Baada ya Kupiga Show ya Nguvu Nigeria usiku wa leo, Diamond kasema haamini Macho yake


Staa Afrika Mashariki, Nasibu Abdul ‘Diamond’, amefunguka kwamba haamini kama kweli amepata nafasi ya kutumbuiza kwenye sherehe za utoaji tuzo za wanamichezo bora zilizoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ambazo zimefanyika usiku wa kuamkia leo jijini, Lagos, Nigeria.
 
Akizungumza na Mpekuzi, Diamond amesema amefurahi kupata nafasi ya pekee ambayo mara nyingi hutolewa kwa wasanii wakubwa Marekani na kuamini kwamba muziki wa Tanzania unathaminika kila kona.
 
“Nimefurahi maana hii inaonyesha jinsi gani muziki wetu umekuwa hadi kufikia Afrika kuwa moja ya kionjo hasa kwenye tamasha kubwa kama hilo, kiukweli sikuwahi kufikiria hapo mwanzo,” alisema Diamond.

Comments

Popular posts from this blog