Posts

Exclusiveee,,,....Radio EFM Wamnyakuwa Lady Jay Dee

Image
Wenyewe wanasema ‘Huu Mchezo Hauhitaji Hasira.’ Ni mchezo upi huo? Usemi huu ulianza baada ya EFM kuwapora watangazaji wawili wa Clouds FM, Gerald Hando na Paul James kabla ya wao nao kuporwa mtangazaji wao, Gardiner G Habash. Na sasa movie linaendelea kunoga. Lady Jaydee anayefahamika kuwa mgogoro mzito na Clouds FM na aliyekuwa mke wa Gardiner, amejiunga na EFM katika mradi ambao ni wao pekee wanaujua kwa sasa. Sitaki kuamini kama Lady Jaydee anaweza kurejea tena kwenye kazi yake ya utangazaji lakini kwa inavyoonekana, kuna kitu wamepanga kukifanya. Jaydee alishare picha na video kadhaa zinazomuonesha akitembezwa na kutambulishwa kwenye studio za EFM. “HuuMchezoHauhitajiHasira #NdiNdiNdi Efm feat Jide,” aliandika Jide kwenye picha moja. Kila mtu anasubiri kujua nini hasa Lady Jaydee na EFM wamepanga kukifanya

Daraja la Kigamboni kufunguliwa rasmi jumanne Aprili 19, 2016

Image
Viongozi Shrika la Taifa Hifadhi ya Jamii NSSF wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakandarasi wa daraja la Kigamboni wakati lilipofunguliwa kwa ajili ya kupita magari kupita bure huku watembea kwa miguu na waendesha baiskeli wakipita bure. Daraja hilo litazinduliwa rasmi na Rais Dk. John Magufuli Jumanne tarehe 19.4.2016. Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Karim Mataka akiwa katika eneo la daraja la Kigamboni mara baada ya kufunguliwa kwaajili ya kupita magari na waenda kwa miguu. Muonekano wa daraja la Kigamboni baada ya magari kuanza kupita. Eneo lililoandaliwa kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi wakati wa uzinduzi rasmi. Pikipiki na magari yakipita darajani. 71 ONLIE

FUVU LA MTU LAKUTWA OFISI YA DIAMOND PLATINUMZ

Image
Fuvu la binadamu lakutwa limewekwa kwenye meza ya Diamond pembeni ya picha ya mwanawe Tifah. Diamond asema ni kweli ni fuvu la binadamu, ila ni pambo tu kama mapambo mengine, yeye anamtegemea Mungu. Wakati mwenyewe akikanusha vikali kwamba hatumii ndumba kwenye muziki wake ambao sasa umemfikisha mbali kimataifa, staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’, ameshikwa uchawi kufuatia kukutwa laivu kwa fuvu la binadamu ndani ya ofisi zake. Fuvu hilo liko mkono wa kushoto mezani kwa Diamond huku jirani yake kukiwa na picha ya mwanaye, Latiffah Nasibu ‘Princess Tiffah’ iliyokuwa kwenye fremu. Shuhuda mmoja aliyehudhuria hafla ya kusaini mkataba wa dili jipya alilosaini Diamond la Ubalozi wa Tomato Sauce ofisini kwake hapo alilithibitishia kuwepo kwa fuvu hilo lilozua gumzo kwa mashuhuda wachache wa tukio hilo. “Ni kweli kuna fuvu la binadamu mezani kwa Mond (Diamond) but (lakini) sikufanikiwa kulishika kwa mikono yangu,” Shuhuda mwingine aliripoti pia: "Kuna ...

MWANAFUNZI MTANZANIA ASHIRIKI ONYESHO LA UBUNIFU LILILOANDALIWA NA RAIS BARACK OBAMA

Image
 .Oh "Kumbe kinafanya kazi hivi" ndivyo anavyoelekea kusema Rais Obama mara baada ya kuweza kukiendesha kifaa hicho kwa kutumia simu, aliyechuchuma ni Stephen Mwingira ambaye pamoja na Wendy Ni na Armon Halwan walipata fursa ya kuonyesha ubunifu wao katika onyesho la mwisho  lililoandaliwa na Rais  Barack Obana na kufanyika White House  April 13. 2016.  .Mwanafunzi  Armo Halwan akimuelekeza Rais  wa  Marekani,Barack Obama anavyoweza kutumia simu  kuendesha   cha  kufanyia usafi ( Vacuum Cleaner) kilichobuniwa na wanafunzi wa Baruch Collage Campus High School ya Jijini New York kupitia timu yao ya  ufumbuzi (Invent Teams)katikati ni Wendy Ni na anayefuatia ni  Stephen Mwingira ( mtanzania) anaonyesha  namna gani  kifaa hicho kinavyofanya usafi kwenye njia za treni za ardhini ( Subways).  Stephen  Mwingira na Wendy Ni, wakiangalia kwa makini  jinsi Rais Obama anavyoeleke...

OFISI YA BUNGE YALIVAA GAZETI LA NIPASHE,YALITAKA LIOMBE RADHI

Image
Ofisi ya Bunge imebaini upotoshwaji mkubwa Katika habari iliyochapishwa na Gazeti la Nipashe toleo la Aprili 16, 2016 yenye kichwa cha habari kisemacho “ Bunge sasa laufyata mkataba wa Lugumi”. Habari hiyo imeandikwa kufuatia ufafanuzi uliotolewa na Bunge jana kuhusu maagizo yaliyotolewa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) dhidi ya utekelezaji wa mkataba wa Jeshi la Polisi na Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd  kuhusu mradi wa utambuzi wa alama za vidole (AFIS) (Automated Fingerprint Identification System.) Ndani ya habari hiyo pia, Gazeti hilo limeeleza kuwa kamati ya PAC iliwahi kuliandikia Jeshi la Polisi kulitaka liwasilishe mkataba huo mbele ya Kamati, jambo ambalo si kweli bali ni upotoshwaji wa makusudi wenye lengo la kujenga hisia mbaya kuhusu mwenendo wa shughuli za Bunge mbele ya Umma. Ukweli ni kwamba PAC haijawahi kuliandikia jeshi la Polisi kama inavyodaiwa na Gazeti hilo. Nukuu ya  maelezo ya PAC katika Hansard kwa Afisa Masuhuli kuhusu jambo ...

RAIS MAGUFULI AFUNGUA RASMI MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA JUU (FLAI OVA) ENEO LA TAZARA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi na kuanza kwa ujenzi  wa mradi wa barabara ya juu Tazara Jijini Dar es Salaam.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akifungua  jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa barabara ya juu Tazara Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akifungua ramani ya mradi wa barabara ya juu eneo la Tazara kuashiria ufunguzi rasmi na kuanza kwa ujenzi  wa mradi huo Tazara Jijini Dar es Salaam.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipokea maelekezo kuhusu mradi wa barabara za juu eneo la Tazara kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wakala wa barabara (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale katika ufunguzi rasmi wa mradi huo Jijini Dar es Salaam.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbaliwa kitaifa na kimataifa wakati wa ufunguzi rasmi na kuanz akwa ujenzi...

Kajala amtolea chozi kigogo wa Wema!

Image
Kajala Masanja Na Imelda Mtema Siku chache baada ya gazeti dada na hili, Risasi Jumamosi kuandika juu ya aliyekuwa kigogo wa msanii Wema Sepetu, Clement Kiondo ‘CK’ kunaswa akiuza mishikaki, tukio hilo limemliza shosti wa Wema, Kajala Masanja. Kumwaga chozi kwa Kajala kumetokana na maelezo yake kwamba, baada ya kuiona habari hiyo hakuweza kuamini kama kweli ni CK yule aliyewahi kumtolea shilingi milioni 13 kama faini ili asiende jela kutokana msala aliokuwa nao. Wema Sepetu Akizunbumza na Ijumaa kwa majonzi, Kajala alisema: “Kiukweli nililia sana, nilishindwa kuamini kama kweli CK amefikia hali hiyo,” alisema Kajala ambaye pia aliwahi kudaiwa kutoka kimapenzi na jamaa huyo. Akasema stori hiyo isingekuwa imeambatana na picha asingeamini lakini alipoona zile picha zinazomuonesha CK akiwa jikoni akimhudumia mtu, alishindwa kujizuia na kujikuta akibubujikwa na machozi. Tukio la kunaswa kwa CK akiuza mishikaki lilinaswa na mapaparazi wetu juzikati kwenye baa m...

TTCL Yajivunia Modemu Mpya za Intaneti ya 4G

Image
Afisa Mauzo Mkuu wa TTCL Shop Mwananyamala, Dar, Bi. Leyla Pongwe (katikati) akielezea namna ambavyo huduma ya 4G  LTE na router mpya ya TTCL inavyofanya kazi, kushoto ni Afisa Masoko, Bi. Mboka Kategela kutoka Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Mwananyamala na kulia ni Afisa Mauzo, Bw. Chacha Ghati Mosenye walipofanya mahojiano na Global TV Online leo. Afisa Masoko Kutoka TTCL Extelecom, Samora Avenue -Dar, Bw. Joel J. Goyayi akielezea namna ambavyo modem zao zinavyofanya kazi. Wakisikiliza swali kutoka kwa mwandishi wa habari wa Global Publishers, Andrew Carlos (hayupo pichani) kuhusu uboreshwaji wa vifurushi vya intaneti vya TTCL. Bi. Mboka Kategela (kushoto) akishika modemu ya Mi-Fi wakati Bi. Leyla Pongwe akishika vocha ya TTCL ya Tsh. 5000/=. Wakitambulisha bidhaa hizo kwa wanahabri wa Global Publishers. Wakiwa kwenye picha ya pamoja. Wakisikiliza swali kutoka kwa mmoja wa wanahabari. Maofisa Masoko kutoka TTCl wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya w...

HAWA NDIO MASTAA WA BONGO WALIOSHINDWA KUTIMIZA AHADI ZAO

Image
Mastaa wengi wa Bongo wamekuwa wakiahidi vitu vingi kwa mashabiki wao lakini vitu hivyo vinakuwa vinapotea hewani bila ya kutekelezeka. ‘Ahadi ni deni’, watu wengi wanakuwa wanasahau maneno ambayo mwanzo waliyasema wenyewe na bila hata ya kurudisha tena mrejesho kwa mashabiki wao juu ya kauli zao za mwanzo walizozisema. Baadhi ya mastaa wameshaanza kupoteza uaminifu kwa mashabiki wao kutokana na kuahidi kuja na vitu vingi lakini muda umezidi kwenda na mambo yanazidi kubadilika huku kauli zao zikiwa hazitekelezwi. Hawa ni baadhi ya mastaa walioshindwa kutekeleza ahadi zao kwa mashabiki wao. Wema Sepetu Ni mwaka mmoja takribani Madam atoe ahadi ya kuachia movie aliyofanya na staa wa movie kutoka Ghana, Van Vicker. Ni kweli kuna kipindi Sepetunga hakuwepo nchini kwa muda kidogo na alidai kuwa anaenda kushoot movie yake na staa huyo wa Ghana. Aliwahi kusema alifanya connection na Van Vicker kupitia Instagram. Movie hiyo hadi leo haijatoka. Naamini ...

Rais Salva Kiir Mayardit wa Sudani Kusini Awasili Tanzania

Image
Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye kofia nyeusi) akishuka katika ndege ya Shirika la Kenya mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam. Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit akiongozana na rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Augustine Mahiga (kushoto) akisalimiana na Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam. Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Richard Sezi...