Posts

Image
JOKATE KIDOTI NA MILLARD AYO WANASWA LIVE KATIKA POZI TATA! 10:02 AM     No comments Jokate Kidoti na Millard Ayo wa Clouds FM!Hakika hata siku moja huwezi kuuficha moto, kwani moshi lazima utakuumbua tu. Baada ya kuumizwa na aliyekuwa mpenzi wake Millard Ayo kwa madai ya kumfumania live Mwanza, Millard aliamua kukaa single kwa muda mrefu na kutokuwa na wazo la kupenda tena! Ila hii picha akiwa na Jokate Kidoti "Jojo" imekua gumzo mtandaoni kuwa eti ni wanapika na kupakua! Stay tuned kama ipo ipo tu mdau!

SHOO YA DIAMOND DAR LIVE YAACHA HISTORIA

Image
Mwanamuziki Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' akipozi katika picha na mashabiki baada ya shoo ya nguvu Dar Live. Diamond akiwa na tuzo pamoja na cheti baada ya kuibuka mshindi wa shindano la Ijumaa Sexiest Bachelor. Diamond Platnumz akifanya makamuzi ya hatari Dar Live. Diamond akifanya yake stejini. Diamond akicheza na dansa wake.

SUPERSTAR WA BONGO MOVIE AFUMANIWA NA MKE WA MTU NA HIKI NDICHO ALICHOFANYIWA

Image
Wakati wengine wakisheherekea sikukuu ya Christmass duniani kote ikiwa ni kumbukumbu kwa wakristo wote kuzaliwa kwa Mwokozi wao "YESU" Wengine siku hiyo wanaifanya kuwa siku ya starehe na kufanya mambo kinyume na maana ya siku yenyewe. Msanii wa filamu za bongo maarufu kwa jina la Pancho Mwamba, anadaiwa kufanyiwa mbaya baada ya fumanizi siku ya Xmass. Msanii huyo inasemekana amefumaniwa na mke ambaye si wake siku ya Christmass maeneo ya Kinondoni jijini hapa.  Patcho Mwamba Lukusa ni muimbaji, Mtunzi, Composer, Music Arranger, Mchezaji, Mchekeshaji na ni muigizaji wa cinema. Patcho amejitokeza kucheza vizuri katika tasmia nzima ya sinema huku ajijizolea umaarufu kama mwanamuziki huyu toka kundi la FM Academia wana Ngwasuma ameweza kujizolea sifa kem kem toka kwa mashabiki wa Dollywood

MAZISHI YA WATU 15 KABURI MOJA HUKO KIGOMA! NI WALE WALIOPATA AJALI YA MELI!

Image
Miili 15 ya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambao walifariki katika ajali ya meli kwenye Mkoa wa Kalemie nchini humo ilipatikana Kigoma na mazishi yamefanyika ambapo kwa upande wa Serikali Congo kulikuwa na muwakilishi ambaye ni Balozi mdogo Congo, Riki Molema.  Hizi ni baadhi ya picha wakati wa mazishi ya watu hao.  Naibu Balozi Mdogo wa ubalozi wa DRC mkoani Kigoma Riki Molema akizungumza na wananchi wa kijiji cha kalilani wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma wakati wa mazishi ya watu hao. Mwenyekiti wa kijiji cha Kalilani, Songoro Saidi akiweka mchanga akiweka mchanga kwenye kaburi la raia wa 15 Congo waliozikwa Kigoma.  Balozi mdogo wa ubalozi wa DRC, Riki Molema akiweka mchanga kwenye kaburi hilo.

ALICHO POST ZITTO KABWE, BAADA YA RAIS KUMVUA MADARAKA WAZIRI ANNA TIBAIJUKA

Image
Nimemsikiliza Mhe Rais. Ninachoweza kusema ni kwamba maazimio yale hayakuwa ya  Zitto Kabwe , PAC, CAG au PCCB. Yalikuwa ni maamuzi ya Bunge zima. Bunge la vyama vyote kikiwamo chama cha Rais Kikwete yaani CCM. Sisi kama Bunge tulitoa maazimio yale kwa maridhiano, uzalendo na bila kutaka kumuonea mtu yeyote. Suala hili sasa naliacha kwa wananchi. Bunge limefanya kazi yake na Serikali ambayo ndiyo tulikuwa tunasubiri maamuzi yake imeamua hivyo. Wananchi wataamua wenyewe. NAWEWE TOA MAONI YAKO HAPA CHINI USIKIKE !

HAYA NDIYO MADHARA YA KUKU WA KISASA

Image
Kwa muda mrefu watu wengi amekuwa wakiwafakamia kuku hawa pasipo kujua madhara yao.  Je umewahi kujiuliza na kutafakari madhara ya ndege hawa watamu??? Yatambue madhara yake hapa.  Kuku hawa tofauti na kuku wa kienyeji hukua kwa haraka sana kutokana na vyakula vya kemikali nyingi walishwazo.ndani ya miezi miwili kuku hawa huwa tayari kwa kitoweo tangu watotolewapo.tena hutotolewa kwa mashine.  wakati kuku wa kienyenj huchukua hadi miezi nane kuwa tayari kwa kitoweo,na hutotolewa na mama zao. MADHARA YAKE NI HAYA.   1.Kwa watoto kukua kwa haraka na kupevuka kimaumbile mapema mno.  2.Kwa Wakubwa;wanaume kunenepa sana na kuota matiti kama wanawake. 3.Kwa wanawake;kuota ndevu kama wanaume,kuwa na vipara kicchwani,na miili legelege kwa wote.  JE,WAJUA NA NINI MAONI YAKO?

WOLPER ADAI HAKUWAHI KUVAA NGUO FUPI .....LAKINI HII YA LEO NI BAHATI MBAYA TU

Image
Mrembo na mwigizaji wa kike wa filamu hapa nchini, Jackline Masawe “Wolper” amekuwa akisifiwa kwa kuvaa nguo za heshima ukilinganisha na mavazi wanayovaa baadhi ya mastaa wengine hapa Bongo wakiwa mitaani au kwenye burudani Sasa jana mrembo huyu akatupia picha hizi akiwa beach amevalia ka-pensi keupe huku juu amavalia brauzi nyeusi na kofia nyeupe kichwanina huku akicheza na ka-"DOG" ..Kisha akawaandikia hivi mashabiki wake; "Sikuwahi kuvaa nguo fupi wakati naenda kanisani au sokoni nawakati wote mmekua mkinisifia navaa nguo za heshima sasa mkitaka niiheshm paka beach mtakua mmetishaa saana wana ndugu mnaojua sheria humu insta so mnataka beach nivae kanic au komeni pita like utaki pita". Mdau umeionaje hii!!!!

NI VITA KARIAKOO,RISASI ZA ZARINDIMA NJENJE,MAGARI SOMA HAPA KUJUA

Image
Vurugu kubwa imetokea mda huu maeneo ya kariakoo Jijini Dar Es Salaam na kupelekea Jeshi la polisi kurusha Risasi hovyo ili kuwatawanya Wamachinga walioanzisha Fujo hizo huku barabara za kuingia na kutoka kariakoo zikiwa zimefungwa kutokana na Matairi ya Gari yaliyochomwa moto barabarani.  Kwa Mujibu wa Shudhuda wetu aliyoko Maeneo hayo ya Kaliakoo anasema Chanzo cha vurugu hizo zinatokana na Wafanyabiashara Wadogodogo Maarufu Wamachinga kudai mfanya Biashara mwenzao kuuliwa na Mgambo wa jiji. Shuhuda huyo alizidi kusema Mfanya Biashara huyo aliuliwa na Mgambo kwa kupigwa kipigo kikali na kumpelekea mauti, Wafanyabiashara hao wanadai hali hiyo ni ishara ya kuchoshwa na Manyanyaso hayo wanayofanyiwa na Mgambo hao na kuanzisha hali hiyo ya Fujo ambayo wanadai ni njia ya kupeleka ujumbe kwa Serikali

OKWI HATI HATI KUIVAA KAGERA SUGAR FC IJUMAA

Image
Mshambuliaji anayetajwa kuwa ‘mtukutu’ wa Simba, Mganda Emanuel Okwi yuko hatarini kuikosa mechi yao inayofuata dhidi ya Kagera Sugar FC. Simba SC iliyoweka kambi Visiwani Zanhzibar tangu jana mchana, itakuwa na kibarua kigumu mbele ya Kagera Sugar FC katika mechi ya raundi ya nane ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Ijumaa. Mratibu wa kambi ya Simba SC visiwani humo, Abdul Mshangama ameuambia mtandao huu kuwa Okwi anatarajiwa kujiunga na timu yao Alhamisi akitokea kwao Uganda alikoenda kwa ajili ya kufunga ndoa. Okwi alifunga ndoa juzi na amekuwa na desturi ya kutorejea katika klabu anazosajiliwa wakati wa sherehe za Krismas ambayo ni siku yake ya kuzaliwa mwaka 1992. “Okwi anatarajia kuja kuungana nasi Alhamisi,” amesema Mshangama. Kama Okwi atarejea nchini siku hiyo ya Sikukuu, nbi wazi kwamba hatakuwa na nafasi ya kukipiga katika kikosi cha kocha Mzambia Patrick Phiri cha Simba SC dhidi ya Kagera Sugar FC

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MSANII NASEEB ABDUL ‘DIAMOND’ IKULU, AWAPONGEZA YEYE NA IDRIS SULTAN KWA KUILETEA SIFA TANZANIA DESEMBA 23, 201

Image
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha msanii Naseeb Abdul “Diamond”  na  kumpongeza kwa kushinda tuzo tano za muziki za kimataifa mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 23, 2014  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa msanii Naseeb Abdul “Diamond” wakati akimuonesha moja ya tuzo kati ya  tuzo tano za muziki za kimataifa alizoshinda mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 23, 2014. kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo  Profesa Hermas Mwansoko. Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa msanii Naseeb Abdul “Diamond”  juu ya ushindi wake wa  tuzo tano za muziki za kimataifa mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 23, 2014 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na msanii Naseeb Abdul “Diamond”  alipomkaribisha Ikulu   kumpongeza kwa kushinda tuzo tano za muziki za kimataifa mwaka huu, Ikulu jiji

KATIBU MKUU KIONGOZI AMSIMAMISHA KAZI KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHARTI NA MADINI

Image
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Yohana Sefue, amemsimamisha kazi kwa muda Ndugu Eliakim Maswi, Katibu Mkuu ya Wizara ya Nishati na Madini, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake, kama ilivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete. Balozi Sefue amemsimamisha kazi Ndugu Maswi kuanzia leo, Jumanne, Desemba 23, 2014, kwa kutumia madaraka aliyonayo kama Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu. Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Balozi Sefue mjini Dar es Salaam imesema kuwa amechukua hatua hiyo “Kwa mujibu wa Kifungu 4(3) (d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Na. 8 ya mwaka 2002 (kama ilivyorekebishwa)” ambapo “Katibu Mkuu Kiongozi ndiye Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.” Badala yake, Balozi Sefue amesema kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi C. Mwihava atakaimu nafasi ya Katibu Mkuu, Wizara y

MWANAFUNZI AMWAGIWA MAFUTA YA MOTO BAADA YA KUFUMANIWA NA BOYFRIEND WA RAFIKI AKE.

Image
Mwanafunzi wa chuo kimoja alimwagiwa mafuta ya moto na rafiki yake kipenzi baada ya kumkuta na boyfriend wake wakifanya mapenzi. Ilikuwa ni siku ya ijumaa Nasra alipokuwa akitoka darasani na kurejea hostel alipokea sms ikisema "Nenda kwa Rafiki yako kipenzi Naima kuna Bonge la Surprize, tafadhali usikose nenda sasa hivi" Nasra aliamua kuchukua pikipiki hadi kwa rafiki yake alipofika tu alikuta viatu vya boyfriend yake nje, akashtuka kwanza kwani sio kawaida ya jamaa huyo kwenda kwa Naima bila ya kuwa na Nasra, Nasra alijaribu sana kugonga lakini hakufunguliwa, na baadae aliamua kupiga simu zote mbili ya rafiki yake na ya boyfriend wake pia zote zikaita tu bila kupokelewa, Alikaa pale nje hadi majira ya saa sita usiku, ambapo alishajua kunakitu kinaendelea. Muda ulivyozidi kwenda  Nasra alitoka na kwenda kuchukua marafiki zake wengine wawili, aliporudi alikuta bado hawajatoka ndani. Mpaka majira ya saa saba hivi usiku, Nasra akiwa amebeba mafuta ya moto

SHILOLE AOGESHWA KAMA MTOTO MDOGO VILE KWENYE PARTY YAKE

Image
Shilole akijiandaa kukata keki pembeni ni Steve Nyerere. Said Fella na Faraji wakimmwagia Shilole maji na bia. Shilole akipiga kelele baada ya kumwagiwa maji na bia. ….akiogelea. Sehemu ilipofanyikia sherehe hiyo. Msanii Mziwanda ambaye ni mpenzi wa Shilole akiwa na Steve Nyerere. Shilole akiwa na wadau. Wadau mbalimbali wakiwa kwenye sherehe hiyo.MWANADADA Zuwena Mohamed ‘Shilole’ jana alidondosha bonge la pati alipokuwa akisherekea siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika katika moja ya apatiment iliyopo nyuma ya Baraka Plaza Mikocheni, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wasanii kama Ditto, Linah, Chegge, Mhe. Temba, Shetta, Mziwanda pamoja na wadau wengine.