BREAKING NEWS: WAJERUHIWA KATIKA VURUGU DUMILA.

WATU kadhaa wamejeruhiwa katika vurugu zilizotokea jioni hii huko Dumila mkoani Morogoro kati ya wakulima na wafugaji ambapo polisi wameingilia kati na kutumia mabaomu ya machozi kutuliza ghasia hizo. 

Chanzo cha vurugu hizo kinadaiwa kuwa ni kukatwa mkono kwa mkulima mmoja aishiye Kijiji cha Mketeni wilayani Kiloasa wakati akibishana na mfugaji ambaye ni kabila la Kimasai kuhusu eneo la kulishia mifugo. 

Kufuatia kitendo hicho cha kukatwa mkono, mkulima huyo aliwafuata wenzake na kuwapa taarifa ambapo walikusanyika na kuanzisha vurugu dhidi ya wafugaji wa eneo hilo.Baada ya kuona kuwa bado haitoshi na baadhi ya wafugaji kukimbia, wakulima walimalizia hasira zao katika Barabara ya Morogoro - Dodoma ambapo waliamua kuifunga kwa takribani masaa mawili huku wakichoma matairi
Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) waliingilia kati na kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wakulima ambao pia walikuwa tayari wamevamia baadhi ya nyumba za kulala wageni zinazomilikiwa na wafugaji eneo hilo na kufanya uharibifu. 
Majeruhi katika vurugu hizo wamepelekwa hospitali kwa huduma ya kwanza.

Comments

Popular posts from this blog