Posts

Kituo cha Foreplan Clinic cha Tabib Mwaka Chafutiwa Usajili

Image
Serikali imekifungia kituo cha tiba asilia cha Foreplan kinachomilikiwa na Juma Mwaka kwa kukiuka masharti ya kibali alichopewa kujitangaza kuwa anatoa tiba za kisasa badala ya matibabu ya asilia. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mwenyekiti Wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Dk Edmund Kayombo amesema kuwa kituo hiko kimefutiwa usajili na hakiruhusu kutoa huduma za tiba asilia na tiba mbadala kwa jamii kwa kutokidhi masharti ya usajili na kufanya kazi kinyume cha usajili wake. “Kuanzia hivi sasa tumekifutia usajili kituo cha tiba asili na tiba mbadala cha Foreplan kwa kukiuka masharti ya usajili na hivyo hakiruhusiwi kutoa huduma kwa jamii  na watanzania kwa ujumla,”amesisitiza Dk Kayombo. Ameongeza kuwa vituo vingine vilivyofungiwa kutoa huduma ni pamoja na Tabibu Abdallah Mandai wa Mandai Herval Clinic na Kituo cha Fadhaget Sanitarium Clinic kinachomilikiwa na Tabibu Fadhil Kabujanja.

KONDA WA DALADALA ACHINJWA KAMA KUKU,UNYAMA WA KUTISHA

Image
Amonike Isdori ‘Dulla’ enzi za uhai wake. Na Waandishi Wetu,   UWAZI DAR ES SALAAM: Zama za mwisho! Kijana aliyefahamika kwa jina la Amonike Isdori ‘Dulla’ (22) mkazi wa Makondeko- Golani, Kimara jijini Dar ambaye ni kondakta wa daladala, hivi karibuni alichinjwa kama kuku na watu wanaodaiwa kuwa ni walinzi shirikishi (sungusungu). Bibi wa marehemu akilia kwa uchungu. Tukio hilo la kusikitisha lilitokea usiku wa siku ya Idd Mosi, majira ya saa 7 usiku ambapo marehemu inadaiwa alikuwa akirejea nyumbani kutoka kwenye sherehe za sikukuu, ndipo alipokutana na watu hao walioanza kumpiga kwa madai alikuwa mwizi. Akizungumza kwa majonzi na waandishi wetu, mama mdogo wa Amonike, Janeth alisema; “Siku ya tukio niligongewa mlango usiku na kundi la watu kama 15, ambao sikuwafahamu wakadai wao ni sungusungu na wamemkamata mwanangu kuwa ni mwizi. “Walikuwa wamemfunga Amonike kamba miguu na mikono huku utosini akiwa na jeraha kubwa na ametapakaa damu. Niliwaambia mwan...

Watu 3200 wakusanyika na kupigwa picha za utupu!

Image
          Sehemu ya umati wa watu 3,200 waliohudhuria tukio hilo. Hull, Uingereza WATU zaidi ya 3200 wamekusanyika na kusherehekea utamaduni wao wakiwa kwenye huku wakiwa wamevua nguo zao zote (utupu) katika Mji wa Hull, Uingereza ikiwa ni tukio la kusherehekea mji huo kama Mji wa Utamaduni. Katika tukio hilo lilitokea Jumamosi ambapo washiriki walijipaka miili yao rangi ya bluu-baharina kisha kupigwa picha wakiwa katika maeneo mashuhuri jijini humo kama sehemu ya mradi uliopewa jina Sea of Hull. Mradi huo unatekelezwa na mpiga picha Spencer Tunick na unadhaminiwa na taasisi ya Sanaa ya Ferens Art Gallery. Picha zilizopigwa siku ya tukio hilo, zitawekwa na kuoneshwa kwa umma wakati wa tamasha ya sanaa ya 2017 itakayoendelea kwa mwaka mmoja. Tunick, anayetoka New York, amewahi kupiga picha za watu wengi wakiwa uchi Sydney Opera House, Place des Arts mjini Montreal, Mexico City na mjini Munich nchini Ujerumani Ger...

URENO WAITANDIKA UFARANSA NA KUNYAKUA KOMBE A UERO 2016

Image
Usiku wa July 10 2016 wapenda soka duniani kote macho na masikio yao ilikuwa Paris Ufaransa kushuhudia fainali ya 51 ya michuano ya Euro, Paris ulichezwa mchezo wa fainali ya Euro 2016 kati ya timu ya taifa ya Ureno dhidi ya mwenyeji Ufaransaambaye mara ya mwisho kufungwa na Ureno ilikuwa April 26 1975. Huu ni mchezo ambao ulikuwa unachezwa lakini nafasi kubwa ya ushindi ilikuwa inapewaUfaransa kutokana na rekodi yake ya miaka 40 kutofungwa na Ureno, lakini pamoja na uwezo wao waliouonesha katika michuano ya Euro mwaka huu, Ureno matumaini yalipotea zaidi dakika ya 23 baada ya nahodha wao Cristiano Ronaldo kushindwa kuendelea na mchezo kwa kuumia. Mchezo ulikuwa mgumu licha ya Ufaransa kuongoza kwa kumiliki mpira kwa asilimia 54 kwa 46, dakika 90 zilimalizika kwa suluhu, hivyo refa akaongeza dakika 30 zilioenda kuimaliza Ufarasa, Ureno walifanikiwa kuibuka a ushindi wa goli 1-0, goli pekee ambalo lilifungwa na Eder Antonio dakika ya 109, Eder aliingia akitok...

NGUO YA MAMA YAKE DIAMOND PLATINUMSYAZUA GUMZO,TEA WAPIGANA VIJEMBE VIKALI

Image
Fashion Photo of the day is from Diamond Platnumz Mother with Long Black Dress

MTOTO WA OSAMAA AAPA KULIPIZA KISASI KWA MAUWAJI YA BABA YAKE

Image
Image copyrightGETTYImage captionKiongozi wa mtandao wa kigaidi wa al Qaeda Osama bin LadenMwanaye aliyekuwa kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa al Qaeda Osama bin Laden, ameapa kulipiza kisasi kwa mauaji ya babake.Katika ujumbe wa sauti uliochapishwa katika mitandao Hamza bin Laden ameapa kulipiza kisasi kwa Marekani kwa kumuua babake 2011 huko Pakistan.Ujumbe huo wa dakika 21 wenye kichwa "We Are All Osama,", Hamza ambaye inaaminika kuwa alikuwa na babake makomando wa Marekani walipowavamia na kumtwaa ameapa kuendeleza kazi aliyoianza babake. Image copyrightFLAGG MILLERImage captionUjumbe huo ni wa dakika 21 wenye kichwa "We Are All Osama," ''Tutaendelea kuwasaka na kuwapiga popote pale mtakapokuwa mumejificha ati nyuma ya pazia za usalama kwa maovu munayoyaendeleza ,Palestina, Afghanistan, Syria, Iraq, Yemen, Somalia na kote kwenye ardhi ya waislamu mnayokalia '' shirika la habari la Reuters linamnukuu. ''na kwa wale wanaodhan...

WAZIRI MKUU WA INDIA AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA SIKU MBILI

Image
1.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Waziri Mkuu wa India Narendra Modi katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama na mgeni wake Waziri Mkuu wa India Narendra Modi wakati wa nyimbo za Taifa zikipigwa kabla ya ukaguzi wa gwaride la heshima katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akikagua gwaride la Heshima katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa Waziri Mkuu wa India Narendra Modi Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa India Narendra Modi wakati wakiwasili kwenye lango kuu la Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli a...

MWANAMITINDO FLAVIAN MATATA AISHUKIA SERIKALI YA MAGUFULI,ASHANGAZWA NA HAYA...!!

Image
Katika kile kinachoonekana kama kuikosoa Serikali na nutendaji wake wa kazi,Mwanamitindo na mjasiriamali wa kiamtaifa Flavian Matata ameijia juu ya Seriakali baada ya kuwataka wakurugenzi wapya kuwasilisha vyeti vyao vya kielimu ili kutambua uwezo wao kielimu. Kupitia ukurasa wake wa Twiiter,Matata alisema kuwa anashanganzwa na tukio hilo kwani ni jambo linaloweka sintofahamu juu ya utendaji wa Serikali. Unahakiki vyeti siku ya kuwaapisha?? Hili halikutakiwa kufanywa kabla ya uteuzi?? pic.twitter.com/w20uSNEGca — Flaviana Matata (@FlavianaMatata) July 9, 2016

Oscar Pistorious asomewa hukumu kwa kosa la kumuua mpenzi wake

Image
Mwanariadha wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius aliyekuwa nakabiliwa na shtaka la kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp leo amesomewa hukumu ya kesi hiyo nchini Afrika Kusini. Pistorius amehukumiwa kifungo cha miaka 6 gerezani kwa kukutwa nahatia ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kwa kumpiga risasi. Pistorius alitenda kosa hilo Februari 13, 2013 ikiwa ni usiku wa kuamkia siku ya Valentine Day na inaelezwa alimpiga mpenzi wake risasi kwa madai alidhani ni mwizi aliyekuwa amejificha bafuni.

Aishi na risasi miaka nane

Image
Hassani Athumani akiugulia. Na Gregory Nyankaira, UWAZI MARA: Ama kweli kabla hujafa hujaumbwa! Kijana Hassani Athumani (30) mkazi wa Kiabakari, Kata ya Kukirango, Wilaya ya Butiama, mkoani Mara anaishi na risasi mwilini kwa miaka nane sasa huku akiwa anasikia maumuvi makali na mwili wake ukiwa umejaa vidonda kutokana na kulala muda wote. Kijana huyo amepata masaibu hayo baada ya kujeruhiwa kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi Machi 6, 2008. Hassani Athumani akiwa na mama yake mzazi na mwanaye. Akisimulia juu ya tukio hilo Ijumaa ya wiki iliyopita nyumbani kwao akiwa amelala huku akitokwa na machozi kutokana na kudhoofika mwili wake kuanzia sehemu ya mgongo aliyopigwa risasi hadi miguuni, Hassani alikuwa na haya ya kusema: “Hiyo Machi sita mwaka 2008 tulikuwa tunacheza disko na wenzangu katika ukumbi mmoja uliopo Kiabakari, ghafla saa 4.30 usiku, majambazi yakiwa yamevalia makoti meusi na kufunika nyuso zao, yalivamia katika ukumbi huo n...