NJIA RAHISI KUSOMA QUR-AN YOTE KATIKA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

Qur’an ina juzuu thelathini sawa na siku thelathini za mwezi, hivyo kwa kusoma juzuu moja kila siku inatosha kutimiza Qur’an yote kwa mwezi, ikumbukwe pia Qur’an (mas’haf) ina kurasa kati ya 604–612. Inahitaji kusoma kurasa ishirini kwa siku kwa muda wa siku thelathini kumaliza msahafu mzima. Siku moja ina swala tano, zikigawiwa kurasa ishirini kwa swala tano zinapatikanaka kurasa nne katika kila swala. zikigawiwa kurasa nne kwa mbili, yaani itakuwa kurasa mbili kabla ya swala na mbili baada ya swala, ni kiasi chepesi kwa mtu kuisoma Qur’an nzima ndani ya mwezi.

Kwa wale ambao hawana muda wa kusoma kurasa nne kila swala, hebu tujaribu hii. Tusome kurasa saba baada ya swala ya sub’hi (alfajir), saba baada ya swala ya laasiri na saba baada ya taraweeh (swala ya Isha). Hivyo itakuwa saba mara tatu ambayo ni sawa na 21. 21 mara siku thelathini ni 630 yaani msahafu na zaidi.

Ikumbukwe tabia hujenga mazoea, hebu chagua hesabu moja na uanze nayo mazoezi katika maisha, Mwisho wa siku utazoea na litakuwa jambo jepesi kwako na la kawaida. Ikumbukwe mtume (S.A.W) Anasema kila herufi moja ya Qur’an ina thawabu kumi, Qur’an nzima ina herufi 323,670 ,hivyo basi kila mwezi utakuwa umejiwekea akiba ya thawabu 3,236,700, yaani323,670 x 10=3,236,700.

Comments

Popular posts from this blog