Posts

YAYA TOURE NDIYO MBABE WA SOKA AFRIKA KWA MARA YA NNE

Image
Yaya Toure kiungo wa timu ya Manchester City Yaya Toure amekuwa mchezaji wa kwanza kutajwa na shirikisho la soka barani Afrika kuwa mchezaji bora wa mwaka kwa mwaka wanne mfululizo. Toure ana umri wa miaka 31,aliteuliwa baada ya kucheza kwa kujitoa na kuleta ushindi katika Premier League na League Cup, na pia alijitoa kuisaidia Ivory Coast kuingia katika kombe la mataifa ya Africa yatakayo fanyika baadaye mwaka huu. Toure amewapiku mshambuliaji kutoka Gabon, Pierre Emerick Aubameyang na golikipa mnigeria Vicent Enyeama.Toure pia alikwaa tuzo ya FIfa ya Ballon D'Or mwezi wa kumi mwaka wa jana..

Kenge 149 wanaswa Uwanja wa Ndege Dar Wakitoroshwa nje

Image
Jeshi la Polisi la   Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)linamshikilia raia wa Kuwait kwa tuhuma za kukutwa na viumbe hai aina ya Kenge 149 wenye thamani ya Sh 6.3 milioni.   Kamanda wa Polisi wa JNIA, Khamis Suleiman alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Hussain Ahmed Ally Mansour(34), raia wa Kuwait ambaye alikamatwa uwanjani hapo jana  majira ya saa 5 usiku wakati akijiandaa  na safari ya  kuelekea nchini Kuwait  kupitia Dubai  na Shirika la Ndege la Emirates  .   Kamanda  Selemani alisema Mansour alikamatwa na wanyama hao ambao aliwahifadhi  kwenye mifuko midogo midogo ilivyowekwa katika begi kubwa lenye rangi nyeusi.   “Kenge waliwekwa kwenye mifuko midogo midogo 15 na kila mmoja kuna kenge 15 na mifuko mingine walikaa wawili,” alisema kamanda Selemani.   Alisema kati ya Kenge hao, 15 walikufa na walio hai walikuwa 134 ambao  walikuwa wamefichwa kwenye mifuko hiyo.   Seleman alisema wakati wanafanyiwa upekuzi ndipo  walipogundua kuna

Penzi Kinyume na Maumbile Lamtesa Lungi

Image
  Msanii wa filamu za Kibongo, Lungi Maulanga, amesema kuwa mpenzi wake amekuwa akimsaliti kila kukicha huku akihisi kuwa, huenda wanawake anaowafuata huko nje wanampa mapenzi kinyume na maumbile.   Akizungumza Gpl Lungi alisema kuwa siku chache zilizopita alilia sana kutokana na usaliti aliofanyiwa na mpenzi wake aliyemhifadhi kwa jina, akasema aliamua kumsamehe kwa kuwa anampenda.    “Naumia sana na nalia kila ninapokumbuka namna mpenzi wangu anavyonisaliti, sielewi ni kwa nini wakati mimi ni mrembo na nina umbo zuri ambalo kila mwanaume akiniona lazima anitamani.   “Nashangaa mwenzangu anavyochepuka, sijui huko nje anawafuata wale wanaotoa ‘mtandao’?” alihoji Lungi na kuongeza: “Mimi siwezi kumsaliti hata iweje, najua huko nje magonjwa ni mengi.”

PICHA NA VIDEO DIAMOND PLUTNUMZ NA P SQUARE NDIO WALIO FANIKIWA KUWATEKA HISIA MASHABIKI TUZO ZA GloCafAwards‬

Image
Wasanii wa Africa walipata nafasi yakutoa burudani katika tuzo hizo za  GloCafAwards‬    ‪ kama Uhuru Mr lavour Uhuru ,soweto gospel choir na wengineo Lakini Watu Waliguswa na Nyimbo ya diamond mdogo My Number one remix ambayo Plutnmz alionyesha uwezo wakuimba ubeti wa Davido Wote Bila yakufwata Cd Back Play nakufanya vizuri P square walifanikiwa kuwa kosha masbabiki baada ya kuimba nyimbo mbili Test MOney Na Ejajo 

YANGA YACHEZEA KIRUNGU NA KUTUPWA NJE KOMBE LA MAPINDUZI

Image
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar YANGA SC imetupwa nje ya kombe la Mapinduzi 2015 kufuatia kutandikwa bao 1-0 dhidi ya JKU katika mechi ya mwisho ya robo fainali iliyomalizika uwanja wa Amaan usiku huu. Bao pekee la Amour Omar ‘Janja’ lililofungwa katika dakika ya 72 limetosha kuwatumbukiza Wanajeshi hao katika hatua ya nusu fainali. Kipindi cha kwanza timu zote ziliuanza mchezo kwa makani na kupata nafasi kadhaa za kufunga, lakini washambuliaji wa timu zote hawakuwa makini. Yanga walianza kwa kutawala mchezo huo wakipigiana pasi za uhakika kuanzia katikati, lakini hesabu zao hazikuwa nzuri kila walipofika eneo la hatari la wapinzani wao. Dakika ya 24 kipindi cha kwanza, Amiss Tambwe aliendeleza maajabu yake ya kukosa mabao ya wazi katika michuano ya kombe la mapinduzi kwani alipata nafasi nzuri ya kufunga kufuatia mabeki wa JKU kuchanganyana na kipa wao Mohammed Abdallah, lakini Mrundi huyo alipiga mpira nje. Dakika ya 35 kwa mara nyingine tena Tambwe
Image
Baada ya Kupiga Show ya Nguvu Nigeria usiku wa leo, Diamond kasema haamini Macho yake 1/09/2015   habari za kitaifa   Staa Afrika Mashariki, Nasibu Abdul ‘Diamond’, amefunguka kwamba haamini kama kweli amepata nafasi ya kutumbuiza kwenye sherehe za utoaji tuzo za wanamichezo bora zilizoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ambazo zimefanyika usiku wa kuamkia leo jijini, Lagos, Nigeria.   Akizungumza na Mpekuzi, Diamond amesema amefurahi kupata nafasi ya pekee ambayo mara nyingi hutolewa kwa wasanii wakubwa Marekani na kuamini kwamba muziki wa Tanzania unathaminika kila kona.   “Nimefurahi maana hii inaonyesha jinsi gani muziki wetu umekuwa hadi kufikia Afrika kuwa moja ya kionjo hasa kwenye tamasha kubwa kama hilo, kiukweli sikuwahi kufikiria hapo mwanzo,” alisema Diamond.

BREAKING NEWS: MASIKINI WALE WATOTO MAPACHA WA KIKE WALIOZALIWA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MARA WALIOUNGANA KIFUA WAMEFARIKI DUNIA,MWANZA

Image
Watoto mapacha wa kike waliozaliwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara iliyopo mjini Musoma wakiwa wameungana sehemu ya kifua na tumbo wamefariki dunia jana majira ya saa 9.10 alasiri wakiwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza kabla ya kufanyiwa upasuaji. Watoto hao pacha walizaliwa januari 4 mwaka huu na mama mmoja mkazi wa manispaa ya Musoma Helena Paulo wakiwa na uzito wa kilo 4.6 na kisha kusafirishwa hadi katika hospitali ya rufaa Bugando kwa ajili ya uchunguzi zaidi ikiwa ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kufanyiwa upasuaji wa kuwatenganisha. Dk. Shukuru Kibwana ambaye ni daktari katika wodi ya watoto ya hospitali ya rufaa Bugando, amesema timu ya madaktari wa upasuaji na wataalamu wengine wamefanya kila lililowezekana kuokoa maisha ya pacha hao walioungana lakini haikuwezekana na kuongeza kuwa kabla ya upasuaji, mapacha hao walitakiwa kupitia tomografia ( CT ) na kufanya kipimo cha ultra sound ili kujua kama watoto hao wameungana

BREAKING NEWZZ! YANGA YAMTOSA KASEJA

Image
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga Jerry Murro akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Unguja katika kambi ya timu yao iliyopo hoteli ya Zanzibar Ocean View KLABU ya Yanga imetengaza rasmi kuachana na mlinda mlango wake Juma Kaseja kwa madai kuwa Tanzania One huyo wa zamani hajaonekana klabuni kwa majuma matatu. Mkuu wa Idara ya habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro amekutana na waandishi wa habari leo mjini Zanzibar na kueleza kuwa kitendo hicho cha Kaseja kimemfanya avunje mwenyewe mkataba wake na klabu hiyo yenye maskani yake makutano ya Twiga na Jangwani , Kariakoo, Dar es salaam. Katika hatua nyingine, Yanga imekanusha madai ya kushindwa kumlipa Kaseja milioni 20 ambayo ni sehemu ya fedha za usajili wake wakidai walishamlipa kabla ya kupeleka barua ya madai. Taarifa rasmi inakujia

Forget About Huddah and Zari from Uganda, This is Vera Sidika, Hottest Kenyan Socialite...see her Hottest Photos

Image

MAHABA: MWANAUME NDIYE MWENYE NAFASI YA KULINDA PENDO!!!

Image
HABARI wadau wa safu yetu, tupo tena pamoja katika kujuzana jinsi gani maisha ya kimapenzi yalivyo. Leo nitakuwa tofauti kidogo na mara zote ambazo nimekuwa nikiwasiliana nanyi, kwani mara nyingi nimekuwa nikizungumzia kuhusu nafasi ya mwanamke, kuwa ili iwe hivi, basi afanye hivi na kadhalika. Maandiko mengi yamekuwa ni kama ya kuonyesha kuwa mwanamke ndiye mwenye dhamana kubwa ya kuamua juu ya penzi au ndoa aliyomo. Ingawa ni kweli kuwa kuna umuhimu mkubwa wa mama kuwa mshirika muhimu katika ndoa, lakini amini usiamini, mwanaume ndiye hasa mwenye kushika turufu ya penzi linalohusika.  Na ninasema hivi hasa kutokana na ukweli ambao nafsi zote mbili zinakubaliana kuwa mwanaume ndiye kichwa cha nyumba. Usemi huu unaweza kuonekana ni mwepesi kama utaangaliwa kwa upande mmoja tu, ambao kimsingi unabeba maana ya uwajibikaji juu ya majukumu ya kuilea na kuilinda familia. TUPE MAONI YAKO NDUGU MDAU WETU KUHUSU HILI NA USISITE KUUNGANA NASI KUPITIA UKURASA WETU WA

Ni kweli Matonya aliwekewa madawa kwenye pombe? Alewa na kukutwa vichakani hajitambui

Image
Hitmaker wa ‘Anita’ Matonya aliwekewa vitu vinavyohisiwa kuwa ni madawa kwenye pombe aliyokuwa akinywa, kwa mujibu wa Rich One ambaye ni jirani yake. Picha ya Matonya inayomuonesha akiwa amelala vichakani hajitambui ilisambaa wiki hii kwenye mitandao ya kijamii kiasi cha watu kuzusha kuwa amefariki dunia.   Rich alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM  kuwa tangu afahamiane na Matonya hajawahi kumuona amekunywa pombe hadi kufikia hatua ya kupoteza.   “Nina imani kuwa washkaji waliokuwa naye walimwekea,” alisema rapper huyo. Bado Matonya hajaweza kuzungumzia skendo hiyo

Picha za Lulu Michael Zatikisa Mitandao ya Kijmanii

Image
Staa wa Bongo Movies, Elizabeth Michael Kimemeta 'Lulu' akiwa katika mapozi tofauti baada ya kuachia picha hizi kupitia account yake ya Instagram siku ya jana na kupelekea kutikisa katika mitandao ya kijamii huku wapenzi wake wakimuita Kim Kardashian wa bongo.         TUPE MAONI YAKO KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.

BILL GATES ANYWA MAJI YA KINYESI

Image
Bill Gates akinywa maji yaliyotokana na kinyesi. Mmiliki wa kampuni ya Microsoft Bill Gates amekunywa maji yaliotengenezwa kutokana na kinyesi cha binaadamu kama maonyesho ya teknolojia mpya itakayoweza kutoa maji safi katika mataifa yanayoendelea. Mwanzilishi huyo wa Microsoft amesema kuwa ataisambaza mitambo ya teknolojia hiyo mpya kote duniani baada ya kuifanyia majaribio mwishoni mwa mwaka huu.Teknolojia hiyo imeungwa mkono na shirika la WaterAid ambalo limesema kuwa itasaidia sana katika maeneo ya miji. Kulingana na shirika hilo la hisani takriban watu millioni 748 hawana maji safi ya kunywa.katika kanda ya video iliyowekwa katika blogu yake,Bwana Bill Gates alishuhudia kinyesi cha Binaadamu kikiingizwa katika mtambo huo kabla ya kunywa maji yaliokuwa yakitoka kutoka kwa kikombe. ''Maji hayo ni mazuri sana ikilinganishwa na maji yoyote yale niliokunywa,na baada ya kusomea teknolojia hii nitayanywa kila siku.Maji haya ni salama kabisa'',aliand

Nisha na Mpenzi Wake Wamwagana

Image
Msanii wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’  na mpenzi wake aliyejulikana kwa jina la Farhad wanadaiwa kumwagana baada ya kuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu.   Chanzo kimoja kimedai  kwamba Nisha na mpenzi wake huyo ambaye walikuwa na mipango ya kuoana mwaka jana lakini ndoa ikayeyuka waliachana kutokana na sababu zisizojulikana na sasa kila mmoja  yupo bize na maisha yake. Baada ya kuzinyaka habari hizo mwandishi wetu alimtafuta Nisha ili kuzungumzia habari hizo ambapo alikiri kwamba ni kweli wamemwagana.   “Sababu za kuachana siwezi kuziweka wazi kwa sasa, niko kikazi zaidi mambo ya mapenzi nimeyaweka pembeni nataka nitimize malengo yangu ambayo hayakutimia mwaka jana,” alisema Nisha.

Mwanamke huyu afunga ndoa na Paka

Image
Dunia haishi maajabu na maajabu yamekuwa yakitokea siku hadi siku na yanatokea karibu kila mahali. Mwanamke mmoja huko nchini Marekani aitwaye Barbarella Buchner ametoa kali ya mwaka 2015 baada ya kufunga ndoa na paka wake wawili. Mwanamke huyo alipokuwa anatoa ufafanuzi juu ya tukio hilo amesema kuwa hakuwahi kuwa na wazo la kuolewa na mpenzi yoyote yule wa kiume kati ya wapenzi alio nao na hajawahi kuwa na wazo kwamba atakuja kuwa mke wa mtu au kiumbe yoyote yule.   Barbarella mwenye umri wa miaka 48 ambaye kazi yake ni ubunifu wa tovuti kwenye mtandao wa internet ameongeza kuwa ana furaha kubwa baada ya kuolewa na paka wake wawili ambao ameolewa nao. Mwanamke huyo alinukuliwa akisema kuwa “Kuna baadhi ya wanawake wamepangiwa kufanya usafi kwa ajili ya waume zao na wameridhia kufanya hivyo , kwangu ni tofauti“ – Barbarella. Ameongeza kuwa haoni shida kuwatumikia paka wake ambao wana majina ya Lugosi na Spider na siku zote atahakikisha wanaish

MWIGULU NCHEMBA AMETIMIZA MIAKA 40,ATUMIA SIKU YAKE KUCHANGIA DAMU,KUSALIMIA WATOTO YATIMA NA KUJULIA HALI WODI YA AKINAMAMA MWANANYAMALA

Image
Mh:Mwigulu Nchemba hii leo ametimiza miaka 40 ya Kuzaliwa kwake. Mwigulu Nchemba akiwasili Hospitali ya Mwananyamala kwaajili ya Kutembelea na kusalimia Wodi ya wazazi kama sehemu yake ya Kusherekea siku ya Kuzaliwa(Miaka 40). Mwigulu Nchemba akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Hospitali ya Mwananyamala hii leo tar.07.01.2015. Mh:Mwigulu Nchemba akimsalimia mtoto aliyepatwa na tatizo la kuungua moto. Mh:Mwigulu akisikiliza kwa makini mahitaji ya wodi ya akinamama kutoka kwa Mganga mkuu Hospitali ya Mwananyamala. Mwigulu Nchemba akisaidia kubeba mtoto wakati alipotembelea \hospitali ya Mwananyamala hii leo kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwake. Mwigulu Nchemba akizungumza na Bi.Saida ambaye ni Mwenyekiti wa kituo cha watoto yatima cha CHAWAKAMA. Mke wa Mh:Mwigulu Nchemba Bi.Neema Ngure akisaidia kubeba mtoto Yatima kwenye kituo cha watoto yatima Sinza hii leo. Baadhi ya watoto yatima wakimsikiliza Mwigulu Nchemba. Mwigulu Nchemba akiwapatia watoto yatima zawadi kwa yeye kuti