ZITTO KABWE ALIVYOVULIWA UBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI
Mnadhimu Mkuu Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, akitoa tamko la kumvua uanachama Zitto Zuberi Kabwe leo. Waandishi wa habari wakifuatilia tukio hilo. Lissu akitoa ufafanuzi baada ya kuulizwa maswali na wanahabari. Katibu Mkuu wa Chadema Willbroad Slaa (kulia) akifuatilia mkutano huo wa kumvua uanachama Zitto Kabwe.MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zuberi Zitto Kabwe, amevuliwa uanachama wake mchana huu katika ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jijini Dar es Salaam katika hatua iliyotangazwa na mnadhimu mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu, baada ya mbunge huyo kushindwa kesi iliyokuwa amefungua katika Mahakama Kuu ya Tanzania. Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi hizo, Lissu alisema Zitto amefutwa uanachama kwa mujibu wa taratibu na sheria ya chama isemayo kwamba endapo mwanachama atapata tatizo lolote binafsi ama la kichama, malalamiko yote yatasuluhishwa ndani ya chama na si mahakamani. “Hivyo, kwa mujibu