TTCL Yajivunia Modemu Mpya za Intaneti ya 4G

TTCL (8)
Afisa Mauzo Mkuu wa TTCL Shop Mwananyamala, Dar, Bi. Leyla Pongwe (katikati) akielezea namna ambavyo huduma ya 4G  LTE na router mpya ya TTCL inavyofanya kazi, kushoto ni Afisa Masoko, Bi. Mboka Kategela kutoka Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Mwananyamala na kulia ni Afisa Mauzo, Bw. Chacha Ghati Mosenye walipofanya mahojiano na Global TV Online leo.TTCL (5)Afisa Masoko Kutoka TTCL Extelecom, Samora Avenue -Dar, Bw. Joel J. Goyayi akielezea namna ambavyo modem zao zinavyofanya kazi. TTCL (7)Wakisikiliza swali kutoka kwa mwandishi wa habari wa Global Publishers, Andrew Carlos (hayupo pichani) kuhusu uboreshwaji wa vifurushi vya intaneti vya TTCL.TTCL (1)Bi. Mboka Kategela (kushoto) akishika modemu ya Mi-Fi wakati Bi. Leyla Pongwe akishika vocha ya TTCL ya Tsh. 5000/=.TTCL (2)Wakitambulisha bidhaa hizo kwa wanahabri wa Global Publishers.TTCL (3)Wakiwa kwenye picha ya pamoja.TTCL (6)Wakisikiliza swali kutoka kwa mmoja wa wanahabari.TTCL (4)
Maofisa Masoko kutoka TTCl wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Global Publishers, Kitengo cha Teknolojia ya  Habari.
mkali,
MAOFISA Masoko kutoka Kampuni ya Mawasiliano ya TTCL wametembelea televisheni ya mtandaoni ambayo ni namba moja nchini, Global TV Online na kufanya mahojiano maalum ambayo yalikuwa na lengo la kuwajulishwa Umma wa Watanzania na watumiaji wa huduma za intaneti kuwa, kampuni hiyo imeingiza sokoni vifaa vya intaneti vinavyotumia na teknolojia ya 4G yenye kasi zaidi.
Akizungumza kwenye mahojiano hayo, Afisa Mauzo Mkuu wa TTCL Shop Mwananyamala, Dar, Leyla Pongwe alisema kuwa, TTCL wamekuja na huduma ya 4G LTE ambayo mtumiaji wake atapata inateti ya kasi zaidi kwenye data na voice kwa wale waishio jijini Dar es Salaam.
Mbali na hivyo TTCL wamkuja na vifaa maalum kwa matumizi ya intaneti, baadhi ya vifaa hivyo ni USB Modem inayotumika kwa kompyuta moja, modem ya wireless (Mi-Fi) inayoweza kuunganisha hadi vifaa 10 vinavyotumia intaneti pamoja na CPE router inayoweza kuunganisha hadi vifaa 32 vinavyotumia intaneti pia inatumia wireless na cabling.
Hata hivyo Maofisa Masoko wa TTCL, Joel J. Goyayi na Mboka Kategela hawakusita kuelezea kuwa, huduma ya 4G kwa sasa inapatikana Dar es Salaam pekee na bado kampuni hiyo inazidi kujenga miundombinu ya kufikisha huduma hiyo mikoa mingine ya Tanzania.
PICHA NA HILARY DAUD/GPL

Comments

Popular posts from this blog