Posts

MAOMBI MAALUM YA KUMWOMBEA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI NA SERIKALI YAKE YAFANYIKA JIJINI MBEYA

Image
Baadhi ya maaskofu kutoka makanisa mbalimbali Mkoani Mbeya wakiwa wamshika Picha ya Rais na ramani ya Tanzania wakati wa maombi maalum ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na serikali yake katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mkapa jijini Mbeya. Picha ya Rais Dkt John Pombe Magufuli ikiwa imeshikwa na maaskofu wa makanisa mbalimbali Mkoani Mbeya kwa ajili ya kufanya maombi maalumu kwa ajili ya rais na serikali yake katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya .  Muongozaji Mkuu wa Maombi ya kumwombea Rais Dkt John Pombe Magufuli ,Askofu Dkt Charles Gadi wa kanisa la The City of refuge Church yenye makao makuu jijini Dar es salaam akizungumza na waumini walioshiriki katika maombi hayo katika ukumbi wa Mkapa .  Askofu Dkt Charles Gadi wa kanisa la The City of refuge Church yenye makao makuu jijini Dar es salaam akizungumza na waumini walioshiriki katika maombi ya kumwombea Rais Dkt John Pombe Magufuli na serikali yake ...

PROF. MUHONGO AAGIZA MALIPO YA USHURU WA HUDUMA YAFANYIKE HADHARANI

Image
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kutoka kulia) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa mgodi. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Zelothe Stephen  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akiwasili katika mgodi wa dhahabu wa Cata Mining. Kulia ni Mkurugenzi wa mgodi huo, Mahuza Nyakirang’ani.  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akikagua shughuli zinazoendelea mgodini hapo. Kushoto kwake ni Meneja wa mgodi huo, Peter Bourhill na kulia kwake ni Mkurugenzi wa mgodi,  Mahuza Nyakirang’ani.  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akisalimiana na baadhi ya wananchi kutoka vijiji vya jirani na mgodi wa Cata Mining waliohudhuria mkutano wake wa hadhara ili kujadili masuala mbalimbali.  Meneja wa mgodi wa Cata Mining, Peter Bourhill akimweleza jambo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alipokua akikagua m...

ORODHA KAMILI YA WAHANGA WA AJALI LEO KATIKA AJALI BARABARA YA MANDELA

Image
  Ajali mbaya sana asubuhi hii barabara ya Mandela eneo la karibu na Daraja la Matumbi. Haitazamiki baada Roli lililokuwa limebeba  ng’ombe kuvaana uso kwa uso na daladala Toyota  DCM  linalofanya safari zake katika ya Gongo la Mboto na Ubungo  limefyekwa lote Taarifa kutoka kwa Stanley Binagi Daktari Kiongozi wa Hospitali ya Amana zinasema zilipokelewa maiti 3 kutokana na ajali hiyo na majeruhi walikuwa 26 hata hivyo majeruhi mmoja alifariki mara baada ya kusikishwa hospitali ya Amana na kufanya idadi ya waliokufa katika ajali hiyo kufikia 4 huku baadhi ya majeruhi wakihamishiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Foleni ilikuwa ni kubwa sana na jitihada za kuyatoa magari hayo kutoka kikosi cha usalama barabarani zilifanyika  na kupunguza foleni katika barabara hiyo. Baadhi ya Ng’ombe walionusurika kwenye ajali  wakitapakaa hovyo barabarani mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo. ...

RAIS WA VIETNAM, MHE. TRUONG TAN SANG AWASILI TANZANIA

Image
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikianowa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Augustine Mahiga (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki wakati wa kumpokea Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 08 Maachi, 2016 Jijini Dar es Salaam.   Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Augustine Mahiga (kushoto), Mkuuwa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (katikati) pamoja na Mkuu wa Wilayaya Kinondoni Paul Makonda wakiteta jambo wakati wa kumpokea Rais wa Vietnam,Mhe. Truong Tan Sang katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 08 Maachi, 2016 Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya Halotel wakiwa tayari kumpokea Rais wao wa Vietnam Mhe. Truong Tan Sang akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016  Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya...