Katibu Mkuu mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Vicent Mashinji, akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho, usiku wa kuamkia leo mara baada ya kuchaguliwa, kwenye Mkutano Mkuu uliokuwa ukifanyika Jijini Mwanza. Dkt. Mashinji anaziba nafasi iliyoachwa wazi na Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dkt. Willbload Slaa. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, Makamu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Mh. Said Issa Mohamed pamoja na Mjumbe wa Mkutano Mkuu, Mh. Edward Lowassa wakifarilia kwa makini hotuba ya Katibu Mkuu mpya wa Chama hicho, Dkt. Vicent Mashinji (hayupo pichani). Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA wakishangilia baada ya kupatikana bila kwa Katibu Mkuu mpya, Dkt. Vicent Mashinji. WASIFU WA DK. VECENT MASHINJI Dk. Mashinji aliyezaliwa katika Wilaya ya Sengerema, alianza elimu ya msingi katika Shule ya Iligamba Januari 1981 hadi Oktoba 1987 na kisha kue...