Wafanyakazi waliofichua ukweli kuhusu kikao cha Dr. Slaa Serena Hotel wafukuzwa kazi

Kama mnavyokumbuka mwezi huu tarehe 1 aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema Dr Slaa aliitisha kikao cha waandishi wa habari pale Serena Hotel, ambapo mkutano huo ulirushwa LIVE na vituo vya televisheni vipatavyo vitano na radio kadhaa nazo zikarusha mkutano huo moja kwa moja.

Katika mkutano huo alitangaza rasmi kujivua Ukatibu Mkuu wa Chadema na uanachama pia wa Chama hicho na kueleza kuwa anastaafu kabisa shughuli za siasa na kwa hiyo akaeleza kuwa hana nia ya kujiunga na chama chochote cha siasa.

Hata hivyo katika kikao hicho ambapo alitumia zaidi ya saa 1 kuongea ambapo alikitumia kikao hicho karibu chote kuporomosha mashambulizi mfululizo kwa chama chake cha Chadema na vyama vinavyounda Ukawa na kumshambulia Edward Lowassa kwa nguvu zake zote na kumuita fisadi mkubwa na kukilaumu chama chake kwa kumpokea Lowassa na kupewa fursa ya kugombea Urais kwa tiketi ya chama cha Chadema kuwa ni sawasawa na kukihamisha choo kutoka chumbani na kukipeleka sebuleni.

Baada ya kikao hicho kwisha kesho yake ikatumbukizwa clip kwenye mitandao ya kijamii ambapo mfanyakazi mmoja wa kike wa Hoteli hiyo aliyatambulika kwa jina la Neema alisikika akielezea namna kikao hicho kilivyoandaliwa na kugharimiwa gharama zote na KITENGO na namna Dr Slaa alivyokuwa amepangiwa chumba katika Hoteli hiyo na KITENGO siku moja kabla na kuwa siku hiyo kabla ya kufanyika kikao hicho Dr Slaa alilala hotelini hapo akiwa na 'mchumba' wake Josephine Mushumbusi.

Dada huyo jasiri na shujaa aliendelea kueleza kwenye clip hiyo namna watu wa KITENGO wakishirikiana na idara ya usalama wa Hoteli hiyo ambavyo walikuwa wakimuingiza kwa kificho hotelini hapo Dr Slaa na mkewe pamoja na Dr Mwakyembe ambaye alikutana na Dr Slaa na kuongea naye kwa masaa matatu kabla ya kikao chake hicho na waandishi wa habari kwa kupitia 'mlango wa nyuma' ambao kwa kawaida hutumika tu na wafanyakazi wa Hoteli hiyo.

Taarifa ambazo zimepatikana ni kuwa Mfanyakazi huyo Neema pamoja na Afisa Mkuu wa Usalama wa Hoteli hiyo pamoja na Msaidizi wake upande wa Usalama, tayari wamashafukuzwa kazi kwa 'maagizo' toka mamlaka za juu za nchi yetu.

Inasemekana pia kuwa wafanyakazi hao hawakupewa hata fursa ya kutoa utetezi wao kwa tuhuma hizo kwenye kikao cha Nidhamu kama ilivyo utaratibu wa kawaida wa Hoteli hiyo na ambavyo pia ni kinyume kabisa cha principle kuu ya Natural Justice ya right to be heard.

Hivyo basi kutokana na taarifa hizo za kutimuliwa kwa wafanyakazi hao kujulikana hivi sasa upo umuhimu mkubwa wa wakereketwa wa haki za binadamu,viongozi wanaounda muungano wa Ukawa na wananchi wengine kwa ujumla wao kulifuatilia kwa karibu suala hilo na kuhakikisha kuwa uonevu huo uliofanywa na serikali hii ya Sisiem dhidi ya wafanyakazi hao unakomeshwa na wafanyakazi hao warejeshwe kazini.
 CHANZO : UDAKU SPECIALLY

Comments

Popular posts from this blog