Njombe kidedea Kampeni ya Usafi, yatwaa Toyota Land Cruiser

1.Wazri wa afya,Jinsia wazee na watoto,Ummy Mwalimu akisoma hotuba yake.         Waziri wa afya, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akisoma hotuba katika hafla hiyo.
2.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwakabidhi cheti baadhi ya viongozi kutoka moja ya Halmashauri zao.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  akiwakabidhi cheti baadhi ya wawakilishi kutoka halmashauri zao.
3.Makonda akiendelea kukabidhi vyeti vya ushindi kutokana na kuibuka washindi kwenye Halimashauri zao.…Akiendelea kukabidhi vyeti vya ushindi.
4.Makonda akimkabidhi kombe la ushindi katika kampeni ya usafi na Mazingira.…Akikabidhi kombe kwa mmoja wa wakilishi wa halmashauri hizo.
5.Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt.Mpoki Ulisubisya akiwakabidhi kombe washindi walioibuka kidedea.Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya akiwakabidhi kombe wawakilishi wa halmashauri zao.
6.Baadhi ya wawakilishi kutoka mikoa mbalimbali wakipita mbele kupata mkono wa hongera.Baadhi ya wawakilishi kutoka mikoa mbalimbali wakipita mbele kupewa mkono wa hongera.
7.Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu (kushoto) akiwa na baadhi ya wawakilishi walioibuka kidedea wa Halimashauri ya Mkoa wa Njombe katika picha.Waziri Mwalimu (kushoto) akiwa na baadhi ya wawakilishi wa Halmashauri ya Mkoa wa Njombe.
8.Baadhi ya pikipiki zilizotolewa katika Halmashauri zilizoibuka kidedea kwa usafi.Baadhi ya pikipiki zilizotolewa kwa halmashauri zilizoibuka kidedea kwa usafi.
9.Waziri Ummy Mwalimu (mwenye kilemba kichwani) akishuhudia gari la Ushindi kwa Halamshauri ya Mkoa wa Njombe baada ya kuibuka kidedea.Mwalimu (mwenye kilemba kichwani) akishuhudia gari la ushindi lililotolewa Njombe.
10.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Njombe, Valentino, Aidani akiwa ndani ya gari hilo walilojishindia baada ya kuibuka washindi wa Usafi wa Mazingira.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Njombe, Valentino Aidani,  akiwa ndani ya gari walilojishindia.
11. Gari la ushindi wa Halimashauri ya Njombe baada ya kuibuka kidedea.Gari la ushindi wa Halimashauri ya Njombe.

HALMASHAURI ya Mkoa wa Njombe leo imeimbuka kidedea na kutwaa gari aina ya  ‘Toyota Land Cruiser’ na pikipiki  baada ya kutangazwa mshindi katika Kampeni ya Kitaifa ya Usafi wa Mazingira ulioanza mwaka jana.
Halmashauri hiyo imeibuka kidedea leo katika hafla fupi iliyofanyika Katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere  jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya ambao walikabidhi zawadi za medali na vyeti vya ushindi.
 Akizungumza katika hafla hiyo, Mwalimu amesema kuwa tangu kampeni hiyo ya kufanya usafi kuzinduliwa na Rais John Pombe Magufuli,  wananchi kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kuwa mabalozi wazuri katika kuhakikisha mazingira wanayoishi yapo safi na kuhimizana kuendelea na usafi wa mazingira kuepukana na ugonjwa wa kipindupindu na kuishi kwenye mazingira ya kuvutia.
Aidha aliziasa halmshauri zote nchini kuhakikisha zinaiga mfano kutoka Halmashauri ya Njombe iliyoibuka kidedea ili ziweze kuwa miongoni mwa washindi wa zawadi nyingine.
Halmashauri ya Njombe iliibuka kidedea katika nyanja mbalimbali za vigezo vilivyokuwa vikizingatiwa ikiwemo mitaa zao za mkoa huo.
Kwa upande wa halmashauri za miji zilizoibuka kidedea ni Halmashauri ya Mbeya na ya Kinondoni huku kwa upande wa manispaa ni Iringa, Moshi na Mpanda.
NA DENIS MTIMA/GPL

Comments

Popular posts from this blog