambaye amekabidhiwa Uenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) akipeana mikono na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Msumbiji Dos Santos JANE (kushoto) ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Shirikisho hilo mara baada ya kukabidhiana Uenyekiti katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC jijini Arusha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akimpa mkono wa pongezi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Ernest Mangu mara baada ya kukabidhiwa Uenyekiti wa SARPCCO kwenye mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi wa Nchi za Kusini mwa Afrika. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Hamad Masauni akihutubia kwenye mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi wa nchi za kusini mwa

Wakurugenzi Manispaa, Miji Na Halmashuri Waapishwa Dodoma

Image
Baadhi ya wakurugenzi wa halmashauri za wilaya wakila kiapo wakati  kukabidhiwa majukumu yao katika ofisi za Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mjini Dodoma Septemba 13. Katibu Msaidizi wa Sekretarieti ya Maadili ya Umma Ofisi ya Kanda ya kati Dodoma, Cathlex Makwaia (kulia) akiwaapisha wakurugenzi 13 wa manispaa, miji na na halmasahuri mjini Dodoma. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Bernard Makali.  Wakurugenzi wakiendelea kula kiapo. …Wakitia saini viapo vyao. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki, akiwapa mawaidha na ushauri wa kiutendaji wakurugenzi baada ya kuapa. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene, akiwapa mawaidha wakurugenzi. Waziri Kairuki akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbulu, Hudson Kamoga. Waziri wa Nchi, Ofisi ya

Simbachawene Awapa Somo Wakurugenzi Wapya

Image
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), George Boniface Taguluvala Simbachawene amewapa somo wakurugenzi wapya walioteuliwa hivi karibu na kuapishwa jana mjini Dodoma. Waziri huyo amewataka wakurugenzi hao kuacha kufanya na mitandao ya kijamii kwa kuwa imekuwa ikitoa taarifa ambazo siyo sahihi. Kauli hiyo aliitoa jana mjini humo alipokuwa akizungumza na wakurugenzi hao baada ya kuapishwa. Alisema:  “Msifanye kazi na mitandao ya  jamii kwa sababu  mingi ni ya uzushi na imekuwa ikidanganya watu, siyo kila unachokiona unakiweka katika mtandao. Waziri huyo alitoa mfano wa taarifa iliyotolewa katika mitandao ya  jamii hivi karibuni kuwa Ofisi ya Rais Tamisemi  imeanza kuwaruhusu waombaji wa ajira za ualimu kuanza kutumia mfumo wa maombi ya ajira za ualimu(On line Teachers Employment Application System-OTEAS) kuwa siyo za kweli. “Imetuletea shida kubwa, inawaumiz,a unakuta mtu ametoka kijijini ametumia zaidi ya Sh 100,000  k