Posts

WABUNGE WALIOSHINDA UCHAGUZI WA 2015

Image
%3 No. MBUNGE JIMBO CHAMA 1 Dk Charles Tizeba Buchosa CCM 2 Nimrod Mkono Butiama CCM 3 Omar Badwel Chilonwa CCM 4 Kanyasu John Geita Mjini CCM 5 Pudensiana Kikwembe Kavuu CCM 6 Sixtus Mapunda Mbinga Mjini CCM 7 Hassan Masala Nachingwea CCM 8 Abdallah Chikota Nanyamba CCM 9 Richard Mbogo Nsimbo CCM 10 Ester Matiko Tarime Mjini CHADEMA 11 Mwakajoka Frank Tunduma CHADEMA 12 Joshua Nassari Arumeru Magharibi CHADEMA 13 Dk Shukuru Kawambwa Bagamoyo CCM 14 Andrew Chenge Bariadi Magharibi CCM 15 Oscar Mukasa Biharamulo Magharibi CCM 16 Wilfred Lwakatare Bukoba Mjini CHADEMA 17 Jasson Rwikiza Bukoba Vijijini CCM 18 Dotto Biteko Bukombe CCM 19 Eshter Bulaya Bunda Mjini CHADEMA 20 Raphael Chegeni Busega CCM 21 Atupele Mwakibete Busekelo Rungwe Mashariki CCM 22 Bilango Samson Buyungu CHADEMA 23 Ridhiwani Kikwete Chalinze CCM 24 Anthony Mavunde Dodoma Mjini CCM 25 ...

MAJINA YA WABUNGE WA VITI MAALUM

Image
source: global pbl

RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AKUTANA NA MAKATIBU WAKU WA SERIKALI LEO IKULU

Image
Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bwana Rished Bade na Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es s...

USIYOYAFAHAMU KUHUSU FIRST LADY MAMA JANETH MAGUFULI

Image
Kila mzazi anapokaribia kupata mtoto, moja ya mambo muhimu ambayo hufikiria juu ya jina la kumpatia baada ya kujifungua na mtoto kuishi duniani.  Wazazi wengi huchukua muda kufikiria ni jina gani zuri la kumpa mtoto wao. Kuna wakati baadhi ya wazazi hufikia hatua ya kuvutana kuhusu jina tu.  Kuvutana huko kunatokana na umuhimu wa jina kwa sababu inaaminika kila jina lina maana yake na tabia zake zitaakisiwa nalo.  Kuna majina ambayo hupendwa sana kutokana na dhana kwamba watu wanaopewa majina hayo huwa na tabia nzuri, upeo mkubwa, uvumilivu na wengine bahati.  Je, ikitokea unabahatika kupata mtoto wa kike uliyemtafuta kwa muda mrefu, utampa jina gani? Huenda jina Janeth likawa miongoni mwa matatu au 10 utakayoorodhesha ili kuchagua moja la kumpa binti yako.  Kama halitakuwapo basi fanya mpango wa kuliweka kwa sababu jina hilo ndiyo habari ya mjini kwa sasa.  Kwa nini jina la Janeth ni habari ya mjini? Siku Dk John Magufuli alip...

RAIS JOHN MAGUFULI AKIWA OFISINI KWAKE SIKU YA KWANZA

Image
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akifanyakazi ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni siku yake ya kwanza ofisini kwake tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya tano. (Picha na Freddy Maro)

TB. JOSHUA ATOA MPYA ASHUKA UWANJA WA NDEGE BONGO BILA VIATU

Image

MAKAMU WA RAIS AIFARIJI FAMILIA YA RUBANI WILLIAM SLAA

Image
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kumfariji Meya wa Manispa ya Ilala Mhe. Jery Slaa alipofika nyumbani kwao Gongolamboto jijini Dar es salaam leo Octoba 20, 2015 kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kufuatia kifo cha Baba yake Marehemu Rubani William Slaa aliyefariki wiki iliyopita kwa ajali ya Hekopta.   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kumfariji Bibi Tabita Slaa aliyekuwa Mke wa Marehemu Rubani William Slaa aliyefariki wiki iliyopita kwa ajali ya Hekopta wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Gongolamboto jijini Dar es salaam leo Octoba 20,2015 kwa ajili ya kutowa mkono wa pole. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo kufuatia kifo cha marehemu Rubani William Slaa aliyefariki Dunia wiki iliyopita kwa ajali ya Helkopta wakati Makamu ...

RAIS KIKWETE AFANYA UTEUZI MPYA,

Image
RAIS Jakaya Kikwete amemteua Awadh Massawe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA). Rais alitangaza uamuzi huo Ijumaa iliyopita wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa bandari mpya ya Bagamoyo inayotajwa kuwa kubwa katika Afrika. Akihutubia katika hafla hiyo, Rais Kikwete alisema yeye alishamaliza uteuzi huo na kumwambia Massawe afuatilie barua yake rasmi ya uteuzi. Kabla ya uteuzi huo, Massawe alikuwa akikaimu nafasi hiyo tangu Februari mwaka huu, huku akitajwa kufanikiwa hadi sasa kufanya mageuzi makubwa katika kuleta ufanisi katika bandari hapa nchini. Kabla ya kukaimu nafasi hiyo, alikuwa Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam. Baada ya kuwa Kaimu Mkurugenzi, alianzisha mikutano ya wadau yenye lengo la kurudisha mahusiano yaliyokuwa yameyumba kati ya pande hizo mbili. Mikutano hiyo inayofanyika kila Alhamisi ya mwisho ya kila mwezi inalenga kuhusisha wadau mbalimbali katika majadiliano ya jinsi ya kuboresha ufanisi katika...

Maneno Ya Lowassa jinsiAlivyopokea Kifo Cha Filikunjombe

Image
Ni taarifa ya kushtusha sana ya msiba wa mwanasiasa chipukizi na jasiri, Deo Filikonjombe kutokana na ajali ya Helikopta jana jioni maeneo ya mbunga ya Selous mkoani Morogoro. Ni pigo lingine kubwa ambalo katika kipindi kifupi Taifa limepata, huku bado likiwa na kidonda cha kuondokewa na wana siasa wengine mahiri,Marehemu Celina Kombani, Dr Abdallah Kigoda na Dr Emanuel Makaidi aliyefariki jana Filikonjombe alikuwa Mbunge mahiri aliyesimama imara kutetea maslahi ya wananchi wa jimbo lake la Ludewa na watanzania kwa ujumla. Alikuwa mwiba kwa serikali ya Chama chake CCM kutetea maslahi ya nchi, mfano ni katika kashfa ya Escrow ambapo alikuwa Makamu Mwenyekiti wa kamati iliyochunguza kashfa hiyo. Mwenyezimungu awape moyo wa subira, familia, jamaa, marafiki na wananchi wa Ludewa, katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao. BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE. -Edward Ngoyai Lowassa

Rais KIKWETE atoa heshima zake za mwisho kwa Marehemu Deo Filikunjombe na wenzake wawili waliofariki katika ajali ya helikopta

Image
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgombea Urais wa tiketi ya CCM Dkt.John Pimbe Magufuli wakitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza ya aliyekuwa Mbunge wa Ludewa(CCM) Marehemu Deo Filikunjombe na wenzake wawili waliofariki katika ajali ya helikopta juzi katika pori la akiba la mbuga ya Selous. Marehemu aliagwa katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Mke wa Marehemu Bi Sarah Filikunjombe wakati wa kuaga mwili wa marehemu katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015. (picha na Freddy Maro)

SIRI YAFICHUKA YA CHANZO CHA AJALI YA CHOPA ILIYO MUUA "DEO FILIKUNJOMBE"

Image
Dar es Salaam. Mgombea ubunge wa Jimbo la Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe na wenzake watatu, akiwamo Kepteni William Silaa wamefariki dunia katika ajali ya helikopta, ambazo wataalamu wanasema husababishwa na kosa la kibinadamu la rubani. Katibu wa Bunge, Thomas Kashilillah alisema jana kuwa walipata taarifa ya ajali hiyo na kuthibitisha kuwa watu wote wanne waliokuwa kwenye helikopta hiyo walifariki dunia. Miili ya Marehemu Filikunjombe, Kepteni Silaa na wengine iliwasili jijini Dar es Salaam jana jioni kwa helikopta ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania, lakini hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu taratibu za mazishi. Hii ni ajali ya sita ya ndege aina ya helikopta, maarufu kwa jina la chopa, katika kipindi cha miaka miwili huku Filikunjombe, ambaye alikuwa mbunge wa Ludewa kuanzia mwaka 2010, akiwa mgombea wa tano kupoteza maisha tangu mchakato wa Uchaguzi Mkuu uanze. Mbali na ajali iliyomuhusisha Joshua Nasari mkoani Arusha, nyingine ilitokea Aprili mwaka jana ikimuhusisha mgo...

DK. MAGUFULI AONGOZA KUAGA MWILI WA DEO FILIKUNJOMBE

Image
  Dr Magufuli akiwa lugalo hospital kumuaga marehemu Deo Filikunjombe.halo akiwa na mke wa marehemu.

ERIC SHIGONGO: NENDA KAMANDA WANGU DEO

Image
Nakupenda Deo Nimesikitishwa sana na kifo chako. Kweli kifo kipo na kila mmoja wetu atakipitia lakini cha aina hii, cha kijana aliyekuwa akipigania watu wake kiasi hiki? Kinaumiza sana, hata hivyo, hatuna budi zaidi ya kukubali kuwa Deo Filikunjombe, jembe la mkono limeondoka. Chopa iliyosababsha kifo cha Filikunjombe, Capt. William Silaa na watu wengine wawili. Nasema kutoka ndani ya moyo wangu, taifa limepoteza mtu muhimu sana, hakusita kupigania alichokiamini bila uoga wala hofu! Wakati mwingine alitofautiana na msimamo wa chama chake kwa maslahi ya Watanzania maskini, kwako ukweli ulikuwa nguzo. Nenda Deo, nenda kapumzike muda si mrefu tutaungana nawe, kila mwanadamu atafariki dunia maana ndivyo ilivyoandikwa. Lakini cha muhimu ni mtu atakuwa anafanya nini wakati anakufa! Je, atakuwa akiiba au akifanya uzinzi? Deo umekufa ukitumikia watu wako, umekufa kifo chema na Wanaludewa watakuombea. Nenda Deo, pumzika Deo, mema yako yamekutangulia. Hayo ndyo yatakutetea mbele ya ...

MIILI YA MAREHEMU DEO FILIKUNJOMBE NA WENGINE WAWILI YAAGWA LUGALO

Image
Mbunge wa Jimbo la Ludewa aliyekuwa anamaliza muda wake, Deogratias Filikunjombe enzi za uhai wake. Majeneza yenye miili ya marehemu yakiandaliwa kwa kuagwa. Ndugu, jamaa na marafiki wakipita kwenye majeneza yenye miili ya marehemu kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho. Waombolezaji wakionekana wenye huzuni wakati wa kuaga miili ya marehemu.… Mbunge wa Jimbo la Ludewa aliyekuwa anamaliza muda wake, Deogratias Filikunjombe enzi za uhai wake. Majeneza yenye miili ya marehemu yakiandaliwa kwa kuagwa. Ndugu, jamaa na marafiki wakipita kwenye majeneza yenye miili ya marehemu kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho. Waombolezaji wakionekana wenye huzuni wakati wa kuaga miili ya marehemu. Zoezi la kuaga miili ya marehemu hao likiendelea. Waombolezaji wakiwa katika msitari kuelekea eneo yalipowekwa majeneza hayo kwa ajili ya kuaga. Mke wa marehemu Deo Filikunjombe, Sarah Filikunjombe (kushoto) akilia kwa uchungu. Nyumbani kwa Deo Filikunjombe, Mtoni-Kijichi, Dar es Salaam. P...

BARAZA KUU LA WAISLAMU MKOA WA MWANZA LAMUONYA ASKOFU GWAJIMA.

Image
Jana Ijumaa ya Octoba 16,2015 Baraza Kuu la Waislamu Mkoa wa Mwanza liliungana na Waislamu wengine kuadhimisha mwaka mpya wa Kiislamu ambao ni 1437. Kwa kalenda ya Kiislamu sherehe hizo zilifanyika jana tarehe mbili, mwezi Muharamu mwaka wa 1437 (02.01.1437) ikiwa maadhimisho yanayoambatana na kumbukumbu ya Kuhama kwa Mtume Muhammad kutoka Mji wa Macca kwenda Madina. Na: George Binagi-GB Pazzo Katika kuadhimisha sherehe hizo, Baraza hilo kupitia kwa Katibu wake Mkoani  Mwanza Sheikh Mohamed Balla (Kulia Pichani) alitoa tamko kwa niaba ya Waislamu wote Mkoani Mwanza kutokana na kauli inayoelezwa kutolewa na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima kwamba ana ndoto ya Misikiti yote nchini kugezwa kuwa Sunday School na Masheikh watakwenda kuangukia katika misalaba. Alisema kauli za namna hiyo si njema kwa mstakabali wa Taifa ambapo alisema kuwa Waislamu wote Mkoani Mwanza wanalaani na kukemea kauli hiyo na nyingine zote za aina hiyo na wale wanaozitoa. Aliwataka Watanza...