Lowassa na Sumaye Wapewa MAKAVU Ndani ya Mkutano wa CCM .........Mpendazoe Ahamia CCM, Mrema Alalama Kuitwa CCM B
VIGOGO mashuhuri wa Chadema waliowahi kuwa mawaziri wakuu; Edward Lowassa na Frederick Sumaye, jana waligeuka gumzo ndani ya Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kumchagua Rais John Magufuli, kuwa Mwenyekiti wa tano wa chama hicho. Gumzo hilo, lilianzishwa na Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Yusuf Makamba, alimpomtaka Askofu wa Kanisa la Ufufuko na Uzima, Josephat Gwajima, asimpotoshe Magufuli ili yasije yakampata ya Sumaye, ambaye sasa anachezea mchangani Kibaha. Sumaye mchangani “Hata akina Sumaye hawakuunda vyama vyao. Bado wanahangaika; na sasa Sumaye anacheza mchangani Kibaha,” alisema Makamba. Sumaye ambaye aliwahi kuwa mjumbe wa Kamati Kuu na NEC ya CCM, kwa sasa anawania uongozi wa Kanda ya Pwani katika Chadema. Kabla ya kusema kuwa Sumaye anahangaika na siasa za mchangani, Makamba alimtaka Gwajima kuacha uongo na kusingizia viongozi wa CCM. Makamba aliyepewa nafasi ya kumuombea kura Rais John Magufuli kwa wajumbe wa Mkut