Posts

RAIS KIKWETE AZINDUA MAJENGO PACHA YA GHOROFA 35 YA PSPF TOWERS MTAA WA SOKOINE JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Image
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa pensheni wa PSPF Bw.  Adam Mayingu alipowasili kuzindua majengo pacha ya ghorofa 35 ya PSPF TOWERS mtaa wa Sokoine jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015  Mrisho Mpoto na Mjomba Band wakitumbuiza kwenye sherehe za  majengo pacha ya ghorofa 35 ya PSPF TOWERS mtaa wa Sokoine jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dr. Ramadhani Dau   alipowasili kuzindua majengo pacha ya ghorofa 35 ya PSPF TOWERS mtaa wa Sokoine jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015   majengo pacha ya ghorofa 35 ya PSPF TOWERS mtaa wa Sokoine jijini Dar es salaam yaliyozindulia  leo Septemba 16, 2015   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea jambo na  Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa pensheni wa PSPF  Mkurugenzin Mkuu  wa  Mfuko  wa  Pensh...

Wafanyakazi waliofichua ukweli kuhusu kikao cha Dr. Slaa Serena Hotel wafukuzwa kazi

Image
Kama mnavyokumbuka mwezi huu tarehe 1 aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema Dr Slaa aliitisha kikao cha waandishi wa habari pale Serena Hotel, ambapo mkutano huo ulirushwa LIVE na vituo vya televisheni vipatavyo vitano na radio kadhaa nazo zikarusha mkutano huo moja kwa moja. Katika mkutano huo alitangaza rasmi kujivua Ukatibu Mkuu wa Chadema na uanachama pia wa Chama hicho na kueleza kuwa anastaafu kabisa shughuli za siasa na kwa hiyo akaeleza kuwa hana nia ya kujiunga na chama chochote cha siasa. Hata hivyo katika kikao hicho ambapo alitumia zaidi ya saa 1 kuongea ambapo alikitumia kikao hicho karibu chote kuporomosha mashambulizi mfululizo kwa chama chake cha Chadema na vyama vinavyounda Ukawa na kumshambulia Edward Lowassa kwa nguvu zake zote na kumuita fisadi mkubwa na kukilaumu chama chake kwa kumpokea Lowassa na kupewa fursa ya kugombea Urais kwa tiketi ya chama cha Chadema kuwa ni sawasawa na kukihamisha choo kutoka chumbani na kukipeleka sebuleni. Baada ya kika...

HIZI NDIO KAULI ZA MBATIA AKIHTUBIA KUPITIA RUNINGA USIKU HUU

Image
- Mbatia analalamikia vitisho vya Mgombea wa CCM, Magufuli kuwa wakiwachagua wapinzani nchi itaingia kwenye machafuko - Mbatia: Watu wameanza kupoteza maisha, wana UKAWA wanadhalilishwa na wengine kutekwa - Mbatia: Hali imeanza kuwa tete, vitisho vya kila aina vimeanza. Tumedhalilishwa sana, tumeitwa matusi ya kila aina. - Mbatia: Lowassa si mdini, alikuwa anataka watanzania wamwombee. Mhe. Lowassa hajaenda kwenye nguvu za giza. Hajatumia viungo vya albino, ameenda kuomba viongozi wa dini wamwombee; udini wake unatoka wapi? - Mbatia: Tunawashukuru Lowassa na Sumaye kwa nia zao njema kuja Upinzani kuongeza nguvu ili tuyafanye mabadiliko ya kweli - Mbatia: Hata CCM wangemweka malaika, si rahisi kupata mabadiliko bila kufanya mabadiliko ya mfumo. - Mbatia: CCM wanasema usichague chama, chagua mtu. Watanzania wanatakiwa kujua kuwa Magufuli ni CCM, na hawezi kujitenganisha na CCM. Huwezi kulisukuma gari ukiwa ndani yake, lazima utoke ndipo ulisukume. Mabadiliko ndani ya CCM hayaw...

MTANGAZAJI WA CLOUDS FM DJ FETTY ATANGAZA KUACHAZA KAZI

Image
Jina lake ni Fatma Hassan aka DJ Fetty, moja ya Watangazaji ambao wamepata majina makubwa sana TZ na East Africa kutokana na kazi ya Utangazaji ambapo ana mchango mkubwa pia kwenye muziki wa Bongo Fleva kama Mtangazaji wa show ya Entertainment,XXL ya Clouds FM. September 15 2015 Show ya XXL inaandika Historia nyingine tofauti ambapo DJ Fettyametangaza kuacha kazi ya Utangazaji na kuingiza nguvu yake zaidi kwenye masuala ya Biashara… wakati Fetty anatangaza hivyo, presenter mwingine pia Kened the Remedyameungana na Timu ya XXL kwa mara ya kwanza. Ndani ya Studio ya Clouds FM, hapo yuko Kennedd, Adam Mchomvu, DJ Zero, B Dozen na DJ Fetty.

LINNAH ATUPIA PICHA MATATA

Image
  Linnah with Mbasha and Mr Blue!!

JK AMTAJA MUHUSIKA WA RICHMOND.

Image
 Rais Jakaya Kikwete amesema anashangazwa na Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu kumtaka amtaje mhusika wa Richmond wakati mwenye Richmond yupo na anatembea naye mikoani. Kikwete aliyasema hayo jana wakati akiwaaga wananchi wa Kigoma katika Uwanja wa Lake Tanganyika na kumtaka Lissu amtaje mwenye Richmond. “Endapo Tundu Lissu atashindwa kumtaja mwenye Richmond, nitatoka hadharani na kumtaja mwenyewe,” alisema Kikwete. Kabla ya mkutano huo, Rais Kikwete alifungua jengo la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, (NSSF) ambalo limejengwa kwa Sh7 bilioni. Akifungua jengo hilo, aliwaomba wawekezaji na mifuko ya kijamii kuiga mfano wa NSSF kwa kuwekeza katika sekta ya majengo kwa kuwa yanapendezesha mji. Kadhalika, Rais Kikwete alizindua jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na nyumba 36 za bei nafuu zilizopo katika eneo la Mlole, Kigoma Mjini. Richmond Suala la Richmond imekuwa moja ya ajenda za CCM katika kampeni za urais hasa baada ya Waziri ...

John Mnyika amtetea vikali Dr.Slaa Adai Yaliyotokea ni Kama Samsoni kwa Delila

Image
Mnyika amemtetea vikali Dr.Slaa na kupingana na wale wanaomkejeli na kumuona hana mchango CHADEMA. Mnyika anasema Dr.Slaa anao mchango wake na yaliyomkuta ni mambo kama yaliyowahi kumkuta Samsoni kwa Delila. Naomba kuisha hapa.

LOWASSA AENDELEA NA KAMPENI ZA KUSAKA URAIS SHINYANGA

Image
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiongozana na aliekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Ndg. Hamis Mngeja wakiwapungia wananchi wa Mji wa Kahama, wakati wakiwasili kwenye Uwanja wa Stendi mpya, Nyasubi, Kahama Mjini leo Septemba 14, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI . Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akipokelewa na Mwenyeji wake, Mgombea Ubunge wa Ukawa kupitia CHADEMA, Mh. James Lembeli, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Stendi mpya, Nyasubi, Kahama Mjini leo Septemba 14, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo. Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akilakiwa na maelfu ya wakazi wa mji wa Kahama, leo Septemba 14, 2015. Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Ch...