MAAJABU: HUYU NDIYE BINADAMU MWENYE VIDOLE 12 MIGUUNI NA MIKONONI!

Vijay akionesha vidole vyake 12 vya mikono. 
Mchapaji wa India Vijay Singh anaweza kuchapa zaidi ya maneno 100 kwa dakika kwa kutumia vidole vyake 12. 
Lakini Vijay, ambaye pia ana vidole 12 vya miguuni kutokana na dosari yake hiyo ya kimaumbile, anasema hawezi kupata kazi katika nchi yake aliyozaliwa sababu waajiri wanataka tu wanawake wenye mvuto.
Sasa anapanga kuhamia Uingereza kwa lengo la kutafuta ajira baada ya kuwa amekataliwa maombi yake ya kazi zaidi ya 50.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 48, anayetokea Agra kaskazini mwa India, alisema: "Wanataka wanawake wenye mvuto, si wanaume wenye vidole 12."
Miguuni pia, Vijay ana vidole 12. 
Watu wenye dosari za kimaumbile wanaonekana wenye bahati nchini India na Vijay yuko kwenye hali nadra kutokana na vidole vyake vya ziada kufanya kazi kama kawaida. 
Watu wengi wenye hali hiyo wana vipande vichache vya tishu laini ambazo zinaweza kuondolewa na mara chache huwa na mfupa, lakini bila viungio.
Lakini licha ya kuwa na uwezo binafsi 'kwenye kompyuta' kutokana na zawadi yake, hajaweza bado kupata kazi na sasa anataka kusafiri kwenda Uingereza kwa matumaini kutakuwa na kitu fulanu cha kufanya, imeripotiwa. 
Mchapaji mwenye kasi zaidi duniani ni Michel Shestov. Anaweza kuchapa katika lugha 27, na kuweza kufikia kasi ya herufi 17 kwa sekunde! 
Shestov alisomea kuchapa katika jeshi la Urusi, ambako alikuwa akichapa kwa hadi saa nane kwa siku

Comments

Popular posts from this blog