Baraza Kuu La CUF Lakataa Kurudia Uchaguzi Zanzibar!
Baraza Kuu la Chama cha Wananchi (CUF), limekutana na kusisitiza kuwa hawatarudia uchaguzi wa Zanzibar. Mkutano huo ulifanyika jana mjini hapa ambapo walijadili mkwamo wa kisiasa nchini na juhudi zinazoendelea katika kukabiliana na hali hiyo. Naibu katibu mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazrui alikaririwa akisema baada ya kikao hicho, “ Wanaosema uchaguzi urejewe waachieni wenyewe, sisi katika CUF hakuna habari hiyo. Kwa sasa kutangaza matokeo ya uchaguzi ndiyo msimamo wetu, ili mshindi atangazwe na kuapishwa .” alisema Mazrui Awali Kaimu Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, Twaha Taslima akiwa na safu ya juu ya uongozi wa chama hicho, walisema kuna haja ya kuendelea kutafuta haki ya Wazanzibari kwa kuitaka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kutangaza matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka huu, ili mshindi ajulikane na aweze kuapishwa. Taslima alisema pia baraza hilo lilibariki juhudi za mgombea urais wa Zanzibar kupitia CUF akiungwa mkono na Ukawa, Maalim Seif Sharif Hamad k