Posts

HUYU NDO MTOTO WA MAREHEMU KEBWE ALIYEGOMA KUMPA MKONO RC MAKONDA

Image

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA JK IKULU JIJINI DAR LEO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete wakifurahia jambo mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU

Shilingi Bilioni 3 na Mali za Bilioni 10 zataifishwa na TRA Kutoka kwa Wakwepa Kodi Bandari Kavu ya Azam

Image
Mamlaka ya kukusanya kodi TRA kupitia madalali wa Yono Auction Mart wamekusanya mali za bilioni 3 pamoja na kutaifisha mali za bilioni 10 kutoka kwa wafanyabiashara waliopitisha makontena 329 kupitia bandari kavu ya Azam bila kulipa kodi na bado wanaendelea na msako bara na visiwani. Madalali hao wamesema watu walipe kodi na watoe risiti za elekroniki la sivyo mali zitakamatwa.

WAZIRI MKUU MH. KASSIM MAJALIWA AKAGUA MRADI WA MABASI YA MWENDOKASI DART LEO

Image
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza na mwanafunzi Amina Abdallah wa darasa la sita katika shule ya msingi ya Ukombozi jijini Dar es salaam ambaye amepanda basi la Mwendo Kasi Ajentina na kushuka Manzese, Waziri Mkuu Majaliwa ametumia usafiri wa DART leo kutoka Feri kwenda Kimara Mwisho wakati alipokagua miundombinu ya usafiri huo ili kujionea mafanikio na changamoto mbalimbali zinazojitokeza mara baada ya mradi huo kuanza mwezi mmoja sasa ili ziweze kurekebishwa na kuuboresha zaidi.  Usafiri DART umekuwa mkombozi kwa wasafiri wengi wa jiji la Dar es salaam wakati wanapotoka majumbani mwao na kuelekea kazini na kurejea majumbani mwao,Katikati ni Bw. David Mwaibula aliyekuwa Mwenyekiti Mamlaka ya Usafiri wa Daladala Dar es salaam (DRTLA) zamani aliyeambatana na Waziri Mkuu kukagua mradi huo leo.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akifurahia

STORI YA KIFO CHA ANETH MDOGO WA BILIONEA ALIYECHINJWA

Image
May 26 kulitokea mauaji ya kutisha ya kukatwa mapanga kwa mwanadada Aneth ambaye ni ndugu wa Tajiri mmoja ambaye naye aliuliwa kwa kupigwa risasi. Aneth amepigwa mapaga na watu wasiojulika na kukimbia. Jirani wa Anetha pia mfanyakazi mwenzake anafafanua vizuri "Yaani Aneth hata siamini, jana tulikua nae kazini, kaondoka kufika nyumbani akakuta housgal katoroka, akapiga simu kwa mwenzetu akamueleza kwamba leo hatokuja ili angalie logistics. Mtoto wake ana miaka minne ndio alpo hojiwa alisema hivi jana walikuja watu watano weusi, wakavunja mlango ni majira ya mama saa tatu usiku, akakimbia chumbani, walipoingia wakamkuta mtoto wakauliza mama huko wapi akasema chumbani, wakamfuata huko mtoto hajui kilichoendelea. hadi asubuhi school bus ilipokuja alijaribu kutoka akashindwa na mwishowe iliondoka. Anafafanua: Baada ya kuona mama yake haamki ndipo alipotoka kwa jirani na kuwaita. Majirani walikwenda na kukuta Aneth akiwa amechinjwa na akiwa uchi (seem

BUNGE LAENDELEA NA KIKAO CHAKE MJINI DODOMA LEO

Image
Baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza cha maswali na majibu na uchangiaji wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi leo mjini Dodoma. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Anthony Peter Mavunde ambaye akiwasalimia kwa furaha wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Dodoma leo kwenye viwanja vya Bunge. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Anthony Peter Mavunde akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi -VETA mkoa wa Dodoma nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma. Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) George Masaju (katikati) akizungumza na viongozi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) waliolitembelea Bunge mjini Dodoma. akiwasisitiza jambo viongozi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) alipokutana nao nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma

Tanzia: Hussein Macheni afariki dunia

Image
\ Hussein Macheni enzi za uhai wake. Aliyekuwa mmiliki wa baa maarufu ya Macheni iliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam, Hussein Macheni amefariki dunia leo baada ya kuanguka ghafla akiwa nyumbani kwake Magomeni. Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu ni kwamba Macheni alianguka ghafla majira ya saa 9 asubuhi na kukimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo iligundulika kuwa tayari amefariki. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Muhimbili kusubiri taratibu nyingine. Mwenyeji Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi. AMEN.

ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUJIRUSHA KUTOKA KWENYE MNARA WA SIMU JIJINI MWANZA.

Image
Kijana Mmoja (picha) Jijini Mwanza amenusurika kifo baada ya kujirusha kutoka katikati ya mnara wa simu. Na BMG Tukio hilo limetokea hii leo na kuvuta watu wengi waliofika kumshuhudia kijana huo ambae amepanda katika mnara huo tangu majira ya asubuhi na kukatalia mnarani hadi majira ya saa sita mchana. Mashuhuda wa tukio hilo ambao pia ni marafiki wa karibu na kijana huyo, wamesema huenda kijana huyo amefikia maamuzi hayo kutokana na ugumu wa maisha ambao amekuwa akiulalamikia huku wengine wakisema ni kutokana na kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo gundi ambayo amekuwa akiyatumia. Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa jeshi la uokoaji na zima moto mkoani Mwanza, mmoja wa maafisa wa uokoaji Mussa Kaboni, amsetoa rai kwa makampuni yenye minara ya simu kuimarisha ulinzi katika minara hiyo ili kuondoa hatari inayoweza kujitokeza kutoka kwa raia wasio wema. Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walionekana kuchukizwa na kitendo cha kijana huyo na kusiki

Aunt: sasa natafuta mapacha

Image
  Aunt Ezekiel akiwa na Mose Iyoyo sambamba na mtoto wao, Cookie STAA wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel amefunguka kuwa baada ya mtoto wake, Cookie kutimiza mwaka, sasa anafanya mpango kutafuta njia ya kupata watoto mapacha ili atulie. Akizungumza na Amani Aunt ambaye amezaa na dansa wa staa wa Bongo Fleva, Diamond, Moze Iyobo alisema kuwa,  anamshukuru Mungu kumpa mtoto ambaye amemfungulia njia lakini kwa sasa anatamani mapacha ili awe na jumla ya watoto watatu kisha ndiyo apumzike aendelee na mambo mengine. “Baada ya Cookie kunifungulia jina la kuwa mama sasa nataka niongeze uzao mmoja wa pacha ili niwe na watatu kisha nitapumzika,” alisema Aunt.

RAIS MAGUFULI AONGOZWA KUPIGWA JUJU,VIGOGO WAHAHA KILA KUKICHA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ Mwandishi wetu, Amani DAR ES SALAAM: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’, huenda ndiye mtu anayeongoza kwa kupigwa juju kwa waganga wa kienyeji kuliko mtu yeyote nchini kwa sasa,   Amani   linakuja na ushuhuda. Sangoma mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Shark Abdullah ‘Kishapu’, akipiga simu kutoka jijini Tanga mwanzoni mwa wiki hii, aliliambia gazeti hili kuwa katika miezi ya hivi karibuni, amekuwa akipata wateja, wakiwemo wafanyabiashara na watumishi wa umma wakimtaka kumpunguza kasi ya utendaji kiongozi huyo, wakisema inawaathiri. “Sikiliza ndugu mwandishi, mimi hapa ni mganga wa kienyeji, nataka nikupe habari. Kuna watu wengi sana wanakuja hapa kwangu kutaka niwakinge na tumbuatumbua ya Magufuli, wengine wanataka nifanye ninavyoweza kumfanya asiweze kutekeleza majukumu yake. “Nimewapokea wafanyabiashara na hata viongozi wakubwa, wanataka utumbuaji wa m

Waziri Mkuu Akutana na Watanzania Waishio Zambia

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watanzania waishio Zambia kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Lusaka Mei 24, 2016. Majaliwa alikwenda Zambia kumwakilisha  Rais John Magufuli kwenye Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika- ADB uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi. Baadhi ya Watanzania  waishio Zambia wakimsikiliza Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa wakatia lipozungumza nao kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Lusaka.  Majaliwa  alikwenda Zambia kumwakilisha Rais John Magufuli kwenye  mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB, Mei 24, 2016. Baadhi ya Watanzania  waishio Zambia wakimsikiliza Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa wakatia lipozungumza nao kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Lusaka.  Majaliwa  alikwenda Zambia kumwakilisha Rais John Magufuli kwenye  mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB, Mei 24, 2016. Baadhi ya Watanzania  waishio Zambia wakimsikiliza Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa wakatia lipozungumza nao kwenye ubal

Boti yapotea Ziwa Nyasa...Watu Kadhaa Wahofiwa Kufa.

Image
WATU kadhaa wanahofiwa kufa maji baada ya boti iliyokuwa ikifanya safari kutoka Mbamba Bay nchini Tanzania kwenda Nkhata Bay Malawi kuzama Ziwa Nyas na boti kutoweka. Duru  za usalama zinasema Boti hiyo haijulikani ilipo wala abiria waliokuwemo ndani yake jambo ambalo limezua sintofahamu kubwa, huku wakihofia kuzama. Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma, kusini mwa Tanzania, Zuberi Mwombeji alisema haifahamiki ajali hiyo ilitokea aneo gani la Ziwa lakini juhudi za kuitafuta zinaendelea. “…Usafiri wa kutoka Mbamba Bay mpaka Nkhata Bay huchukua saa tano mpaka sita, walipoona Nkhata Bay hawajafika waliwasiliana na watu wa Mbamba Bay ndipo ilipojulikana kuwa kuna tatizo limetokea,” alisema Kamanda Mwombeji. Chanzo cha ajali hiyo kinaaminika ni hali mbaya ya hewa ziwani, hali inayoaminika kuwa ilisababisha Boti hiyo kupigwa dhoruba. Hata hivyo taarifa zinasema boti hiyo ikiwa njiani ilianza kuingiza maji ndipo juhudi za kuyatoa ndani ya boti zilianza kabla ya kuzidiwa.

Baada ya Jackline Wolper kuwa na Harmonize, kataja jina analomuita Diamond kwa sasa.

Image
Kwa sasa headlines nyingi katika upande wa mastaa Tanzania ni stori kuhusu penzi la muigizaji Jackline Wolper na msanii wa Bongo fleva kutoka Wasafi Classic Baby (WCB) Harmonize ndio Topic kubwa town. Katika mahojiano na Take One ya Clouds TV  na Zamaradi Mketema , Jackline Wolper ameeleza mambo kadhaa kuhusiana na penzi lake la Harmonize , Diamond ambaye aliwahi kuwa mpenzi wake anachukuliaje mahusiano yao? “Diamond rafiki yangu sana ni mtu ambae nategemea hata kuja kufanya nae filamu, Diamondi ni rafiki yangu sana licha ya watu wanaweza wasielewe, lakini sasa hivi Diamond ni baba mkwe wangu, “kuhusu Harmonize nampenda kwa sababu ana hofu ya mungu, ana heshima sana mwisho hawezi kufanya maamuzi bila kuomba ushauri, katika kunipenda mimi alipiatia pia kuomba ushauri kwa Diamond ambaye ni boss wake kaka yake na kupewa ruhusa kwa hiyo Baraka zimetoka kwa Diamond mwenyewe”

DIVA ASEMA ANATAKA KUZAA MTOTO MMOJA TU AFUNGE KIZAZI

Image
Star wa Clouds FM, Diva, amefunguka na amesema kwenye maisha yake anataka azae Mtoto Mmoja tu wa Kiume na kufunga Kizazi baada ya hapo. Akiongea na Makorokocho, Diva amesema amekuwa akisumbuliwa na Maumivu ya Tumbo toka anakuwa binti na imefikia kipindi analazwa kwa siku 1 au 2 toka anasoma ili apate matibabu akiwa karibu na madaktari sababu wakati anasoma alikuwa anafika stage anazimia maumivu hayo yakizidi lakini baada ya kuwa mkubwa yakaanza kupungua. Mwaka jana, 2015, Diva alifanyiwa operesheni katika hospital ya Sanitas na ushauri alioambiwa ni akae kidogo halafu azae. Na sasa star uyo amefunguka na kusema atazaa Mtoto Mmoja tu na anaombea awe wa Kiume na baada ya hapo atafunga kizazi. "Naogopa sana kubeba mimba na kuzaa, so wil do that Mara Moja tu Kwa Miezi 9 then after that Ntafunga kizazi na Mtoto wangu nitaenda jifungulia nchi za Marekani ili apate uraia wa huko" Alisema Diva.

MTOTO WA KABWE AMCHUNIA MAKONDA

Image
Siku ya jana ilikua ni siku ya kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Ndg. Wilson Kabwe iliyofanyika viwanja vya Karimjee katikati ya Jiji la Dar es salaam. Katika hali ya kutoelewa nini kinachoendelea, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alijikuta akiganda kwa sekunde kadhaa mbele ya binti wa marehemu Wilson Kabwe anayefahamika kwanjina la Anna pale alipo jaribu kumpa mkono wa pole lakini binti huyo alikataa kujibu huku akibubujikwa na machozi ya uchungu. Habari kutoka kwa watu karibu wa familia zinasema binti huyo alifanya hivyo kutokana na machungu aliyokuwa nayo juu ya Makonda ambae wiki za usoni inaeleweka ya kwamba Mkuu huyo wa mkoa alikuwa mstari wa mbele kuchochea moto ambao ulisababisha Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumsimamisha kazi Mkurugenzi huyo . Habari za ndani zinasema kitendo hicho cha binti huyo cha kukataa mkono wa Makonda kimetokana na hotuba aliyotoa Mh. Makonda ambayo kwa maudhui ilikua im

Mamia Wauaga Mwili wa Kabwe Dar

Image
         Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene akipita mbele ya jeneza. Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda (kulia) akimpa pole mke wa Marehemu Kabwe aitwaye Faith Kabwe. Viongozi mbalimbali wakipita mbele ya jeneza kutoa heshima za mwisho. Mwanasiasa mkongwe hapa nchini, Kingunge Ngombale Mwiru (kulia) akipita mbele ya jeneza. Waombolezaji wakiendelea kutoa heshima za mwisho. Mamia ya waombolezaji wakiwa katika mstari kutoa heshima zao. Walioko mbele ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, Waziri George Simbachawene, Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi. Waombolezaji wakiwa katika viwanja vya Karimjee Dar. Mke wa marehemu Kabwe, Faith Kabwe (wa kwanza kulia) akiongozana na wanafamilia walipofika viwanja vya Karimjee. Jeneza lenye mwili likiwa limebebw