Simbachawene Awapa Somo Wakurugenzi Wapya

????????????????????????????????????

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), George Boniface Taguluvala Simbachawene amewapa somo wakurugenzi wapya walioteuliwa hivi karibu na kuapishwa jana mjini Dodoma.
Waziri huyo amewataka wakurugenzi hao kuacha kufanya na mitandao ya kijamii kwa kuwa imekuwa ikitoa taarifa ambazo siyo sahihi.
Kauli hiyo aliitoa jana mjini humo alipokuwa akizungumza na wakurugenzi hao baada ya kuapishwa. Alisema:
 “Msifanye kazi na mitandao ya  jamii kwa sababu  mingi ni ya uzushi na imekuwa ikidanganya watu, siyo kila unachokiona unakiweka katika mtandao.
Waziri huyo alitoa mfano wa taarifa iliyotolewa katika mitandao ya  jamii hivi karibuni kuwa Ofisi ya Rais Tamisemi  imeanza kuwaruhusu waombaji wa ajira za ualimu kuanza kutumia mfumo wa maombi ya ajira za ualimu(On line Teachers Employment Application System-OTEAS) kuwa siyo za kweli.
“Imetuletea shida kubwa, inawaumiz,a unakuta mtu ametoka kijijini ametumia zaidi ya Sh 100,000  kuja mjini kutuma maombi hayo halafu anakuta siyo ukweli hii mitandao tuachane nayo.’’
Aliwataka wakurugenzi hao kutokaa ofisini na badala yake waende kusikiliza kero za wananchi kwenye maeneo yao.
Wakurugenzi walioapishwa na Halmashauri zao katika mabano  ni Mwantumu Dau (Bukoba), Frank Bahati (Ukerewe), Hudson Kamoga (Mbulu), Mwailwa Pangani (Nsimbo), Godfrey Sanga (Mkalama) na Yusuph Semuguruka(Ulanga).
Wengine  ni Bakari Mohammed (Nachingwea), Juma Mnweke (Kibondo),  Batamo Ndalahwa (Moshi),  Waziri Mourice (Karatu), Fatma Latu (Bagamoyo),  Godwin Kunambi (Manispaa Dodoma) na Elias Ntiruhungwa (Tarime Mjini).

Waziri Simbachawene akizungumza na wakurugenzi hao.

Comments

Popular posts from this blog