Posts

Wabongo wafungukia simu feki kuzimwa

Image
Stori:  Gladness Mallya, Risasi Jumamosi DAR ES SALAAM: Baada ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ‘TCRA’ kutangaza kuzima simu feki usiku wa Juni 16, mwaka huu, wananchi mbalimbali wa Jiji la Dar, wamefunguka ya moyoni: BARIKI GASTON (MWENGE) “Kuzimwa simu feki kumeniumiza sana na siyo mimi tu wapo wengi hasa wenye hali ya chini japokuwa zina madhara wangetuachia kwa muda mrefu kidogo ili tujipange kwanza.” HIDAYA SAID (MWANANYAMALA) “Serikali ilivyofanya siyo vizuri kwa sababu hali ya maisha ni ngumu, nafanya mama ntilie hapa sina uwezo wa kununua simu orijino, wangetuangalia sisi watu wa vipato vya chini wasingezima ila wangezuia zile zinazoingia nchini lakini hizi tunazomiliki tubaki nazo.” JOSEPH VENANCE (MWENGE) “Suala la simu feki kuzima limetuchanganya sana maana tulishazoea kununua kwa bei rahisi lakini sasa haya ni majanga kwa sababu mpaka upate hela ya kununua simu orijino ni kazi sana lakini inabidi tukubaliane tu hali halisi maana zina ...

Video ya aibu ya Wema yavuja!

Image
Wema Sepetu (kulia) wakati wa hafla hiyo. Stori: Andrew Carlos, Risasi Jumamosi DAR ES SALAAM: Video ya aibu inayomuonesha msanii maarufu wa filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ akicheza kihasara mbele ya mwanaume imevuja, Risasi Jumamosi linayo kibindoni. ‘Klipu’ hiyo ambayo Wema anaonekana akikata mauno huku suruali aliyokuwa amevaa ikimvuka na kuacha wazi sehemu ya makalio yake, ilivujishwa hivi karibuni na mdau mmoja wa burudani ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini. Wema na Igwe wa Pah One wakiyarudi. “Hii video niliichukua siku ya ile eventi ya Christian Bella ya kutimiza miaka 10 pale Escape One. Wakati akicheza na msanii wa Kundi la Pah One aitwaye Igwe, Wema alionekana kama alikuwa amelewa, alikuwa akikata mauno lakini aibu zaidi ilikuwa pale ambapo ile suruali yake ilipomvuka na sehemu ya makalio yake kubaki wazi. “Sidhani kama alikuwa kavaa kufuli, baadhi ya watu waliokuwa wakimkodolea macho walishindwa kuamini kama ni Wema yule wanayemju...

Shamsa Ford: Vimini vyangu havimuathiri mtoto

Image
Shamsa Ford Boniphace Ngumije, Risasi Jumamosi DIVA mwenye ‘title’ kubwa Bongo, Shamsa Ford amesema kuwa tangu awe mzazi anajitahidi kuishi maisha ya kistaarabu sana kiasi kwamba hahitaji kuwa na skendo ili kuitunza heshima yake kwa mwanaye wa kiume aitwaye Terry pale ambapo atakuwa kijana. Shamsa na mwanaye. Shamsa alisema hayo wakati akipiga stori mbili-tatu na gazeti hili, alipoulizwa kwa nini anapendelea kuvaa mavazi mafupi alisema kuwa hiyo ni ‘hobby’ yake tangu utotoni, kila mmoja kwenye familia yake anafahamu hilo na wala haihusiani kabisa na malezi ya mtoto. “Mimi nililelewa na mama yangu mkubwa ambaye ameolewa na Mzungu, tangu udogoni alikuwa ananivalisha nguo fupi pamoja na watoto wake. Kwenye familia yetu suala hilo si tatizo wala halihusiani na malezi ya mtoto, ninaimani hata Terry akikua ataliona kuwa ni jambo la kawaida kabisa,” alisema Shamsa.

ALIYEKUWA BEKI WA TP MAZEMBE ATUA SIMBA

Image
Kweli Simba wameamua, tayari beki Janvier Besala Bokungu raia wa DRC, ametua Dar es Salaam kimyakimya ili kumalizana na uongozi wa Msimbazi. Bokungu ni beki wa zamani wa TP Mazembe, kama unakumbuka vizuri ndiye walimchezesha katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba ikakata rufaa kwenye Shirikisho la Soka Afrika (Caf), TP Mazembe wakaondolewa mashindanoni na Simba kupata nafasi ya kucheza na Wydad Casablanca ya Morocco.  “Tayari wametua hapa nchini na wataanza mazungumzo na taratibu nyingine, maana Bokungu alikuwa Esperance ya Tunisia. Mimi ninaamini atasajiliwa Simba maana kiwango chake kipo juu tu,” kilieleza chanzo. Caf, ilitangaza uamuzi wa kuiondoa TP Mazembe Mei 14, 2011 na mechi ikachezwa kwenye uwanja huru wa Petrojet jijini Cairo, Misri, Simba ikatandikwa mabao 3-0, hiyo ilikuwa Mesi 28, 2011.  Bokungu yuko jijini Dar es Salaam pamoja  na kiungo mwingine raia wa DR Congo pia wakisubiri ‘kuonwa’ na makocha au watu maalum kabla ya ku...

Mwalimu Afungwa Jela Miaka 90 kwa kuwanajisi wanafunzi

Image
  Mwalimu John Gichia Mugi. Nairobi, Kenya Mwalimu mmoja wa shule ya msingi aliyetambulika kwa jina la John Gichia Mugi mwenye umri wa miaka 23 nchini Kenya amehukumiwa kifungo cha miaka 90 jela kwa kuwanajisi wanafunzi wake wenye umri kati ya miaka 13 hadi 16. Hii ni moja kati ya vifungo vya muda mrefu zaidi kuwahi kutolewa kwa watu wanaowaingilia watoto kijinsia nchini Kenya. Mwalimu John Gichia alishtakiwa kwa kuwabaka wavulana 9 wa shule ya msingi ya Muthiria iliyopo Muran’ga takriban kilomita 120 Magharibi mwa Nairobi nchini humo mnamo Januari na Mei mwaka 2015. Mwalimu huyo atatumikia kifungo cha miaka 10 kwa kila kosa alilotenda yaani kubaka watoto 9, hivyo kufanya jumla ya miaka atakayotumikia jela kufikia 90. Jaji alisema mwalimu walikuwa amesaliti dhamana na imani aliyopewa na wazazi wa wanafunzi hao wachanga ambao alipaswa kuwatunza, inasemekana alikuwa akiwafanyia vitendo hivyo viovu watoto hao baada ya muda wa masomo wa usiku (preps). Wavu...

Mastaa hawa wameachiwa chata, hakijaelewaka!

Image
    Rose Ndauka Mwandishi wetu, Risasi Jumamosi MPANGO au matarajio ya kila mwanadamu ni kuishi katika uchumba, kuolewa kisha kupata watoto! Wapo ambao wamefanikiwa hilo, wapo ambao wamepata kwanza mimba baadaye wakaolewa lakini wapo pia waliopata mimba kabla ya ndoa kisha wakatofautiana na waliowapa, kila mmoja anaishi kivyake. Katika ulimwengu wa mastaa wa kike Bongo, leo nakuletea baadhi ya mastaa ambao wamepata watoto lakini kwa namna moja au nyingine safari yao na waliowapa ujauzito haikufika mbali, ikavunjika. Wapo ambao walipata kabla na wengine baada ya ndoa. Wengi wao huwanadi watoto hao mitandaoni kwa maneno mazuri wakionesha kwamba ndiyo faraja yao baada ya kuachana na wapenzi au waume wao; ROSE NDAUKA Aliingia katika uchumba na Malick Bandawe. Wakafanikiwa kupata mtoto mmoja, uchumba ukayeyuka wakati wawili hao wakiwa katika mchakato wa kuelekea kwenye ndoa. SNURA MUSHI Amefanikiwa kupata watoto wawili; wa kike na wa kiume kwa baba ...

KIKWETE ATEULIWA KUWA BALOZI WA HESHIMA

Image
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho  Kikwete akipokea barua ya uteuzi kutoka kwa Prof. Kamuzora alipofanya ofisi za CCM Lumumba   Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho   Kikwete akizungumza na  Prof. Kamuzora alipofanya ofisi za CCM Lumumba

MERCY KITOMARI, MJASIRIAMALI KIJANA ANAYETAKA KUMUONA ‘ROLE MODEL’ WAKE RAIS MAGUFULI

Image
Mjasiriamali kijana na mmiliki wa Nelwa’s Gelato, Mercy Kitomari wakati akizungumza na Meneja Uendeshaji wa mtandao wa Habari wa  Modewjiblog , Zainul Mzige (hayupo pichani). MJASIRIAMALI kijana na mmiliki wa Nelwa’s Gelato, Mercy Kitomari amesema anatamani kukutana na Rais John Pombe Magufuli kumwelezea haja ya kukutana na wanawake wajasiriamali vijana wamweleze matatizo yao. Amesema Rais baada ya kukutana na makundi mbalimbali ya wafanyabiashara , inafaa akutane na wajasiriamali wanawake vijana ambao wanapita katika magumu mbalimbali . Alisema katika mahojiano hivi karibuni ambayo sehemu yake itachapishwa katika mtandao wa Modewjiblog muda wowote kwamba, rais Magufuli akiwa kama ‘Role Model wake’ katika kujituma, anaweza kuwasikiliza wanawake hao vijana na kusaidia kuwasukuma juu zaidi katika kampeni ya kuiweka Tanzania kuwa nchi ya viwanda. “Nimekuwa nikikutana na wanawake wenzangu ambao wamekata tamaa na wamekuwa wakiniuliza ninawezaje kuende...

Wabunge wengine wasimamishwa kuhudhuria vikao leo June 17 2016

Image
Leo June 17 2016 idadi ya wabunge kusimamishwa imeongezeka baada ya Naibu Sika, Tulia Ackson kutangaza kusimamishwa kwa wabunge wawili ambao ni Mbunge wa viti Maalum CHADEMA Suzan Lyimo na Anatropia Theonest. Mbune Suzan Lyimo amesimamishwa na Bunge kuhudhuria vikao vitano vya Bunge baada ya kubainika kusema uongo kwamba Jeshi la polisi nchini limenunua magari 777 ya washawasha wakati ukweli ni kwamba hiyo ni Idadi ya magari inayopangwa kuingizwa na jeshi hilo kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Licha ya Mbunge kuonesha ushirikiano kwa kamati ya maadili, haki na madaraka ya bunge, kamati imemwona Mbunge ni mzoefu wa shughuli za bunge hivyo anapaswa kusimamishwa vikao hivyo kuanzia June 17 hadi 24 mwaka huu. Aidha Mbunge Anatropia Theonest amesimamishwa kuhudhuria vikao vitatu vya bunge kwa kosa la kulidanganya Bunge kuwa waziri wa ardhi na nyumba William Lukuvi alichukua ardhi ya wananchi akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.

Unawafanyia nini wazazi wako kipindi hiki wakiwa hai?

Image
Amrani Kaima A ssalam aleikum mpenzi msomaji wangu. Uhali gani wewe uliyepata bahati ya kunisoma tena wiki kupitia ukurasa huu? Ni matumaini yangu kwamba kwa rehema zake Mwenyezi Mungu umzima na unaendelea vyema na mishemishe zako za kimaisha. Mimi nitakuwa mchoyo wa shukurani kama sitatumia fursa hii kumshukuru Mungu kwa kila ambalo amekuwa akinitendea katika kila siku ya maisha yangu. Niseme tu kwamba Mungu ni mwema sana kwangu. Mpenzi msomaji wangu, najua Waislam wako katika mfungo wa Mwenzi Mtukufu wa Ramadhani na wale wanaofuatilia safu hii watakumbuka niliwahi kuzungumzia suala la kila mmoja kuiheshimu imani ya mwenzake. Asitokee hata mmoja wa kujiona yeye ni bora zaidi ya mwingine au kwamba yeye ndiye ambaye yuko kwenye mstari ulionyooka. Wote  tuko sawa na sote ni ndugu, tofauti zetu za kiimani, kikabila na kirangi zisitufanye tukafarakana. Baada ya kusema hayo nirudi sasa kwenye mada yangu ambayo nimedhamiria kukuletea kwa wiki hii. Nawazungum...

WATANZANIA WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZA SOKO LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Image
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO, Tarehe 16.06.2016 WAFANYABIASHARA wa Tanzania wametakiwa kutumia fursa za biashara zinazopatikana katika soko la nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuuza bidhaa zao ndani ya Jumuiya hiyo.Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. “Wafanyabiashara wanatakiwa kuchangamkia fursa ya biashara katika soko la pamoja kwa kuwa ni haki yao na ni utekelezaji wa malengo ya Mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kifungu cha tano ambapo ilianzishwa itifaki ya umoja wa forodha ” ,alisema Bi. Mindi Wafanyabiashara hao pamoja na wasafirishaji wanaotaka kufanya biashara katika soko la Jumuiya hiyo watatakiwa kuonesha cheti cha uasilia wa bidhaa wakati wakiingia nchi wananchama wa Jumuiya hasa kwa wafanyabiashara wadogo wenye bidhaa zisizozidi dola za kima...

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ALIPOKUWA AKIJIBU MASWALI BUNGENI LEO MJINI DODOMA

Image
Wabunge wa Upinzani wakitoka Bungeni baada ya dua kusomwa na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson Juni 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali bungeni mjini Dodoma Juni 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri .kuu) Wageni waliofika Bungeni mjini Dodoma kujionea shughuli  mbalimbali za bunge wakifuatilia kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu  Juni 16, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiteta na Mbunge wa Nkansi Kaskazini, Ally Kessy bungeni mjini Dodoma Juni16, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa zamani wa Singida mjini , Mohammed Dewji kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 16, 2016.

Amfumania mume, achoma nyumba!

Image
  Monika akiwa amezimia. Waandishi wetu, Amani Dar es Salaam: Mapenzi uchizi! Hii ndiyo kauli pekee unayoweza kuitumia baada ya mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Monika, mkazi wa Tabata-Senene jijini Dar, kudaiwa kumfumania mumewe na mchepuko ndani kwake kisha kuchoma moto nyumba kabla ya kuzimia. Nyumba ilivyochomwa moto. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo lililojaza umati, sekeseke hilo lilijiri wiki iliyopita, mishale ya saa 5:00 asubuhi nyumbani kwa wanandoa hao maeneo hayo ambapo mwanamke huyo hakuwepo nyumbani hivyo aliporudi ndipo akaanzisha timbwili, akidai kumkuta mumewe ndani na mchepuko. “Unaambiwa baada ya Monika kurudi nyumbani na kumfuma mumewe ‘akimalizana’ na mchepuko, palikuwa hapatoshi. “Monika aliangusha timbwili la aina yake lakini yule mchepuko alifanikiwa kutoka nduki. “Kutokana na hasira, Monika alijifungia ndani, akamwagia nyumba mafuta ya taa, akawasha moto akitaka kujitoa uhai. “Tunashukuru Mungu, askari wa zima moto walifika na k...

Huzuni…Familia ya Hoyce yanusa kifo ajalini

Image
Mama mzazi wa Hoyce Temu IMELDA MTEMA, Amani Dar es Salaam: Familia ya Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akiwemo mama yake mzazi, dada zake watatu na mdogo wake, wamenusurika kupoteza maisha baada ya gari walilokuwa wakisafiria, kupata ajali mbaya kwenye makutano ya Barabara za Ali Hassan Mwinyi na ile ielekeayo kwenye Ufukwe wa Coco, Amani linakujuza. Ajali ilivyotokea Akizungumza kwa masikitiko, Hoyce alisema ajali hiyo ilitokea mchana wa Jumapili iliyopita wakati wanafamilia hao wakielekea Ufukwe wa Coco kwa ajili ya kupata chakula cha mchana ambapo ghafla, gari jingine aina ya Range Rover Vogue, lililigonga gari walilokuwemo ndugu zake na kuwasababishia madhara makubwa. Hoyce aliongeza kuwa alipata taarifa za kupata ajali ndugu zake hao wakati akiwa Bagamoyo, Pwani kwenye kambi ya watoto wenye ulemavu wa ngozi. Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu Mrembo huyo alisema kuwa alipigiwa simu na dada yake mkubwa aitwaye Edith aliyekuwa kwenye ajali hiyo na kumtaarifu kwamba wamep...

Manji apiga hodi kwa JPM

Image
Dar es Salaam. Kama ulidhani lile sakata la ufukwe wa Coco Beach uliopo kandokando mwa Bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam linalomhusisha Mwenyekiti wa Kampuni za Quality Group Limited (QGL), Yusuf Manji limemalizika, elewa kwamba bado. Manji amezungumza mambo mengi na gazeti la Mwananchi, lakini akasema bado anasubiria majibu yake kutoka kwa Rais John Magufuli baada ya kumwandikia barua Desemba, mwaka jana. Mfanyabiashara huyo ambaye anatarajiwa kustaafu uongozi katika kampuni hiyo mwezi ujao, amesema anatamani kuona suala hilo linamalizika haraka.

Kutoka Arusha: Mbaroni kwa kutupa mapacha

Image
Mtuhumiwa Happiness Joel JOSEPH NGILISHO, Amani ARUSHA: AMENASWA! Msako uliofanywa na wananchi wa Kitongoji cha Namayana, Kata ya Kiranyi wilayani Arumeru mkoani hapa, kufuatia tukio la mwanamke kudaiwa kutupa vichanga mapacha, umefanikiwa kumnasa mtuhumiwa Happiness Joel (29), tembea na Amani. Mwenyekiti wa kitongoji hicho, Elias Naigisa akizungumza na gazeti hili mwanzoni mwa wiki hii, alisema June 7, mwaka huu alipata taarifa ya kutupwa kwa vichanga viwili katika chemba ya choo kinachomilikiwa na mkazi wa kitongoji hicho, Elibariki Loti. Alisema baada ya taarifa hiyo, yeye na wananchi walikwenda kushuhudia na kukuta vichanga hao  wamefariki dunia na kutoa taarifa kwa jeshi la polisi huku yeye na wananchi wake wakianzisha msako mkali kumbaini mwanamke aliyekuwa na ujauzito. “Polisi walifika na kuchukua miili ya vichanga hao na kwenda kuihifadhi katika chumba cha maiti katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kusubiri uchunguzi,” alisema mwenyekiti huyo. Akipa...

MANENO MUME ALIYOMWAMBIA MKE WAKE USIKU BAADA YA SHEREHE YA HARUSI YAO.

Image
   "Mke wangu, watu wote wameenda nyumbani kwao , mziki umezimwa, shamrashamra zimeisha. Harusi yetu ilikua nzuri mno ila sasa imepita. Tumemaliza harusi sasa ni muda wa kujenga familia yetu. Tuliobaki baada ya harusi hii ni mimi na wewe tu peke yetu. Hatma ya kesho huanza leo. Maisha yetu sasa sio kama ya nyuma ... . Nakumbuka kuna kipindi ulivaa gauni jekundu, lilikupendeza sana, siku ile nlitaman kukugusa, tulikua kwenye maonyesho ya sinema nilikua na shauku kubwa sana kwako. Nilitamani japo kukusogeza upande wa chooni ili nikakubusu tu ila haikuwezekana. Niliumia sana moyoni. Ila sasa wajua nini siri ya furaha yangu? Jibu la siri ya furaha yangu ni kuwa sasa nimekupata, niko na wewe pamoja milele, naweza sasa kukubusu kila siku. Kabla sijakuvua nguo na kufanya mapenzi na wewe kwanza ngoja nikuambie vitu vichache vya muhimu mno......... Sina cha kukuficha, kuanzia leo simu yangu waeza kuitumia kama yako pia waeza tumia account na profile zangu Facebook, whatsapp na...

NJIA RAHISI KUSOMA QUR-AN YOTE KATIKA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

Image
  Qur’an ina juzuu thelathini sawa na siku thelathini za mwezi, hivyo kwa kusoma juzuu moja kila siku inatosha kutimiza Qur’an yote kwa mwezi, ikumbukwe pia Qur’an (mas’haf) ina kurasa kati ya 604–612. Inahitaji kusoma kurasa ishirini kwa siku kwa muda wa siku thelathini kumaliza msahafu mzima. Siku moja ina swala tano, zikigawiwa kurasa ishirini kwa swala tano zinapatikanaka kurasa nne katika kila swala. zikigawiwa kurasa nne kwa mbili, yaani itakuwa kurasa mbili kabla ya swala na mbili baada ya swala, ni kiasi chepesi kwa mtu kuisoma Qur’an nzima ndani ya mwezi. Kwa wale ambao hawana muda wa kusoma kurasa nne kila swala, hebu tujaribu hii. Tusome kurasa saba baada ya swala ya sub’hi (alfajir), saba baada ya swala ya laasiri na saba baada ya taraweeh (swala ya Isha). Hivyo itakuwa saba mara tatu ambayo ni sawa na 21. 21 mara siku thelathini ni 630 yaani msahafu na zaidi. Ikumbukwe tabia hujenga mazoea, hebu chagua hesabu moja na uanze nayo mazoezi katika maisha, Mwisho ...

Usome Hapa Waraka wa Edward Lowassa kwa IGP Mangu

Image
Mhe. Edward Ngoyai Lowassa. Kwako Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Salaam, Kwanza niwie radhi kwamba nimelazimika kwa nafasi yako na yangu, kukiuka taratibu za kiitifaki hata nikalazimika kuandika waraka huu kwako. Ninafanya hivyo si kwa sababu yoyote, bali kwa sababu tu jambo au mambo yaliyonisukuma kukukifikishia ujumbe huu, yana uzito mkubwana kimsingi yanaweza kuathiri mustakabali mwema wa kitaifa. Msingi wa waraka wangu huu ni agizo ulilotoa wewe, Inspekta Jeneraliwa Polisi la kupiga marufuku mikutano ya hadhara ya kisiasa namaandamano ya vyama vya upinzani. Ni bahati mbaya kwamba wakati ukitoa maagizo hayo, nilikuwa niko njeya nchi, ingawa kwa bahati njema, Watanzania wenye mapenzi mema nataifa lao waliopo hapa nchini na nje, walinifikishia taarifa juu ya agizolako hilo. IGP, siyo desturi yangu kuandika waraka wa namna hii mtandaoni au kupitia vyombo vya habari, ingawa safari hii nimelazimika kufanyahivyo ili kuweka rekodi sahihi, sambamba na kukosoa sababu ulizotoakuwa...

Mbunge wa Ukonga Ashinda Kesi ya Uchaguzi

Image
    Mbunge wa Jimbo la Ukonga (Chadema), Mwita Waitara (kulia) akitoka mahakamani. (Picha na Maktaba). Mbunge wa Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mwita Waitara leo ameshinda kesi ya uchaguzi iliyokuwa imefunguliwa na mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jerry Silaa. Hukumu hiyo imetolewa leo muda mfupi uliopita na Jaji Fatma Msengi wa Mahakama Kuu ya Dar es Salaam.