Posts

'Ni vizuri mwanaume, amfiche mkewe vipato vyake’

Image
  Ukipata bahati ya kukaa kwenye vijiwe vingi vya wanaume, kauli za ‘mwanamke usimueleze kila kitu’ huwa zinatawala. Wanaambizana kwamba ili uhusiano udumu, usimueleze kila kitu mwanamke. Wanasema mfiche asijue kila kitu. Taswira hiyo imeanza kama utani lakini pengine kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kusonga mbele, sasa inakuwa kama sheria. Wanaume wanasambaziana mbinu hiyo ili kukabiliana na wanawake zao. Wanaona ni bora kuwaficha baadhi mambo ili mambo yaende vizuri. Mwanaume anaamini akimficha baadhi ya vitu mkewe, inasaidia kumfanya aishi kwa amani. Hataki kumueleza kila kitu kinachomhusu kwani anaamini uwezo wake wa kukabiliana na mambo hauwezi kuwa sawa na yeye hivyo bora amfiche. Hali hiyo haikuja hivihivi, imetokana na visa mbalimbali wanavyokutana navyo katika uhusiano. Wanafikia hatua ya kuwafananisha wanawake na watoto. Kwamba hata kama mwanaume hana fedha, hapaswi kumueleza mwanamke kuwa hana fedha. Kwamba mwanamke usimueleze vyanzo vyote

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU KUMWAKILISHA RAIS MAGUFULI RWANDA KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI WANACHAMA WA UMOJA WA AFRIKA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN ataondoka nchini kesho jumamosi kwenda KIGALI nchini Rwanda kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 27 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU). Makamu wa Rais atamwakilisha Rais Dkt JOHN MAGUFULI katika Mkutano huo wa siku MBILI ambao unatarajiwa kufanyika KIGALI – RWANDA kuanzia Julai 17-18 mwaka huu. Katika Msafara wake, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN atafuatana na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Balozi AUGUSTINE MAHIGA na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Zanzibar Issa Haji Ussi. Mkutano huo ambao utahudhuriwa na Makamu wa Rais utaanza kwa vikao vya ndani ambapo viongozi watajikita katika kujadili masuala ya kimkakati ikiwemo umuhimu wa kuliunganisha Bara la Afrika kibiashara kwa kuwa na soko la biashara huria ifikapo mwaka 2017 pamoja na mageuzi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Aidha Waju

TANZANIA YAFANYA UPASUAJI WA KIHISTORIA,YAWEKA BETRI KWENYE MOYO

Image
Na John Stephen, MNH Dar es Salaam, Tanzania.Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)-Muhimbili LEO imefanya upasuaji mkubwa wa moyo kwa mtoto, Happiness John Josephat ambaye amepandikizwa peacemaker (betri ya umeme wa moyo) kwenye mfumo wa moyo wake. Mmoja wa madaktari wa moyo walioshiriki kwenye upasuaji huo, Dk Godwin Sharau wa taasisi hiyo amesema upasuaji huo umechukua saa moja na kwamba mtoto anaendelea vuzuri. Dk Sharau amesema mtoto huyo amepandikizwa peacemaker (betri ya umeme wa moyo) ambayo itasaidia kuunganisha mishipa ya fahamu ya umeme wa moyo ambayo inaunganisha vyumba vya moyo vya juu na chini kwenye moyo wa binadamu. “Upasuaji huu ni wa kwanza kufanyika Tanzania. Upasuaji kama huu unafanyika kwa watu wazima, lakini watu wazima hawahitaji upasuaji wa moyo wa kupandikiza. Watoto wanahitaji upasuaji wa moyo wa kuipandikiza. “Tatizo la mtoto huyu ni la kuzaliwa. Na ni nadra kutokea. Inaweza kupita miaka mingi bila watoto kutokea tatizo kama hilo.

STEVE NYERERE AIZUNGUMZIA ISSUE YA KUKOSA U DC ,AELEZA MENGI

Image
Baada ya madai kuwa msanii wa filamu, Steve Nyerere alikuwa na matumaini ya kuteuliwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli katika uteuzi wa wakuu wa wilaya (ma-DC) wapya, staa huyo wa filamu amefunguka na kuzungumzia issue hiyo. Steve Nyerere Steve Nyerere amesema yeye ni mmoja kati ya watu ambao walikuwa wanasubiria uteuzi wa ma- DC na hajajisikia vibaya kukosa kwa kuwa ana imani bado Magufuli anamwangalia. “Mtu kama upo smart kwanini usisubirie nafasi kama hizo, mimi ni mtu safi na kazi naiweza,” alisema Steve. Aliongeza, “Uteuzi nimeusikia, tuombe mungu kama akinifikiria kwa awamu nyingine sio mbaya, tena ningependa Kinondoni, ni sehemu ambayo naona naweza kuifanyia kazi vizuri kwa sababu hata kwenye nafasi za ubunge nilishika nafasi yatatu, kwa hiyo kama ningepata Kinondoni ingekuwa poa zaidi” Mwigizaji huyo ni mmoka kati ya wasanii ambao walikuwa katika team ya kampeni ya Magufuli katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2016.

Njombe kidedea Kampeni ya Usafi, yatwaa Toyota Land Cruiser

Image
         Waziri wa afya, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akisoma hotuba katika hafla hiyo. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  akiwakabidhi cheti baadhi ya wawakilishi kutoka halmashauri zao. …Akiendelea kukabidhi vyeti vya ushindi. …Akikabidhi kombe kwa mmoja wa wakilishi wa halmashauri hizo. Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya akiwakabidhi kombe wawakilishi wa halmashauri zao. Baadhi ya wawakilishi kutoka mikoa mbalimbali wakipita mbele kupewa mkono wa hongera. Waziri Mwalimu (kushoto) akiwa na baadhi ya wawakilishi wa Halmashauri ya Mkoa wa Njombe. Baadhi ya pikipiki zilizotolewa kwa halmashauri zilizoibuka kidedea kwa usafi. Mwalimu (mwenye kilemba kichwani) akishuhudia gari la ushindi lililotolewa Njombe. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Njombe, Valentino Aidani,  akiwa ndani ya gari walilojishindia. Gari la ushindi wa Halimashauri ya Njombe. HALMASHAURI ya Mkoa wa Njombe leo imeimbuka kidedea na kutwaa gari aina ya  ‘Toyota La

Nafasi 500 za Udereva Kutoka UDA

Image
Uongozi wa UDA Management Agency Limited unatangaza kazi za Madereva 500 wenye leseni daraja “C” na uzoefu wa kuendesha mabasi ya abiria kwa miaka kuanzia 2 na kuendelea. Maombi yawasilishwe kwa Charles Nzilankoma -Operations Manager 0763 600 376 au kwa Cyprian Malekela 0754 266 029 kwa Usaili wa awali.

WAKURUGENZI WA HALMASHAURI ZA MAJIJI, MANISPAA,MIJI NA WILAYA WALA KIAPO CHA AHADI YA UADILIFU KWA VIONGOZI WA UMMA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni na kuwataka kuwatumikia wananchi ikiwemo kuondoa kero zinazowakili wananchi katika maeneo yao kama utitiri wa kodi hasa kwenye bidhaa wanazozalisha.Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Angella Kairuku na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan. wakati wa hafla ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kwa wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni.Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akiongea na wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya (Hawapo pichani) walioteuliwa hivi karibuni na kusisitiza kwenye matumizi ya Kanuni, Sheria na Taratibu katika kutimiza majukumu y

Mfanyabiashara Anayedaiwa Kujipatia Milioni 7 Kwa Dakika Afikishwa Mahakamani Na Kusomewa Mashitaka 199

Image
Hatimaye mfanyabiashara aliyetajwa na Rais John Magufuli kuwa amekuwa akiibia Serikali takriban Sh7 milioni kwa dakika, amepandishwa kizimbani na wenzake wanne na kusomewa mashtaka 199, wote kwa pamoja. Mfanyabiashara huyo, Mohamed Mustafa Yusufali na wenzake Alloyscious Gonzaga Mandago, Isaac Wilfred Kasanga, Taherali Sujjauddin Taherali na Mohamed Seif Kabla, walipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.  Washtakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo kwa mamlaka za Serikali, utakatishaji fedha na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh15 bilioni. Katika ya mashtaka hayo, Yusufali maarufu kwa majina ya Mohamedali, Choma au Jamalii anakabiliwa na mashtaka 198 yeye peke yake huku wenzake wakikabiliwa shtaka moja la utakatishaji fedha. Kutokana na wingi wa mashtaka hayo, waendesha mashtaka wawili; Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shadrack Kimaro na Wakili wa Taasisi y

Cameron Kuachia Ngazi Leo Uingereza

Image
David Cameron . Theresa May leo anakuwa waziri mkuu wa pili mwanamke katika historia ya nchi ya Uingereza baada ya Margaret Thatcher aliyetumikia nafasi hiyo kati ya 1979-1990. Waziri mkuu huyo mtarajiwa  huenda akaongeza nafasi nyingi zaidi za wanawake kwenye baraza la mawaziri. Mwanamama Amber Rudd huenda akateuliwa katika moja ya nafasi nyeti ya waziri wa mambo ya ndani au waziri wa fedha. Justine Greening. Justine Greening na Priti Patel waliokuwa vinara wa kutaka nchi ya Uingereza kujitoa kwenye Jumuiya ya Ulaya wanapewa nafasi kubwa ya kuteuliwa na waziri mkuu mpya anayeamini umefika wakati wa wanawake kupewa majukumu zaidi katika nafasi nyeti ndani ya serikali. Priti Patel. Waziri mkuu mtarajiwa anaweza kuvunja rekodi ya kuwateua wanawake wanane kwenye baraza lake la mawaziri. Leo asubuhi waziri mkuu aliyejiuzulu atawasilisha barua kwa Malkia Queen Elizabeth II itayohitimisha utawala wake na kutoa nafasi ya kuundwa kwa serikali mpya ya May.

Polisi wavamia nyumbani kwa Diamond usiku!

Image
Diamond Platnumz IMELDA MTEMA NA GABRIEL NG’OSHA DAR ES SALAAM: Polisi wenye silaha hivi karibuni wali ka nyumbani kwa msanii nyota, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anayeishi Mivumoni Madale na kusitisha shughuli za burudani zilizokuwa zikiendelea ndani, Risasi Mchanganyiko limedokezwa. Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, shughuli iliyositishwa  na polisi ilikuwa ni ile ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mama mzazi wa mkali huyo wa muziki, Sanura Kassim ‘Sandra’ iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. Ilidaiwa kwamba msanii huyo amekuwa akifanya sherehe mara kwa mara katika nyumba yake hiyo, hali inayosababisha kero kwa baadhi ya majirani zake, ambao nao, wamekuwa wakilalamika mara kwa mara kwa viongozi wa serikali ya mtaa huo. Nyumbani kwa Diamond Platnumz Gazeti hili baada ya kuupata ubuyu huo, lilifunga safari hadi nyumbani kwa msanii huyo na ku kia ofisini kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mivumoni, Deodatus Kamugisha ambaye baada ya kuulizwa ku

Kituo cha Foreplan Clinic cha Tabib Mwaka Chafutiwa Usajili

Image
Serikali imekifungia kituo cha tiba asilia cha Foreplan kinachomilikiwa na Juma Mwaka kwa kukiuka masharti ya kibali alichopewa kujitangaza kuwa anatoa tiba za kisasa badala ya matibabu ya asilia. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mwenyekiti Wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Dk Edmund Kayombo amesema kuwa kituo hiko kimefutiwa usajili na hakiruhusu kutoa huduma za tiba asilia na tiba mbadala kwa jamii kwa kutokidhi masharti ya usajili na kufanya kazi kinyume cha usajili wake. “Kuanzia hivi sasa tumekifutia usajili kituo cha tiba asili na tiba mbadala cha Foreplan kwa kukiuka masharti ya usajili na hivyo hakiruhusiwi kutoa huduma kwa jamii  na watanzania kwa ujumla,”amesisitiza Dk Kayombo. Ameongeza kuwa vituo vingine vilivyofungiwa kutoa huduma ni pamoja na Tabibu Abdallah Mandai wa Mandai Herval Clinic na Kituo cha Fadhaget Sanitarium Clinic kinachomilikiwa na Tabibu Fadhil Kabujanja.

KONDA WA DALADALA ACHINJWA KAMA KUKU,UNYAMA WA KUTISHA

Image
Amonike Isdori ‘Dulla’ enzi za uhai wake. Na Waandishi Wetu,   UWAZI DAR ES SALAAM: Zama za mwisho! Kijana aliyefahamika kwa jina la Amonike Isdori ‘Dulla’ (22) mkazi wa Makondeko- Golani, Kimara jijini Dar ambaye ni kondakta wa daladala, hivi karibuni alichinjwa kama kuku na watu wanaodaiwa kuwa ni walinzi shirikishi (sungusungu). Bibi wa marehemu akilia kwa uchungu. Tukio hilo la kusikitisha lilitokea usiku wa siku ya Idd Mosi, majira ya saa 7 usiku ambapo marehemu inadaiwa alikuwa akirejea nyumbani kutoka kwenye sherehe za sikukuu, ndipo alipokutana na watu hao walioanza kumpiga kwa madai alikuwa mwizi. Akizungumza kwa majonzi na waandishi wetu, mama mdogo wa Amonike, Janeth alisema; “Siku ya tukio niligongewa mlango usiku na kundi la watu kama 15, ambao sikuwafahamu wakadai wao ni sungusungu na wamemkamata mwanangu kuwa ni mwizi. “Walikuwa wamemfunga Amonike kamba miguu na mikono huku utosini akiwa na jeraha kubwa na ametapakaa damu. Niliwaambia mwanangu

Watu 3200 wakusanyika na kupigwa picha za utupu!

Image
          Sehemu ya umati wa watu 3,200 waliohudhuria tukio hilo. Hull, Uingereza WATU zaidi ya 3200 wamekusanyika na kusherehekea utamaduni wao wakiwa kwenye huku wakiwa wamevua nguo zao zote (utupu) katika Mji wa Hull, Uingereza ikiwa ni tukio la kusherehekea mji huo kama Mji wa Utamaduni. Katika tukio hilo lilitokea Jumamosi ambapo washiriki walijipaka miili yao rangi ya bluu-baharina kisha kupigwa picha wakiwa katika maeneo mashuhuri jijini humo kama sehemu ya mradi uliopewa jina Sea of Hull. Mradi huo unatekelezwa na mpiga picha Spencer Tunick na unadhaminiwa na taasisi ya Sanaa ya Ferens Art Gallery. Picha zilizopigwa siku ya tukio hilo, zitawekwa na kuoneshwa kwa umma wakati wa tamasha ya sanaa ya 2017 itakayoendelea kwa mwaka mmoja. Tunick, anayetoka New York, amewahi kupiga picha za watu wengi wakiwa uchi Sydney Opera House, Place des Arts mjini Montreal, Mexico City na mjini Munich nchini Ujerumani Germany. Bw Tunick amesema kazi zake “hu