Posts

Faida za kiafya za kunywa maji ya moto

Image
NJIA SITA ZA KUNYWA MAJI YA MOTO ZINAZOTIBU MWILI WAKO. Kunywa kikombe kimoja cha maji ya moto kila asubuhi inaweza kukutibu mwili wako kwa kusaidia umeng’enywaji wa chakula na kuzuia kuzeeka mapema kabla ya wakati. Wengi wetu huianza asubuhi vyema kwa kikombe safi cha kawaha ya moto au chai ya moto kwa lengo la kuuchangamsha miili yetu baada ya kutoka kitandani. Pale tunakunywa maji, basi wengi wetu hupendelea kunywa ya baridi, lakini kutokana na watalaam wa afya wanavyosema,  tunafanya makosa kufanya hivyo. Mara nyingi unywaji wa maji moto au uvuguvugu, hususani majira ya asubuhi, inasaidia kuiponya miili yetu na kuitibu, kwa kusaidia kuongeza nguvu katika mmeng’enyo wa chakula ma kupunguza taka mwili ambazo zinaweza kuzuia kinga zetu kuwa katika hali yake nzuri ya mfumo sahihi. “matabibu wanasema na kushauri kunywa maji moto ama uvuguvugu nyakati za asubuhi, kila siku, sambamba na mchanyanyo wa maji ya limao, au chai ambayo haina madhara kwa mwili” anase

Vyakula 10 vinavyoongeza uwezo katika tendo la ndoa

Image
Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume na kuacha idadi ya wanawake wanaokabiliwa na tatizo hilo kwa mujibu wa uchunguzi kubaki na asilimia 13. Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili. Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina kumi ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa. Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo: PILIPILI Pilipili zilizocheshwa zimetajwa kuwa na uwezo wa kusaidia msukumo wa usambazaji damu mwilini, ambao kwa kiasi kikub

Jinsi ya kudumisha uzito wa kawaida wenye afya

Image
Kudumisha uzito wa mwili bora unakusaidia wewe kutokana na hatari Unapaswa kufahamu ya kwamba unakula zaidi kama unazindisha kulingana na vile mwili wako unavyohitaji. • Unapokula zaidi na haufanyi aina yeyote ya mazoezi ya kujenga mwili, unaweza kupata uzito au unene mwingi kupita kiasi. • Kuishi kwa ile hali ya kuwa na uzito wa mwili vyema, ni muhimu kwako kula chakula bora na kwa kiasi. • Kuna njia muafaka ambazo unaweza kufanya ili kudumisha ule uzito wa mwili ambao unaofaa, kama vile:- - kupunguza jinsi unavyokula mafuta na sukari - kupunguza kiasi cha chakula - kuacha kula tu mradi umeshiba - kuongeza kufanya mazoezi ya mwili • Kudumisha uzito wa mwili bora unakusaidia wewe kutokana na hatari kama vile:- - kuumwa na viungo vya mwili - kupandwa na damu - ugojwa wa sukari - ugojwa wa moyo - ugojwa wa saratani manyandahealthy

madhara ya sabuni za kurudisha ubikra!!

Image
  WANAWAKE wameshauriwa kuacha kutumia sabuni za kunawia sehemu za siri ambazo hudaiwa kurejesha ubikira kwani zina madhara makubwa ikiwemo kusababisha kansa ya shingo ya kizazi. Mkaguzi wa Dawa na Mfamasia wa Manispaa ya Dodoma Daria Mwanuka alisema hayo mwishoni mwa wiki katika mahojiano na mwandishi wa habari hizi wakati wa uteketezaji dawa, vipodozi na vyakula visivyofaa kwa matumizi ya binadamu.   Kazi hiyo ilifanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Kati. Alisema kumekuwa na sabuni mbalimbali ikiwamo Kaisiki ambapo wanaoziuza wanadai zimekuwa zikisababisha bikira iliyopotea kurudi kitu ambacho si kweli. "Sabuni hizo zinapunguza tu majimaji yaliyo sehemu za siri za mwanamke jambo ambalo husababisha wakati wa kufanya mapenzi mwanaume kupata ugumu kwenye muingiliano kwa vile mwili unakuwa umekataliwa kutoa maji na hivyo kuleta michubuko kitu ambacho ni hatari hasa wenye maambukizi ya magonjwa," alisema.   Alisema mich

BREAKING NEWS: WAJERUHIWA KATIKA VURUGU DUMILA.

Image
WATU kadhaa wamejeruhiwa katika vurugu zilizotokea jioni hii huko Dumila mkoani Morogoro kati ya wakulima na wafugaji ambapo polisi wameingilia kati na kutumia mabaomu ya machozi kutuliza ghasia hizo.  Chanzo cha vurugu hizo kinadaiwa kuwa ni kukatwa mkono kwa mkulima mmoja aishiye Kijiji cha Mketeni wilayani Kiloasa wakati akibishana na mfugaji ambaye ni kabila la Kimasai kuhusu eneo la kulishia mifugo.  Kufuatia kitendo hicho cha kukatwa mkono, mkulima huyo aliwafuata wenzake na kuwapa taarifa ambapo walikusanyika na kuanzisha vurugu dhidi ya wafugaji wa eneo hilo.Baada ya kuona kuwa bado haitoshi na baadhi ya wafugaji kukimbia, wakulima walimalizia hasira zao katika Barabara ya Morogoro - Dodoma ambapo waliamua kuifunga kwa takribani masaa mawili huku wakichoma matairi Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) waliingilia kati na kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wakulima ambao pia walikuwa tayari wamevamia baadhi ya nyumba za kulala wageni zinazomili

DUNIA IMEKWISHA: BINTI AKUTWA AKIFANYA JARIBIO LA KUMLA MTOTO WAKE BAADA YA KUJIFUNGUA!

Image
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Li Zhenghua 24, amekutwa akifanya jaribio la kumla Mtoto wake aliyejifungua siku chache zilizopita, baada ya kumkuta taya yake ikiwa imenasa kuzunguka Mkono wa Mtoto wake.  Tukio hilo la ajabu lilitokea katika Hospitali iliyoko Shenzhen Kusini mwa jimbo la Guangdong, China ambapo mwanamke huyo alifikishwa kujifungua na baadaye wahudumu wa Hospitali kufanya jitihada za kutafuta ndugu zake.  Hata hivyo mwanamke huyo akiwa na siku ya tatu Hospitalini hapo alikutwa na nesi akiwa katika jaribio la kumng’ata mtoto ambapo madaktari walitumia nguvu na kufanikiwa kumuokoa mtoto huyo ambaye tayari alikuwa na jeraha mkononi.

MAADHIMISHO YA MIAKA 53 YA UHURU WA TANZANIA BARA YAFANA JIJINI DAR LEO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mikono wananchi waliofurika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara akiwa katika Gari maalum liliozunguuka katika uwanja huo leo.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Davis Mwamunyange. Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikitoa salamu ya heshma wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam leo katika sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lilioandaliwa katika sherehe za kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mri

BILIONEA EMAMI WA NIGERIA AMPATIA TAYO DOLA 350,000/= KAMA BACKUP BAADA YA KUSHINDWA KWENYE SHINDANO LA BBAHOTSHOTS

Image
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255765957698 au email: pharsnyanda@gmail.com .  Tunashukuru kwa ushirikiano wenu. Mshindi wa pili wa  BBAHotshots, Tayo Folarin   Baada ya East Africa yote kuinua shangwe kubwa siku ya Jumapili Desemba 7 kusherehekea ushindi wa nguvu alioupata Mtanzania   Idris   kwenye  BBAHotshots , kulikuwa na story kwenye mitandao ya kijamii ambazo hazikuwapendeza watu wengi kwani ilionekana kama baadhi ya watu kama Nigeria hawakuwa na amani kuukosa ushindi huo na kuuona ukija Tanzania. Bilionea  Ayiri Emami Sasa mpya kutoka Nigeria ni kwamba bilionea mmoja hakupendezwa kumuona mwakilishi wao Tayo akiambulia patupu, bilionea huyo  Ayiri Emami  amempatia  Tayo Folarin  pesa ambazo ni zaidi hata ya kiwango ambacho kimetolewa na  BBAHotshots  kwa mshindi wa kwanza.  Tunawafahamu mabilionea wachache k

BREAKING NEWS: WATU WANNE WAFARIKI KATIKA AJALI YA HELIKOPTA HUKO GOMBO LA MBOTO JIJINI DAR!

Image
Muonekano wa Helikopta eneo la Gonga la Mboto jijini Dar.  Wananchi wakiwa eneo la tukio baada ya Helikopta kuanguka. Helikopta imeanguka leo eneo la Gongo la Mboto, Moshi Bar jijini Dar, kuna watu wanadaiwa kufariki dunia lakini polisi hawajatoa taarifa rasmi juu ya tukio hili.

HATIMAYE LADY JAY DEE AKIRI KUMUACHA MUMEWE GADNER HABASH - MSIKILIZE HAPA

Image
Hatimaye Lady Jaydee amethibitisha kwa kauli yake mwenyewe kuwa ndoa yake na mtangazaji mkongwe wa redio, Gadner G Habash imevunjika. Akiongea leo kwenye Exclusive Friday ya kipindi cha Sunrise cha Times FM, Jaydee amesema ni yeye ndiye aliyeamuacha Gadner. Kwenye mahojiano hayo, Jide alizungumzia kuwa kwenye uhusiano na mtu aliyekuwa akimpiga mara kwa mara licha ya kutomtaja moja kwa moja kuwa ni Gadner lakini alisema alikuwa akiteswa. Kabla ya kuamua kuusema ukweli huo, Jide aliweka wazi kuwa siku zote amekuwa akiepuka kuongea masuala yake binafsi kwenye vyombo vya habari.“Kitu kimoja ambacho ningependa watu wafahamu, mimi sio mtu ambaye huwa napenda kuongea maisha maisha yangu kwenye media, kwenye magazeti au wapi,” alisema. “Na ndio maana lolote ambalo linaendelea ndani ya nyumba yangu au kwenye maisha yangu, sijawahi kulitoa nje. Ni watu wanaongea chochote wanachohisi, chochote wanachotaka kusema.  SOMA ZAIDI>>>>

ANGALIA PICHA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA ARUSHA LEO

Image
Simanzi zimetanda jiji la Arusha baada ya watu zaidi ya 15 kufa katika ajali iliyotokea eneo la Tengeru. Akiongea na mwandishi wetu mmoja ya mashahidi aliyefika eneo la tukio na hospitali ya Mount Meru amesema ajali ilitokea majira ya saa kumi jioni huko maeneo ya Sadec-Darajani -Tengeru iliyohusisha gari la abiria aina ya Hiace linalobeba watu toka Usa-River kwenda Arusha mjini na Lori la mafuta.Aliongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa hiace (gari la abiria) iliyokuwa ikijaribu kupita magari mengine ndiyo akakutana uso kwa uso na lori hilo. Habari kamili zitawajia punde.