Posts

WEMA SEPETU AREJEA NA KITU KIPYA BAADA YA KURUDI KUTOKA SOUTH AFRICA,TEAM YAKE WAMWAGIA SIFA

Image
History of Dreadlocks Dreadlocks have been around since the dawn of time. Ancient Egyptians wore them, ancient Asian emperor’s wore them, cavemen wore them, even John the Baptist and Samson wore them.

Papa Francis Awatembelea Waliokua Makahaba Zaidi ya 20 Roma

Image
Roma, Italia Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amewashangaza makahaba wa zamani 20 alipowatembelea katika ziara ya kushitukiza kwenye makazi yao yenye ulinzi mjini Roma. Papa Francis alizungumza na wanawake hao, ambao baadhi yao walisafirishwa kutoka Afrika na maeneo mengine ya Ulaya, kwa muda wa zaidi ya saa moja. Wanawake hao waliokolewa kutoka kwenye madanguro walikokuwa wametekwa na mwanamume aliyekua akiwauza kama makahaba na sasa wamepewa makazi na ulinzi katika jengo la ghorofa linalomilikiwa na kanisa katoliki katika Mji Mkuu wa Italia. Papa Francis mwenye umri wa miaka 79 amekua akirejelea mara kwa mara kwamba biashara ya kuwasafirisha binadamu “ni uhalifu dhidi ya binadamu”. Papa Francis aliketi na wanawake hao, wakiwemo wanaigeria saba, waromania sita na wanne kutoka Albania, na kusikiliza habari zao kuhusu namna walivyo lazimishwa ukahaba, ulisema utawala wa Vatican. Wengine watatu katika kundi hilo wanatoka Italia,

VIONGOZI WA CUF WAKIONGOZWA NA MAALIM SEIF WAMTEMBELEA SPIKA WA BUNGE MHE. JOB NDUGAI NYUMBANI KWAKE LEO JIJINI DAR

Image
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Kulia) akiwaeleza jambo viongozi wa CUF walioongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (Katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Julius Mtatiro waliomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo Agosti 13, 2016. Mhe. Spika, Job Ndugai amerejea nchini hivi karibuni akitokea nchini India alikokwenda kwa ajili ya uchunguzi na matibabu. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Kulia) akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (Katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Julius Mtatiro waliomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo leo Agosti 13, 2016 . Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Kulia) akimweleza jambo Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (kushoto) aliyeambatana na viongozi wenzake wa CUF nyumbani kwa Mhe. Spika Job Ndu

Yanga yashinda bao 1-0 dhidi ya Mo Bejeia

Image
Straika mpyawa Yanga, Obrey Chirwa (katikati) akiwatoka wachezaji wa Mo Bejaia. Kikosi cha Mo Bejaia wakipasha kabla ya mechi. Kikosi cha Yanga wakipasha kabla ya mechi. TIMU ya Yanga imeshinda bao 1-0 dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria katika Kombe la Shirikisho Afrika, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam  na kufikisha point 4.  Bao la Yanga limefungwa kipindi cha kwanza Dakika ya pili na Amissi Tambwe. Kikosi cha Yanga SC; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul/Said Juma ‘Makapu’ dk46, Mwinyi Mngwali, Andrew Vincent ‘Dante’/Kevin Yondan dk17, Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Obrey Chirwa na Deus Kaseke/Juma Mahadhi. MO Bejaia; Chamseddine Rahmani, Ismail Benettayeb, Faouzi Rahal, Sofiane Khadir, Soumaila Sidibe, Zakaria Bencherifa, Mohamed Yacine Athmani, Morgan Betorangal, Sofiane Baouali, Amar Benmelouka na Kamel Yesli.

VERA SIDIKA AELEZA SABABU NA KIASI ALICHOTUMIA KUONGEZA MATITI YAKE

Image
Mrembo maarufu kutoka Kenya,Vera Sidika ameweka wazi kuwa alifanya plastic surgery ili aweze kuwa na matiti makubwa. Vera aliyasema hayo akiwa kwenye mahojiano ya Tv na kipindi cha FNL cha EATV ambapo alieleza kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kuona sehemu zingine za mwili wake ni kubwa kasoro matiti,hivyo akaamua kutafuta mwili wenye uwiano. “Kipindi nakua kutoka utotoni na kuwa kijana,mwili wangu ulianza kuwa mkubwa na ukaanza kuwa mkubwa sehemu nyingine huku kwa juu nikawa kama nimenyimwa kidogo,halafu kwenye industry kama hollywood sio big deal,watu wanafanya surgery kama kawaida ila kwa Afrika ni kitu kipya..Nilifanyiwa surgery ya matiti,inaitwa boob job,nilikuwa nataka niwe na mwili wenye uwiano,nilifanyiwa Marekani mjini hollywood na iligharimu kama dola elfu 30” alifunguka vera sidika ambaye pia alidai kuwa uamuzi huo ulichangiwa na ukweli kwamba alitaka avutie zaidi kwenye show biz na kuongeza kuwa hela alizotumia kufanya plastic surgery zinarudi kutokan

Fidel Castro Agonga Miaka 90

Image
Fidel Castro RAIS wa zamami wa Cuba na Kiongozi mwanamapinduzi, Fidel Castro anasherehekea kutimiza miaka 90 tangu kuzaliwa kwake. Fidel Castro alizaliwa Agosti 13, 1926  huko Birán nchini Cuba na aliyetawala Kisiwa hicho kwa zaidi ya miaka 50, hajaonekana hadharani kwa miezi mingi na bado haijabainika iwapo atajitokeza leo. April 19, 2011, Fidel Castro, kushoto, akinyanyua mkono wa mdogo wake, Rais wa Cuba, Raul Castro, wakati wa Mkutano wa Chama cha Congress, Havana, Cuba. Ingawa Cuba imebadilika sana tangu mdogo wake, Raul Castro achukue madaraka miaka nane iliyopita, na ushawishi wa Fidel umeshuka, bado anaenziwa sana na raia wengi wa Cuba. Raul alizaliwa mnamo June 3, 1931 huko huko Birán nchini Cuba Picha za Fidel Castro, kuanzia kushoto akiwa Havana Aprili 29, 1961 kuzungumza na wanahabari, Washington, D.C., Aprili 6, 2000 na Februari. 13, 2016. Hakuna hafla yoyote rasmi iliyopangiwa kufanywa, lakini Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, taifa mshirika

Kitwanga, JPM Wakutana Uso kwa Uso

Image
Rais John Magufuli jana alikutana ana kwa ana na rafiki yake, Charles Kitwanga ikiwa ni siku 80 baada ya kumvua cheo cha Waziri wa Mambo ya Ndani kwa kosa la kuingia bungeni kujibu maswali akiwa amelewa. Wawili hao walikutana kwenye Jimbo la Misungwi ambako Rais alisimama akitokea Wilaya ya Sengerema ambako alihutubia wananchi. Rais alitengua uteuzi wa Kitwanga Mei 20, wakati sakata la utekelezwaji mbovu wa mkataba wa Sh37 bilioni baina ya Jeshi la Polisi na kampuni ya Lugumi Enterprises likivuma kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano. Lakini jana, hali ilionekana ya kikazi zaidi wakati Rais alipofika kwenye jimbo hilo. Kitwanga, ambaye ni mbunge wa Misungwi mkoani Mwanza, alitumia nafasi hiyo kukutana na Rais kwa mara ya kwanza hadharani, kuwasilisha kero za wananchi wake, hasa ya maji. Katika tukio hilo lililovutia hisia za waliokuwepo, Rais aliuthibitishia umma kuwa yeye na Kitwanga ni marafiki wa muda mrefu, alipokuwa akijibu ombi la mbunge huyo la kutaka Ser

Njemba Avamia Makao Makuu ya Trump, Apanda Ghorofa 21 kwa Saa 3

Image
Polisi wakijitahidi kumtoa njemba huyo aliyepanda juu ya ghorofa. Njemba huyo katika haakati za kukwea jengo hilo la ghoofa 58. Akikazana kukwea. Hali ilivyokuwa Mashuhuda wakitahauki. Polisi wakijitahidi kumdhibiti Akitolewa na polisi NEW YORK: Njemba mmoja nchini Marekani aliyejiita kuwa ni mtafiti binafsi na shabiki wa Donald Trump, jana Agosti 10, 2016 alitumia masaa matatu kupanda jengo la mfanyabiashara huyo maaufu duniani ambaye pia ni mgombea urais wa nchi hiyo kwa tiketi ya Chama cha Republican lililopo jijini New York. Taarifa zimeeleza kuwa njemba huyo mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa Virginia alitumia vifaa maalum kupanda ghorofa hilo lililojengwa kwa vioo ambalo pia ni Makao Makuu ya Kampeni za Bwana Trump na ndiyo Makao yake Makuu Kibiashaa kabla ya polisi kumtoa akiwa amefikia ghorofa ya 21 huku akiwa amechomwa vibaya na vioo vya jengo hilo. Trump anaishi kwenye ghorofa ya ya juu kabisa ya jengo hilo lakini kwa sasa an

RAIS DKT. MAGUFULI AANZA ZIARA YAKE MKOANI MWANZA.

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella mara baada ya kuwasili katika Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza.    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza mara baada ya kuwasili akitokea Chato mkoani Geita. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wanakwaya wa UWT Kisima cha maji Chumvi mara baada ya kuhutubia wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza.     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwalimu Mstaafu wa Shule ya Sekondari Sengerema Wilson Fumbuka Mbanga ambaye walifundisha naye shule hiyo tokea mwaka 1982-1985 mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara Sengerema Mkoani Mwanza.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaagana na wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza mara baada ya kumaliza kuwa