Neymar afungiwa mechi nne na bonge la faini
Nyota wa Brazil na klabu ya Barcelona Neymar hatocheza tena michuano ya Copa America inayoendelea huko Chile baada ya kufungiwa kucheza mechi nne kutokana na kitendo chake cha utovu wa nidhamu alichokifanya wakati Brazi ikicheza dhidi ya Colombia mchezo ambao ulimalizika kwa Brazil kufungwa kwa goli 1-0. Nahodha huyo wa Brazil alioneshwa kadi nyekundu baada ya filimbi ya mwisho ya mwamuzi kupulizwa kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la Santiago Jumatano iliyopita. Neymar alimpiga na mpira mgongoni kwa makusudi mchezaji Pablo Armero wa Colombia mara baada ya mwamuzi kupuliza filimbi ya mwisho kumaliza mchezo huo. Mshikemshike baada ya Neymar kuzua tafran kwa kupiga mpira ulio ‘mbabua’ mgongoni mchezaji wa Colombia Awali alifungiwa kucheza mechi moja, lakini baadae shirikisho la soka la Amerika ya Kusini (South America Football Confederation) liliongeza kifungo na faini ya dola 10,000 za Kimarekani baada ya Neymar kugundulika kuwa alimtolea maneno machafu m