Faida za kiafya za kunywa maji ya moto
NJIA SITA ZA KUNYWA MAJI YA MOTO ZINAZOTIBU MWILI WAKO. Kunywa kikombe kimoja cha maji ya moto kila asubuhi inaweza kukutibu mwili wako kwa kusaidia umeng’enywaji wa chakula na kuzuia kuzeeka mapema kabla ya wakati. Wengi wetu huianza asubuhi vyema kwa kikombe safi cha kawaha ya moto au chai ya moto kwa lengo la kuuchangamsha miili yetu baada ya kutoka kitandani. Pale tunakunywa maji, basi wengi wetu hupendelea kunywa ya baridi, lakini kutokana na watalaam wa afya wanavyosema, tunafanya makosa kufanya hivyo. Mara nyingi unywaji wa maji moto au uvuguvugu, hususani majira ya asubuhi, inasaidia kuiponya miili yetu na kuitibu, kwa kusaidia kuongeza nguvu katika mmeng’enyo wa chakula ma kupunguza taka mwili ambazo zinaweza kuzuia kinga zetu kuwa katika hali yake nzuri ya mfumo sahihi. “matabibu wanasema na kushauri kunywa maji moto ama uvuguvugu nyakati za asubuhi, kila siku, sambamba na mchanyanyo wa maji ya limao, au chai ambayo haina madhara kwa mwili” a...