Posts

Matukio Yanayoendelea Mkutano Mkuu wa CCM, Dodoma

Image
Sehemu ya Meza kuu kama ionekanavyo pichani tayari wamekwisha ingia ndani ya ukumbi wa Dodoma Convetion Center (DCC) kukamilisha mchakato wao wa kumchagua Mwenyekiti mpya wa chama hicho cha CCM.Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Mwenyekiti wa CCM ambaye leo anatarajiwa kukabidhi kijiti kwa Mwenyekiti Mpya,Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete,Makamu Mwenyekiti Zanzibar Rais Dkt Shein pamoja na Mwenyekiiti mtarajiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli. Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa ratiba na miongozo mbalimbali kwa Wajumbe wapatao zaidi ya 2000 wa mkutano Mkuu Maalum wa CCM ambao tayari wako ndani ya ukumbi wa Dodoma Convetion Center (DCC) kukamilisha mchakato wao wa kumchagua Mwenyekiti mpya wa chama hicho cha CCM. Mwanana mahiri wa nyimbo za Taarab kutoka kundi la Tot Plus Khadija Kopa akiimba mbele ya Wajumbe wapatao zaidi ya 2000 wa mkutano Mkuu Maalum wa CCM ambao tayari w

Taarifa Kuhusu Kufunguliwa kwa Mfumo wa Udahili wa Pamoja NACTE

Image
  Baraza linapenda kutoa taarifa kuwa Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) umefunguliwa tena kuanzia tarehe 22 Julai 2016 ili kujaza nafasi za udahili zilizo wazi baada ya Baraza kuchagua waombaji udahili waliowasilisha maombi yao kuanzia tarehe 4 Machi 2016 hadi tarehe 3 Juni 2016. Mwisho wa kuwasilisha maombi ni  tarehe 5 Agosti 2016 saa sita usiku. Waombaji wapya na baadhi ya waombaji walioshindwa kukamilisha maombi yao kupitia mtandao ilipofika tarehe 3 Juni 2016, wanaarifiwa kuanza kuwasilisha maombi ya udahili kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) ili kujaza nafasi zilizo wazi. Waombaji wanahimizwa kutumia muda huu wa nyongeza ili kuwasilisha maombi. Baraza linapenda pia kuwaarifu waombaji udahili na umma kwa ujumla kuwa vikao vya Kamati za kuidhinisha majina ya waombaji udahili kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) vilipitisha orodha ya majina  ya wenye sifa za udahili kulingana na nafasi za udahili kwa kila kozi zitolewazo na vyuo husika kat

Vigogo wote Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Watumbuliwa MAJIPU

Image
SERIKALI imemuondoa katika nafasi yake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Gerald Kamwenda na wakurugenzi wenzake, katika jitihada za kufumua na kusuka upya shirika hilo. Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, ametangaza hatua hiyo ya serikali jana alipokutana na vyombo vya habari na kuongeza kuwa, watumishi wengine 41 wamehamishwa vituo vya kazi. Alifafanua kuwa hatua hizo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, lililotaka kufumuliwa na kusukwa upya kwa TFS ili kuongeza ufanisi. Kutokana na hatua hiyo, Waziri Maghembe alisema Profesa Dos Santos Silayo ameteuliwa kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa TFS, wakati Kamwenda anahamishiwa Chuo cha Viwanda vya Misitu kilichopo Moshi. Aidha, Mwanaidi Kijazi aliyekuwa Mkurugenzi wa Usimamizi wa Raslimali za Misitu na Nyuki, yeye amekwenda kuwa Mhifadhi Mkuu Amani Nature Reserve na nafasi yake inachukuliwa na Zawadi Mbwambo. Waziri Maghembe alisema

KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM MJINI DODODMA LEO

Image
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akifungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa, Rais John Pombe Magufuli na Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt, Ali Mohamed Shein . Kulia ni Makamu Mwenye kiti wa CCM, Bara, Philip Mangula na wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.   Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akisisitiza jambo mbele ya Wajumbe wa Mutano wa Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kufungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM mjini Dodomam leo Julai 21, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa, Rais John Pombe Magufuli na Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt, Ali Mohamed Shein . Kulia ni Makamu Mwenye kiti wa CCM, Bara,

Mwanaheri: Umbo langu linanitesa

Image
Stori: Imelda Mtema MSANII anayekuja vizuri kwenye Tasnia ya Filamu Bongo, Mwanaheri Ahmed ametoa dukuduku lake la moyoni kuwa umbo lake limekuwa likimtesa sana na mara  nyingi amekuwa hawezi hata kukatiza sehemu waliokaa vijana wa kiume. Mwanaheri ambaye kwa sasa anajizolea mashabiki wengi mitandaoni kutokana na umbo lake, alisema anapata wakati mgumu sana na umbo lake hilo kwa sababu hawezi kusema akatize mitaa ‘korofi’ kama Manzese akiwa anatembea kwa miguu. “Umbo ni zuri na linanipendeza lakini kuna wakati mwingine linageuka kero kabisa maana huwezi kuwa huru useme unaweza kukatiza mitaani bila hofu, yaani ni lazima uchukue usafiri ili uweze kufika sehemu husika,” alisema Mwanaheri ambaye amefanya vizuri kwenye Filamu ya Mwanaheri.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi ya July 23

Image
Advertisement

Yanga yamuacha Kessy

Image
Mchezaji wa Yanga, Hassan Kessy. Wilbert Molandi, Dar es Salaam MSAFARA wa wachezaji 21 wa Yanga, asubuhi ya kesho Jumamosi utaondoka kuelekea nchini Ghana kwa ajili ya kukipiga na Medeama ya nchini humo huku wakiwaacha mabeki wao, Hassan Kessy na Mtogo, Vincent Bossou. Yanga itarudiana na Medeama katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada kutoka sare ya kufungana bao 1-1 mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Julai 16, mwaka huu. Chini ya Kocha Mholanzi, Hans van Der Pluijm, Yanga inatakiwa kushinda kwenye mchezo huo ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu kucheza Nusu Fainali ya michuano hiyo, kinyume na hapo hali ya mambo inaweza kuwa mbaya na yawezekana wakawa wamefuta ndoto za kusonga mbele. Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, amesema msafara wao unatarajiwa kuwa na watu 30, kati ya hao, wachezaji ni 21 na viongozi tisa. Amesema msafara huo unatarajiwa kuondoka saa moja asubuhi kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JN