Mwanaheri: Umbo langu linanitesa

mwanaheri (7) Stori: Imelda Mtema
MSANII anayekuja vizuri kwenye Tasnia ya Filamu Bongo, Mwanaheri Ahmed ametoa dukuduku lake la moyoni kuwa umbo lake limekuwa likimtesa sana na mara  nyingi amekuwa hawezi hata kukatiza sehemu waliokaa vijana wa kiume.
mwanaheri (11)Mwanaheri ambaye kwa sasa anajizolea mashabiki wengi mitandaoni kutokana na umbo lake, alisema anapata wakati mgumu sana na umbo lake hilo kwa sababu hawezi kusema akatize mitaa ‘korofi’ kama Manzese akiwa anatembea kwa miguu.
mwanaheri (1)“Umbo ni zuri na linanipendeza lakini kuna wakati mwingine linageuka kero kabisa maana huwezi kuwa huru useme unaweza kukatiza mitaani bila hofu, yaani ni lazima uchukue usafiri ili uweze kufika sehemu husika,” alisema Mwanaheri ambaye amefanya vizuri kwenye Filamu ya Mwanaheri.

Comments

Popular posts from this blog