Wanafunzi Wadaiwa Kuwacharaza Viboko Walimu Wao
Wanafunzi wa Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Usevya wilayani Mlele Mkoa wa Katavi, wanadaiwa kuwashambulia kwa kuwacharaza viboko walimu wao wawili miongoni mwao akiwemo Makamu Mkuu wa Shule hiyo, Makonda Ng’oka “Membele’‘ (34) ambaye ameng’olewa meno matano kwa kipigo hicho. Walimu hao wawili wamedai kuwa hawako tayari kuendelea kufundisha katika shule hiyo huku wakisisitiza kuwa ni fedheha kwao kucharazwa viboko na wanafunzi wao wenyewe ambapo Mwalimu Gabriel Kambona aliachwa na ngeu kichwani. Mei mwaka huu, Ng’oka “Membele” alifikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi wake akidaiwa kutenda kosa hilo kati ya Novemba 2015 na Aprili mwaka huu. Ilisemekana kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa Makamu Mkuu huyo wa shule hiyo kulifuatia wanafunzi wa kiume wanaosoma Kidato cha Tano sasa wako Kidato cha Sita katika shule hiyo kumkataa na kutishia kuandamana kupinga vitendo vyake vya kuwalawiti wanafunzi wake. Wanafunzi ha