Boti yapotea Ziwa Nyasa...Watu Kadhaa Wahofiwa Kufa.


WATU kadhaa wanahofiwa kufa maji baada ya boti iliyokuwa ikifanya safari kutoka Mbamba Bay nchini Tanzania kwenda Nkhata Bay Malawi kuzama Ziwa Nyas na boti kutoweka. Duru  za usalama zinasema Boti hiyo haijulikani ilipo wala abiria waliokuwemo ndani yake jambo ambalo limezua sintofahamu kubwa, huku wakihofia kuzama.

Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma, kusini mwa Tanzania, Zuberi Mwombeji alisema haifahamiki ajali hiyo ilitokea aneo gani la Ziwa lakini juhudi za kuitafuta zinaendelea.

“…Usafiri wa kutoka Mbamba Bay mpaka Nkhata Bay huchukua saa tano mpaka sita, walipoona Nkhata Bay hawajafika waliwasiliana na watu wa Mbamba Bay ndipo ilipojulikana kuwa kuna tatizo limetokea,” alisema Kamanda Mwombeji.

Chanzo cha ajali hiyo kinaaminika ni hali mbaya ya hewa ziwani, hali inayoaminika kuwa ilisababisha Boti hiyo kupigwa dhoruba. Hata hivyo taarifa zinasema boti hiyo ikiwa njiani ilianza kuingiza maji ndipo juhudi za kuyatoa ndani ya boti zilianza kabla ya kuzidiwa.

Shughuli za kuisaka boti hiyo zinaendelea japo zilisimama leo kutokana na hali mbaya ya hewa katika Ziwa Nyasa. Tayari hofu kubwa imetanda kwa ndugu jamaa na marafiki wanaoamini huenda wenzao wamekufa maji kutokana na ajali hiyo.
Tangazo

Comments

Popular posts from this blog