Posts

Ajifungua pacha wa kike walioungana kifua, tumbo

Image
Musoma. Mwanamke mmoja mkazi wa Kata ya Buhare, Manispaa ya Musoma mkoani Mara, Helena Paulo (20), amejifungua watoto pacha wa kike walioungana eneo la kifuani hadi tumboni wakiwa na uzito wa kilo 4.6 kwa pamoja. Tukio hilo la ajabu katika Mji wa Musoma na mkoa kwa jumla, liliwavutia hisia za wananchi hali iliyosababisha msongamano katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa madhumuni ya kutaka kushuhudia. Akizungumza katika wodi ya wazazi hospitalini hapo, muuguzi wa zamu, Naabu Geraruma alisema mwanamke huyo alijifungua juzi saa saba usiku kwa njia ya upasuaji. Geraruma alisema tukio hilo ni la kwanza katika hospitali hiyo na hali ya afya ya mzazi huyo na watoto inaendelea vizuri na muda wowote atahamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mwanza. Kwa upande wake, Mganga wa Idara ya Magonjwa ya Wanawake, Dk Simon Kamuli alisema baada ya jitihada za kuhakikisha mwanamke huyo anajifungua salama kukamilika, kinachofuatia ni kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando...

JB AWEKA WAZI JINSI ANAVYOMPENDA MKE WAKE NA KUITHAMINI NDOA YAKE

Image
Mwigizaji na mwogozaji wa filamu za hapa bongo, Jacob Stephen ‘JB’ amefunguka ya moyoni juu ya upendo wake kwa mke wake na kuendelea kudumisha ndoa yao. JB tofauti na mastaa wengi wa hapa bongo, amemuweka na kumwambia waziwazi mke wake wa ndoa maneno ya upendo ambayo huwafanya mashabiki wake wote kkujua na kumtambua shemeji yao au wifi yao. JB leo hii ameweka picha hiyo mtandaoni akiwa na mke wake na kuandika maneno haya; “Mke wangu,rafiki yangu, nampenda sanaa. Siku kama ya leo tuliingia kanisani tukatoa kiapo cha maisha,hakuna kilicho badilika wala kitakacho badilika mpaka kifo kitakapo tutenganisha. NAKUPENDA SANA MKEWANGU,Mungu azidi kuibariki ndoa yetu”. JB alimaliza. Tunakupongeza JB kwakuendelea kuheshimu na kuitunza ndoa yako, tunawatakia baraka katika maisha yenu.

Mke wa Mtu Asaula Nguo Akimfuta Jasho Bi. Harusi

Image
Mwanamke mmoja ambaye inadaiwa ni mke wa mtu aliyefahamika kwa jina la Mishi Choggo ametoa kali ya mwaka baada ya kusaula kisha kutumia gauni lake kumfutia jasho bi. harusi. Bi’mkubwa huyo alifanya kioja hicho Jumamosi iliyopita katika Ukumbi wa Rose Garden maeneo ya Mafinga mkoani Morogoro katika harusi ya Rose Raphael na Edward Sebastian ambao walikuwa wakibariki ndoa.   Wakati sherehe ikiwa imepamba moto na waalikwa mbalimbali wakianza kutoa zawadi, mama huyo alimfuata DJ na kuomba awekewe wimbo wa taarabu, akaanza kucheza kwa madaha huku akienda kutunza.    Mama huyo alipomkaribia bibi harusi, alisaula gauni lake refu na kulitumia kumfuta jasho bi. harusi baada ya kukosa hanjifu.   Kitendo hicho kiliwafanya baadhi ya watu wanaojiheshimu kuinamisha vichwa chini kwa aibu huku wale micharuko wenzake wakishangilia. TUPE MAONI YAKO KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI...

LAIVU BILA CHENGA WEMA SEPETU ANASWA NYUMA YA UKUMBI WA MATEI LOUNGE DODOMA AKIWA NA MENEJA WA .....

Image
Siku ya mkesha wa mwaka mpya kulifanyika Bonge la Party ndani ya Ukumbi wa Matei lounge ambapo team nzuma ya Endeless Fame walikinukisha pande hizo huku kukiwa na maelfu ya wakazi wa Dodoma waliohudhuria Party hiyo.. Katika Party hiyo wema Sepetu alipoingika katika ukumbi wa Matei Lounge alikuwa yuko poa yani namaanisha alikuwa hajagida kilevi chochote...Ila baada ya muda wa kama Nusu saa Madam Wema alionekana kuwa karibu na Meneja wa Boss Ngasa Tz ambaye anajulikana kwa jina la Meneja Erick Mshana ambapo madam ndio alikuwa anapenda kumwita kila saa.. Paparazi wetu bila hiyana akaendelea kwenda na Muvi..wenyewe wakaitana kimya kimya kwa pembeni yani nyuma ya back stage kilichoendelea huko hakuna aliyeyekijua ila waliingia ndani ya gari mara gafla madam akaibuka huku akiwa amechangamka kwa sana namna ya kupepesuka.... Wema akaanza uchizi wake sasa wakukata mauno back stage akiwa hana hata mshipa wa Aibu... baada ya hapo akapanda stejini Kiukweli madam alipiga bong...

NANI ZAIDI KWA UZURI KATI YA WEMA SEPETU NA ZARI THE LADY BOSS ?

Image
Kwenye Mitandao ya Jamii Hasa Instagram kwa Sasa zimeibuka Team Mbili Kubwa zinazoshinda huko kwa Kupeana Vijembe vya Hapa na Pale Kuhusu Wema Sepetu na Mrembo Zari The Lady Boss wa Uganda, Ushandani huo wa Team Zari na Team Wema Umekuja Baada ya Mwanamuziki Diamond Kuwa na Mahusiano ya Kimapenzi na Wote hao wawili kwa Muda tofauti ambapo kwa sasa Diamond Ameweka Wazi Kuwa anatoka na Zari .. Ubishi mmoja wapo ni kuwa nani ni mzuri wa Umbo na Sura kati ya wema Spetu na Zari , Nasisi hatuna hiyana tumeona tuwabambanishe Hapa tuone nani atapata kura nyingi ... Haya Nani Mrembo zaidi kati ya Wema Sepetu na Zari The Lady Boss?

MIMI SI MENEJA TENA WA ROSE MUHANDO-MSAMA

Image
HATIMAYE Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, Alex Msama, ameibuka na kutamka yeye si Meneja wa malkia wa nyimbo za injili nchini, Rose Muhando akisema amekuwa akishirikiana naye katika mazingira ya kawaida kama ilivyo kwa waimbaji wengine. Kwa mujibu wa taarifa ya Msama kwa vyombo vya habari jana, yeye akiwa mlezi wa waimbaji wote wa muziki wa Injili, amekuwa akishirikana nao kwa karibu kutokanana nafasi yake katika huduma hiyo ya uimbaji kwa kipindi cha miaka 15. Msama, mtu aliyechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya muziki wa injili nchini kutokana na kuandaa matukio ya muziki huo kama Tamasha la Pasaka, uzinduzi wa albamu na Tamasha la Krismas, alisema ameamua kutoa tamko hilo kutokana na malalamiko ya muda mrefu ambayo amekuwa akipata juu ya Rose. "Nimekuwa nikipokea malalamiko mengi ikiwemo kutoka kwa viongozi wa kiroho wakiwemo wachungaji, kwamba pengine nimekuwa nikimzua Rose (Muhando) katika mtamasha wanayom...

Aunt Ezekiel: Mume wangu Hajui kama nina Mimba

Image
Msanii wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel ‘Mama Kijacho’ amefunguka kuwa, licha ya ujauzito wake kuwa mkubwa, mume wake Sunday Demonte hana taarifa yoyote juu ya kitumbo hicho.   Akizungumza na mwandishi wetu, Aunt alisema maneno hayo yanaweza kuwashangaza watu lakini ndiyo ukweli wenyewe.   Alidai kuwa yeye na mume wake huyo hawajaachana na hajapewa talaka kama watu wanavyodai lakini hajui kwamba ni mama mtarajiwa na hata akijua hawezi kumuacha.   “ Kiukweli mume wangu hajui kuwa nina ujauzito na hata akijua wala hawezi kuniacha, ananipenda sana. Sijaachana naye na wala sijapewa talaka, hayo yanayosemwa ni umbeya tu, ” alidai Aunt.

HABARI YA MJINI: WAKATI DIAMOND AKIMTESA NA ZALI, WEMA AJIBU MAPIGO!

Image
Habari ya mjini!  Gumzo katika ulimwengu wa mastaa Bongo ni kitendo cha mkali wa muziki wa Kizazi Kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuendelea kujiachia na staa wa mrembo mwenye maskani yake nchini Uganda na Afrika Kusini ‘Sauz’, msanii Zarinah Hassan ‘Zari’ au ‘The Boss Lady’  huku  aliyekuwa ‘kiburudisho’ wa jamaa huyo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ akijibu mapigo kwa kumnasa mwigizaji Joseph Van Vicker wa Ghana, Ijumaa lina sarakasi nzima.  Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye akimbusu Van Vicker kimahaba.   WEMA ATIMKIA GHANA Wakati Diamond akitimkia Marekani kwenda kutumbuiza kwenye sherehe za 53 za Uhuru wa Tanganyika kwa Wabongo waishio nchini humo (Diaspora), Desemba 9, mwaka  huu , Wema yeye alitimkia kwenye Mji Mkuu wa Ghana jijini Accra kuungana na Van Vicker kwa ajili ya ‘projekti’ kama ilivyokuwa kwa Diamond na Zari.  Habari za uhakika zilizothibitishwa na Wema mwenyewe zilieleza kwamba yupo nchi...

PENNY: NATAMANI MTOTO, SINA WA KUZAA NAYE

Image
Stori: Imelda Mtema Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ Penniel Mwingilwa amesema sasa anatamani kuzaa lakini tatizo lipo kwa mwanaume wa kuzaa naye. Penniel Mwingilwa. Penny alitoa tamko hilo baada ya Diamond kunukuliwa jana (Alhamisi) na gazeti dada la hili, Amani kuwa, alimpa mimba mara mbili binti huyo lakini zikayeyuka katika mazingira ya kutatanisha. Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni Penny alisema, sasa hivi anapomuona mtoto anachanganyikiwa na kujikuta akitamani naye kuitwa mama hivyo akimpata mwanaume sahihi wa kutimiza ndoto yake hiyo hatafanya ajizi. “ Kiukweli sasa ndiyo ule wakati wa kuzaa, natamani sana mtoto lakini sasa wa kuzaa naye yuko wapi? Hapo ndiyo tatizo maana siyo kuzaa na mtu ili mradi mtoto awe na baba,” alisema Penny .

HIVI NDIVYO MADAHA ALIVYOFUNGUKA KUHUSU SKENDO YA KUJIUZA, KUTOKUWA NA PA’ KUISHI

Image
Baby Joseph Madaha ndiye ambaye wiki hii yuko hapa kujibu maswali 10 ambayo mwandishi wetu Gladness Mallya alimuuliza. Ilikuwa hivi; Staa Baby Joseph Madaha. Ijumaa: Umekuwa ukitajwa kuwa wewe ni msanii wa kike unayeongoza kwa kubadilisha mabwana kila kukicha, hili likoje? Baby Madaha: Ukweli hiyo huwa inatokea tu na huwa sipendi kusumbuliwa na mwanaume, nikiona ananizingua nammwaga. Hata hivyo, kwa sasa nimeamua kutulia kwanza, nafanya kazi, mapenzi pembeni. Ijumaa: Unadhani kwa nini umekuwa ukiingia kwenye uhusiano kisha kutoswa, ni umachepele wako au kitu gani? Baby Madaha: Mimi wala siyo machepele kama watu wanavyonifikiria na kiukweli huwa nawaacha mimi na siyo wao kuniacha. Ijumaa: Mpaka sasa umeshakuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume wangapi? Baby Madaha: Wanaume niliotembea nao ni siri yangu kwa sababu nikitaja idadi hapa watu watalia na wewe mwandishi unaweza kuzimia. Ijumaa: Kuna tetesi kwamba wewe na msanii mwenzako Isabela Mpanda huwa mnaishi kama ...

Mwana wa Raila Odinga afariki

Image
Fidel Castro Fidel Odinga mwana wa aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga amepatikana akiwa amefariki nyumbani kwake huko Karen. Maafisa wa polisi tayari wameanzisha uchunguzi kuhusiana na kifo cha mfanyibiashara huyo ambaye pia amekuwa akionekana katika ulingo wa kisiasa. Maafisa wa Polisi wanasema kuwa uchunguzi wa mapema umeonyesha kuwa Fidel alikuwa nje usiku wa jumamosi na alirudi mapema jumapili. Aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga. Haijulikani ni nini kilichosababisha kifo chake. Kundi la wabunge pamoja na maseneta liliwasili katika nyumba ya Raila baada ya kupata habari hizo. Maafisa wanaosimamia kesi hiyo wanasema kuwa wanataka kujua ni wapi Fidel alikuwa usiku wa jumamosi na alikuwa na nani.

DIAMOND ATEULIWA KUTUMBUIZA TUZO ZA MWANASOKA BORA CAF

Image
Msani Nasib Abdul ‘Diamond’ amechaguliwa kuwa mmoja wa wasanii watakaotumbuiza kwenye hafla ya utoaji tuzo za mwanasoka bora Afrika 2014. Diamond atatumbuiza katika tuzo hizo ambazo wachezaji 25 nyota barani Afrika wamechaguliwa kugombea tuzo hizo. Hafla hiyo itafanyika Januari 8, 2015 jijini Lagosi Nigeria.  Mwanasoka Bora, Yaya Toure raia wa Ivory anayeitumikia Manchester City ya England ni kati ya watakaowania nafasi hiyo.  Wanaowania tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika: 1.      Ahmed Musa                              (Nigeria, CSKA Moscow) 2.      Asamoah Gyan                           (Ghana, Al Ain) 3.      Dame N’doye      ...

DEREVA TEKSI AFUMANIWA, AUAWA KWA KUCHOMWA KISU KIFUANI

Image
DEREVA teksi Hamis Seleman (18), mkazi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam, amekufa baada ya kuchomwa kisu kifuani na Ali Kimodo, aliyemfumania akiwa na mpenzi wake. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Mary Nzuki alisema tukio hilo lilitokea usiku wa saa 9:00 wa kuamkia mwaka mpya, katika eneo la Vingunguti mtaa wa Magenge, ambapo Seleman alifumaniwa na msichana mmoja (jina tunalihifadhi), mwenye umri wa miaka 15, mkazi wa Tabata. Nzuki alisema kuwa baada ya tukio hilo kutokea, Kimodo pamoja na binti huyo walitoroka, hivyo polisi inaendelea na upelelezi kwa ajili ya kuwapata watu hao. Aliongeza kuwa katika maeneo mengine ya mkoa huo, hali ilikuwa shwari katika sherehe hizo za sikukuu ya Mwaka Mpya. Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kihenya Kihenya alisema hali ilikuwa shwari katika eneo lake, kuanzia Krismasi na Mwaka Mpya. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillus Wambura alisema katika eneo lake, pia hakukuwa na tukio lolote kubwa la u...

PICHA ZA BAADHI YA WAKE WA MFALME MSWATI>>EBWANA JAMAA ANAJUA KUCHAGUA

Image
Meet some of KING MSWATI's wives, Very Hot, the Guy must be lucky