ORODHA KAMILI YA WAHANGA WA AJALI LEO KATIKA AJALI BARABARA YA MANDELA

 

AJI1
Ajali mbaya sana asubuhi hii barabara ya Mandela eneo la karibu na Daraja la Matumbi. Haitazamiki baada Roli lililokuwa limebeba  ng’ombe kuvaana uso kwa uso na daladala Toyota  DCM  linalofanya safari zake katika ya Gongo la Mboto na Ubungo  limefyekwa lote Taarifa kutoka kwa Stanley Binagi Daktari Kiongozi wa Hospitali ya Amana zinasema zilipokelewa maiti 3 kutokana na ajali hiyo na majeruhi walikuwa 26 hata hivyo majeruhi mmoja alifariki mara baada ya kusikishwa hospitali ya Amana na kufanya idadi ya waliokufa katika ajali hiyo kufikia 4 huku baadhi ya majeruhi wakihamishiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Foleni ilikuwa ni kubwa sana na jitihada za kuyatoa magari hayo kutoka kikosi cha usalama barabarani zilifanyika  na kupunguza foleni katika barabara hiyo.
AJI2
Baadhi ya Ng’ombe walionusurika kwenye ajali  wakitapakaa hovyo barabarani mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo.
AJI3
Haya ndiyo mabaki ya daladala hilo.
AJI4
Askari wa kikosi cha usalama barabarani akitekeleza majukumu yake mara baada ya ajali hiyo.

Comments

Popular posts from this blog